HOJA Kwanini wenye nyumba Tanzania wanalazimisha kodi iwe miezi mitatu au sita?

HOJA Kwanini wenye nyumba Tanzania wanalazimisha kodi iwe miezi mitatu au sita?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Katika jambo la hovyo ambalo sijawahi kulielewa ni hili la wenye nyumba kudai kodi miezi mitatu mpaka sita.

Nini hasa kinachosababisha mwenye nyumba atake kodi ya miezi mitatu au sita?! Duniani kote kodi huwa inalipwa mwezi mmoja mmoja na pesa ya tahadhari ya ziada inawekwa ni mwezi mmoja.

Serikali inahitajika kuingilia kati kudhibiti huu unyonyaji wa kijinga wa watu wajinga.
 
Njaa kivipi mkuu? Mimi nafikiri ni ujinga wa wapangaji zaidi na serikali kushindwa ku regulate biashara ya upangaji nyumba/fremu.
Wengi wanapenda kuchukua kwa mkupuo ili kumudu gharama za maisha wanaona kuchukua ya mwezi ni kama vile haiwatoshi ndiyo maana wengi wanapenda wachukue ya miezi 6 na wengine wasivyo na aibu hata kabla ya hiyo miezi sita haijaisha wanakuja kudai ushahidi ninao nimeishi sana nyumba za kupanga
 
mi naona iko poa tu maana unapata na gape la kuweka mambo yako sawa sio kila mwezi unalipia,, ila mi pesa inayo niuma ni ya dalali wanakata sana wale majamaa
Aisee hao madalali ni hatari. Yaani wanakula kodi ya mwezi mzima kama ilivyo.

Kama ni sehemu ya biashara hapo unakuta hujajua hata biashara yenyewe itakwendaje.
 
yani ni matapeli mno hata kwenye kupanga bei kwenye frame mpya wanahusika pia kuongeza vi chenchi ili wapate cha juu
Kuna sehemu niliwahi kwenda kuuliza Frem zilikuwa mpya nikichokutana nacho yule mwenye fremu kwa mwezi kodi ni laki na nusu lakini alichokifanya dalali kalipia yeye kodi ya miezi 6 halafu anaipangisha tena ila sasa kajiwekea kodi yake yaani yake kwa mwezi laki tano.

Niliduwaa kiufupi.
 
Katika jambo la hovyo ambalo sijawahi kulielewa ni hili la wenye nyumba kudai kodi miezi mitatu mpaka sita.

Nini hasa kinachosababisha mwenye nyumba atake kodi ya miezi mitatu au sita?! Duniani kote kodi huwa inalipwa mwezi mmoja mmoja na pesa ya tahadhari ya ziada inawekwa ni mwezi mmoja.

Serikali inahitajika kuingilia kati kudhibiti huu unyonyaji wa kijinga wa watu wajinga.
Kuna ambao sio waaminifu.
Lakini anakuwa amekusajdia kufanya mambo mengine ndani ya hiyo miezi sita utakayokuwa umelipa.
 
WAHI SASA KABLA BEI HAIJAPANDA, USICHELEWE KUWEKA ODA YAKO

1. ✅ Banner 10,000 / meter
2. ✅ Stika 9000 / meter
3. ✅ Vitabu vya risiti 4000 Tsh size A6
4. ✅ Business cards pc100 Tsh 20,000 tu
5. ✅ Tshirt Tsh 2500 kuanzia pc10
6. ✅ Bango ya 3D Tsh 450,000 Tsh / meter
7. ✅ Rollup banner 120,000 Tsh
8. ✅ Kitambulisho ngumu 4000 Tsh
9. ✅ Vipeperushi pc100 size A6 Tsh 20,000
10. ✅ Kikombe Tsh 8000

Tunapatikana Nyamwezi na Muhoro
📲0675-545-795
 
Katika jambo la hovyo ambalo sijawahi kulielewa ni hili la wenye nyumba kudai kodi miezi mitatu mpaka sita.

Nini hasa kinachosababisha mwenye nyumba atake kodi ya miezi mitatu au sita?! Duniani kote kodi huwa inalipwa mwezi mmoja mmoja na pesa ya tahadhari ya ziada inawekwa ni mwezi mmoja.

Serikali inahitajika kuingilia kati kudhibiti huu unyonyaji wa kijinga wa watu wajinga.
Ningepata wapangaji wanaojitambua kama wa nchi wanazolipa kodi kwa mwezi, ningechukua kodi kwa mwezi maanake idadi ya units nilizonazo hata nikichujua kwa mwezi inatosha.
Lakini, kwa wabongo hawa kuchukua kodi kwa mwezi maana yake utasumbuana na mtu kila mwezi. Wacha tufanye kwa miezi sita at least.
 
Back
Top Bottom