Maana yake sasa wamemwona kwa jinsi ya mwili wa mwanadamu...
Uungu wa Yesu ulianza vipi?
Tangu mwishoni mwa Karne ya tatu ulitokea mvutano mkubwa sana katika Kanisa kuhusu mafundisho ya Maaskofu kuhusu Cheo cha Yesu na Mariamu. Mabishano hayo yaliendelea kwa kasi kila mtu alimtafsiri Yesu kivyake.
Hali ilizidi kuwa mbaya sana mnamo mwaka 325 AD ilimlazimu Mfalme wa wakati huo Konstantine awaite Maaskofu wote wakati huo Kanisa lilikuwa na Maaskofu 300 ili waje waelewane na kuwa na msimamo mmoja lakini ni sehemu tu ya Maaskofu walio hudhuria.
Wakati huo Konstantine alikuwa Mpagani mwabudu jua kwa wazazi wake,soma
The Early Church. Kwa hiyo aliwakusanya Maaskofu ili kuletautulivu katika utawala wake. Mfalme huyu ndiye aliyekuwa Mwenyekiti namtendaji muhimu katika mkutano huo.
Majadiliano yalikuwa makali sana iliwachukua miezi miwili bila mwafakawowote ndipo Mfalme aliingilia kati na kutoa uamuzi wake na ndiyo ilibidi ufuatwe, yeye aliwaunga mkono wale waliosema Yesu ni Mungu kweli na mtu kweli ni mwana wa Mungu aliye sawa na Baba yake Mungu, pia Mariamu ni mamawa Mungu pia ni Malkia wa Mbinguni. Kwa hiyo Mfalme Mpagani akawa ameshiriki sehemu ya maana sana katika kumpandisha cheo toka kuwa mtume hadi kuwa Mungu kamili na Mariamu akawa mama wa Mungu.
Kama nilivyosema Kostantini alikuwa Mpagani hivyo, hakuwa na ujuzi kamili juu ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa katika Thiolojia ya Kigiriki alilojua ni kuleta amani katika utawala wake tu. Soma
A. Short. History of Christian Doctrine.
Uamuzi huo ulikuwa ni wa kijeshi siyo hiyari hapo Maaskofu waliomuhofu Mfalme walitia sahihi zao lakini wengine walikataa waliokataa waliteswa sana na kunyanyaswa hadi waliuwawa kikatili sana.
Mkutano huo ulikuwa katika mji wa NICEA na uliitwa Baraza la NICEA mwaka325 AD.
Uamuzi wa NICEA haukuleta utulivu kama walivyotegemea bali vurugu zahali ya juu, mateso na mauaji yalikuwa makubwa sana hasa kwa wale waliokataa fundisho hilo la Yesu kuwa Mungu na Mariamu mama wa Mungu, Malkia na Mbinguni.
Mateso na mabishano yalienea zaidi huko Ufaransa ya Kusini, Hispania na Ujerumani miaka mingi iliyopita hasa baada ya Patano la Milano ambapo Kostantini na Kanisa walishirikiana vizuri Makanisa yakajengwa kwa gharama za serikali hapo mateso yalizidi watu wengi waliuwawa vibaya hovyohovyo tu.
Ilipofika mwaka 381 A.D. mambo yalizidi kuwa mabaya sana hapo Mfalme aliyekuwa anamiliki wakati huo Theodosius aliitisha tena mkutano wa Maaskofu wote katika mkutano huo Mfalme alitangaza rasmi kuunga mkono uamuzi waBaraza la NICEA.
Pia walikubaliana Roho Mtakatifu aunganishwe katika utatu Mtakatifu hapo ndipo imani ya utatu wa Mungu Mmoja ilianza ili kuwathibiti wale waliokuwa wanapinga ilitolewa amri kwamba hakuna ruksa kwa mtu yeyote kupinga au kutafsiri neno linalohusu Biblia au mapokeo soma. Hati ya Funuo ya Vaticani 10:4 imeandikwa:- Lakini haki ya kutoa tafsiri thabiti ya neno la Mungu au mapokeo imekabidhiwa mamlaka ya kifundishi ya Kanisa Katoliki peke yake tu. Mkutano huo unaitwa Baraza la Kostantinopol. Mwaka 381 A.D.
Historia inaendelea kutueleza kwamba Kanisa liliendelea kuwatesa nakuwauwa wote waliojaribu kupinga au kufafanua vingine mamlaka ya Kanisa ikishirikiana na serikali, watu waliteswa kwa njia nyingi, mfano:- wapo waliofungwa na kunyimwa chakula hadi kufa, wengine walitupwa kwenye zizi lililokuwa na wanyama wakali na kuliwa na wengine walilazimishwa kukalia vyuma vyenye moto, wengine walivalishwa shingoni mkufu wenye misumari yenye ncha kali baadaye misumari ilipigiliwa na kuingia shingoni hadi kufa. Wengine walibanwa na Koleo maalum Magotini na kuvunja miguu na kuwalazimisha wakubali mafundisho ya Kanisa la Roma.
Wapo waliochunwa ngozi ya mwili mfano wa mbuzi na walikufa kwa mateso mno. Uamuzi huu wakutisha ulikuwa unatimiza maneno ya Yesu Matayo 12:37-43.
Akasema azipandaye mbegu njema ni mwana wa Adamu lile Konde ni ulimwenguzile mbegu njema ni wana wa Mfalme, yale magugu ni wana wa yule mwovu aliyepandani Ibilisi mavuno ni mwisho wa dunia wavunao ni malaika kama vile maguguyanavyokusanywa na kuchomwa motoni ndivyo itakavyokuwa katika mwisho waDunia… mwenye masikio na asikie.
Uamuzi huo ulitimiza kweli magugu yalikuwa yamepandwa Ulimwenguni imaniya uongo iliingia kwa nguvu kama vile magugu yanavyoingia shambani na kuharibu ngano ndivyo ilivyo hadi leo hii fundisho hilo la uongo limekuwa ndiyo msingi mkubwa wa imani ya Kanisa Duniani pote.
Ipo njia inayoonekana kuwa sawa machoni mwa mtu lakini mwisho wake ni mauti mithali 14:12 Viongozi wa Kanisa waliona kwamba njia nzuri ya kumuheshimu Yesu ni kumpandisha Cheo toka Mtume wa Mungu hadi kuwa Mungu sawa Mungu Muumba vyote kabisa.
Mariamu akapandishwa kutoka mama wa Mtume Mtakatifu. Viongozi wakampandisha cheo cha mama wa Mungu nani Malkia wa Mbinguni!!! Viongozi hao inafaa wafungwe jiwe la kusagia shingoni sababu wamewakosesha watu hadi leo hii wanaendelea kuwakosesha kwa mafundisho ya uongo Marko 9:42. Ninakushauri uende Maktaba utaona vitabu na kurasa maelfu ambavyo wanathiolojia wamejitahidi sana kutoa fafanuzi mbalimbali na mitajo ya kila aina ili kupata ukweli wa mambo kuhusu utatu lakini huishia kuchanganyikiwa, na kuacha bila kuelewana hawapati ushahidi ulio.