Kwanini Yesu anaitwa Mungu? Sababu na ushahidi huu hapa

nukuu wanafunzi wa Yesu wakamuuliza kiama itakuwa lini ? Yesu akajibu hata mwana ajui ila baba ...wwnafunzi wake wakadhani kawaambia kuwa ajui siku ya kiama kumbe maana ya yale maneno yalikuwa ni mwili aujui ila nafsi yangu inajua ...baba ndiyo nafsi ya yesu
Sasa kama yesu ndiyo Baba pia na nafsi yake inajua kuhusu kiama,.. kwanini asiwajibu hao wanafunzi wake directly?

Kumbuka umesema Yesu ndiyo Baba,... na umesema jibu la hilo swali wanafunzi walililouliza, Baba analijua,.

Tunaomba ufafanuzi hapo.
 
Yesu ni kielelezo kasome ...ni mwalimu..walimu utoa mifano kwa vitendo tumia akili...ndani ya uislamu kuna sehemu Allah ana sema ...na nukuu 👉Na apa kwa yeye aliye ziumba mbingu na ardhi ....sasa ana apa kwa nani ikiwa yeye ndiye mungu aliye ziumba mbingu na ardhi

Hujajibu swali?
Yesu alikuwa anaenda kuomba kwa nani na tumeambiwa mara nyingine alikuwa anaomba hadi alalie huko?
"Watu wangu wata angamia kwa kukosa maarifa"
 
Hata msalabani aliomba ...baba wasamee kwa maana awajui watendalo ...jibu alikuwa anaomba kwa baba yani nafsi yake mwenyewe ....
 
Majibu yako ni sawa na mtu akuulize Raisi wa Tanzania anaitwa nani unajibu Raisi wa Kenya anaitwa Ruto!
"Watu wangu wata angamia kwa kukosa maarifa"
 
Hujajibu swali?
Yesu alikuwa anaenda kuomba kwa nani na tumeambiwa mara nyingine alikuwa anaomba hadi alalie huko?
Majibu yako ni sawa na mtu akuulize Raisi wa Tanzania anaitwa nani unajibu Raisi wa Kenya anaitwa Ruto!
"Watu wangu wata angamia kwa kukosa maarifa"
Aliomba kwa nafsi yake kama mungu a apavyo uapa kwa nafsi yake mwenyewe....nimekuambi hata katika uislamu mungu alisema na Apa kwa yeye aliye umba mbingu na ardhi ...maana yake hali apa kwa nafsi yake ..ndiyo hivyo hivyo kwa yesu uomba kwa nafsi yake mwenyewe maana ndiyo mungu mwenyezi allah
 
Je mungu ni mti au mungu ni moto? Mtume musa aliona mti uwakao moto akasema ni mungu ...hivyo mungu kuonekama kama mtu akumfanyi yeye kuwa mtu ...Yesu akuwa na nafsi ya binadamu bali nafsi ya Mungu.... hivyo nafsi ya mungu siyo mtu.

Mtume Mussa alipoona moto hakusema kuwa ni Mungu , usimpakazie. Yesu Hakuna mahali alisema yeye ni nafsi ya Mungu usimpakazie

Wewe ni mtu ninapokuita wewe ni nguruwe utakasirika vibaya sana, hivyo hivyo Mungu kumwuita Yesu yaani ni kiumbe chake anakasirika vibaya sana na ni shirki kubwa ambayo hasamehe ameweka wazi kabisa
 
Mtume Mussa alipoona moto hakusema kuwa ni Mungu , usimpakazie. Yesu Hakuna mahali alisema yeye ni nafsi ya Mungu usimpakazie
Siyo tu akusema...bali huo mti uwakao moto ulijitambulisha wenyewe kwake kuwa ni mungu wa Ibrahim mungu wa isaka mungu wa yakobo .....maana musa angesema yeye tu kuwa huyo ni mungu mngesema hata mitume wanaweza kukosea lakini aliye sema ni mungu mwenyewe kabla ya musa kusema...na musa akasema je nikiwaendea wana wa Israel na kuwaambia kuwa mungu wa baba zetu kanitokea awata nisadiki ndipo mungu akamwambia una nini mikononi mwako musa akasema nina fimbo ...nakupewa ishara akaambiwa akazifanye mbele ya wazee waisrael kwanza nao watamsadiki.
 
ungaliweka Aya kuthibitisha maneno yako kuwa moto alisema kuwa Mimi ni Mungu
 
Yohane 20:17

Yesu akamwambia, “Usinishike; sijaenda bado juu kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu uwaambie: Naenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.”
Ndugu yangu, tafsiri sahihi ya Andiko hilo inahitaji kuangalia muktadha mzima wa Biblia. Yesu aliposema 'Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu,' hakukana Uungu wake. Alikuwa akizungumza kama Mwana wa Mungu aliyekuwa katika hali ya kibinadamu(Mathayo 26:64, Wafilipi 2:6-8).

Unaposoma Biblia, usisome mstari mmoja tu ukaishia hapo. Angalia mistari yote hii inavyothibitisha kuwa Yesu ni Mungu:
  1. Yohana 1:1, 14 – ‘Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu.’
  2. Yohana 10:30 – ‘Mimi na Baba tu umoja.’
  3. Wakolosai 2:9 – ‘Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.’
  4. Tito 2:13 – ‘Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu.’
 
ungaliweka Aya kuthibitisha maneno yako kuwa moto alisema kuwa Mimi ni Mungu
Unataka tu kunisumbua kama waislamu wenzako wanavyo fanyaga ..nikileta aya wanakimbia uzi...kasome upya msahafu wote na injili na biblia yote kabla ya kuja hapa kubisha mambo....je nikileta haya na maandiko utakubali kuwa yesu ni mungu kwenye nafsi?
 
Ni kuwa huna Aya ambayo inayosema Mungu ni kichaka cha moto hapa upp JF na Kama wewe ni mwalimu shuleni basi hufai kabisa
 
Tatizo linakuja kwenye kuelimisha ng'ombe...kazi sana kuelimisha ng'ombe...kwani wewe ujui kuwa kuona ni mlango mmoja tu wa fahamu ....musa alisikia sauti ya mungu ni mlango mwingine wa fahamu wa kusikia ...mungu anaweza kuonekana kama kitu chochote atakavyo yeye ...labda Allah ndiyo dhaifu awezi kuonekana atakavyo
 
Yesu ni Mungu:
Mda flani pendelea kusikiliza kuliko kusikilizwa.

Yn 8:40

Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo.
 
Mda fulani pendelea kutafakari Maandiko kuliko kunukuu tu mistari.

Mtu gani anayeweza kutembea juu ya bahari? Mtu gani anayeweza kusema akifa atafufuka siku ya tatu? Mtu gani anayeweza kubadili maji yakawa divai?

Katika Andiko ulilonukuu Yesu alikuwa akiongea kama Mwanadamu. Alikuwa Mungu aliyevaa ubinadamu. Ndio maana aliitwa Emanueli. Isitoshe Mungu ana Nafsi 3: Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu(Mt 28:19). Hivyo usishangae kusikia Mungu Mwana anaongea na Mungu Baba.

Mwapotea kwakuwa hamyajui Maandiko(Mt 22:29).
 
Unaweza kutuletea Aya Yesu anasema Mimi ni Mungu ninayeongea Kama mwanadamu ?
 
Back
Top Bottom