Kwanini wizara ya ardhi DSM iliamua kupima mbuga na mabonde yote ya kulima mpunga kuwa sehemu ya makazi?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Ukizunguka mkoa wa Dar es salam! Maeneo yote yenye chemchem za maji ndiyo yaliyopimwa viwanja rasmi kwa ajili ya makazi ya binadam!

Je; ni kwanini wizara iliacha kupima maeneo salama ikakimbilia kupima mashamba ya mpunga kuwa makazi?

Mbezi beach yote, kunduchi, ununio na mbweni kote huku yalikuwa mashamba ya mpuga yenye chemchem za maji, ilikuwaje serikali ya ikaamua kupima maeneo hayo na kuacha maene safi ambayo yangefaa kujengwa na hata wenye vipato vidogo?

Huko kigamboni kibada kulikopimwa Block E kote huko kuna jaa maji na kumepimwa rasmi kwa ajili ya makazi! Je hawa wasomi walitumia akili gani kuelekeza nguvu kubwa kupima maeneo hayo na kuacha sehem salama kwa ajili ya makazi?

Au wizara ya ardhi yote imejaa vijana kwa kauli ya ndugai! Kiasi kwamba busara za wazee zilikosekana?
 
Posta mpya yote yalikuwa mashamba ya mkonge na MAENEO MAKUBWA ya temeke yalikuwa mashamba ya mpunga ikiwemo maeneo ya Mwananyamala YOTE yalikuwa mashamba ya mpunga

Msasani kulikuwa madimbwi ya kugema chumvi.Kulikuwa na mabwawa ya kuvuna chumvi na mashamba ya mipunga pia
 
Kweli kabisa
 
Ukizunguka mkoa wa Dar es salam! Maeneo yote yenye chemchem za maji ndiyo yaliyopimwa viwanja rasmi kwa ajili ya makazi ya binadam!

Je; ni kwanini wizara iliacha kupima maeneo salama ikakimbilia kupima mashamba ya mpunga kuwa makazi?

Mbezi beach yote, kunduchi, ununio na mbweni kote huku yalikuwa mashamba ya mpuga yenye chemchem za maji, ilikuwaje serikali ya ikaamua kupima maeneo hayo na kuacha maene safi ambayo yangefaa kujengwa na hata wenye vipato vidogo?

Huko kigamboni kibada kulikopimwa Block E kote huko kuna jaa maji na kumepimwa rasmi kwa ajili ya makazi! Je hawa wasomi walitumia akili gani kuelekeza nguvu kubwa kupima maeneo hayo na kuacha sehem salama kwa ajili ya makazi?

Au wizara ya ardhi yote imejaa vijana kwa kauli ya ndugai! Kiasi kwamba busara za wazee zilikosekana?

Hakuna sehemu duniani palipo kamilika ila mwanadamu hana weza kupatengeneza mfano dubai
IMG_4653.jpg

Mfano poland
IMG_4654.jpg

Yote haya ni taaluma na jinsi ya kupatengeneza achana na hapo nchi kama japani kuwa na majengo mazuri lakini ndio inaongoza kwa matetemeko
IMG_4655.jpg

Hata leo tukikata dodoma kuwa ya kijani kama arusha inawezekana
IMG_4656.jpg

Kazi kwako
 
Hakuna sehemu duniani palipo kamilika ila mwanadamu hana weza kupatengeneza mfano dubai View attachment 1754951

Mfano poland
View attachment 1754958

Yote haya ni taaluma na jinsi ya kupatengeneza achana na hapo nchi kama japani kuwa na majengo mazuri lakini ndio inaongoza kwa matetemeko
View attachment 1754964

Hata leo tukikata dodoma kuwa ya kijani kama arusha inawezekana
View attachment 1754967

Kazi kwako
Mfano uliouweka hauko sawa! Hayo majengo ni serikali na makampuni yenye fedha ndiyo yaliyowekeza hapo!
Unataka kuniambia Dubai walivyojenga baharini na sisi tupime viwanja baharini kwa ajili ya makazi?
Tofautisha serikali na ujenzi wa binafsi kwa ajili ya makaz
 
Ukizunguka mkoa wa Dar es salam! Maeneo yote yenye chemchem za maji ndiyo yaliyopimwa viwanja rasmi kwa ajili ya makazi ya binadam!

Je; ni kwanini wizara iliacha kupima maeneo salama ikakimbilia kupima mashamba ya mpunga kuwa makazi?

Mbezi beach yote, kunduchi, ununio na mbweni kote huku yalikuwa mashamba ya mpuga yenye chemchem za maji, ilikuwaje serikali ya ikaamua kupima maeneo hayo na kuacha maene safi ambayo yangefaa kujengwa na hata wenye vipato vidogo?

Huko kigamboni kibada kulikopimwa Block E kote huko kuna jaa maji na kumepimwa rasmi kwa ajili ya makazi! Je hawa wasomi walitumia akili gani kuelekeza nguvu kubwa kupima maeneo hayo na kuacha sehem salama kwa ajili ya makazi?

Au wizara ya ardhi yote imejaa vijana kwa kauli ya ndugai! Kiasi kwamba busara za wazee zilikosekana?
Huwezi kuogopa kupima eneo la makazi kisa ni mashamba ya mpunga,watu wanazaliana,miji inapanuka
La muhimu ni kuichora nyumba na kuijenga kitaalam
 
Tatizo ni kukosekana kwa proper drainage systems, zikiwepo mbona hakuna shida
 
Huwezi kuogopa kupima eneo la makazi kisa ni mashamba ya mpunga,watu wanazaliana,miji inapanuka
La muhimu ni kuichora nyumba na kuijenga kitaalam
Pale bondeni jangwani kwanini waliwafukuza wale watu badala ya kuwapimia waishi palepale bondenj kama ni kweli mji hupanuliwa bondeni
 
KWANINI WALIWATIMUA WALE MASIKINI WALIIOJENGA PALE BONDENI JANGWANI Kama hoja ni Drainage tu?
Hao unaosema maskini pale jangwani
Hukuona adha waliyokuwa wanapata kila mwaka!
Na wale kabla walipewa viwanja huko mwagwepande wakaviuza wakarudi tens
Hapo jangwani
Sasa hapo nani wa kulaumiwa

Ova
 
Si umesema bondenj hapana shida, cha mhimu ni drainage, kwanini wasingeweka hiyo drainage badala yake wakaamua wao kujenga ofisi za mwendokas kwa fedha za masikin walewale eneo lile lile walilosema halifai?
 
KWANINI WALIWATIMUA WALE MASIKINI WALIIOJENGA PALE BONDENI JANGWANI Kama hoja ni Drainage tu?
Kuna tofautu kati ya mabonde na flat lands, shida ya ukanda wa Mbezi mpaka Mbweni ni kuwa flat na mvua zikinyesha maji hayatembei, drainage ikiwa sawa, bahari haiko mbali kupeleka maji. Sasa bonde unafanya nalo nini? Maana ndio drainage yenyewe, huwezi kujenga kwenye njia maji
 
Pale bondeni jangwani kwanini waliwafukuza wale watu badala ya kuwapimia waishi palepale bondenj kama ni kweli mji hupanuliwa bondeni
Ule ni mto sio bonds,ni kinyume Cha Sheria kupima viwanja kwenye lango la mto
 
Back
Top Bottom