Kwanini Yesu anaitwa Mungu? Sababu na ushahidi huu hapa

Kwanini Yesu anaitwa Mungu? Sababu na ushahidi huu hapa

Kulingana na yohana "hapo mwanzo"alikuwa anaongelea kuhusu mbigu na nchi?
au alikuwa anaongelea mwanzo wa neno na mungu!?
Swali lako nililijibu nikidhani umeuliza kuhusiana na kitabu cha Mwanzo(Genesis). Hata hivyo kitabu cha Yohana 1:1 hakisemi kwamba Yesu alianza kuwepo wakati huo, bali kinaeleza kwamba Yesu(Mungu Mwana) alikuwepo hata wakati wa huo mwanzo wa uumbaji wenyewe, akiwa pamoja na Mungu Baba.
 
Sasa kama alikufa kwa nini unasema ni wa milele
Maana yangu ni hii, Yesu(Mungu) alikuja duniani ili atuokoe. Ilibidi damu imwagike ndio tupate ondoleo la dhambi. Hivyo Yesu aliuvaa mwili wa binadamu kwa kuzaliwa na bikira Maria. Mwili huo ndio uliokufa. Sio Mungu. Na ndio sababu alifufuka.
 
Maana yangu ni hii, Yesu(Mungu) alikuja duniani ili atuokoe. Ilibidi damu imwagike ndio tupate ondoleo la dhambi. Hivyo Yesu aliuvaa mwili wa binadamu kwa kuzaliwa na bikira Maria. Mwili huo ndio uliokufa. Sio Mungu. Na ndio sababu alifufuka.
Kwa hiyo hakufa
 
Yohane 20:17

Yesu akamwambia, “Usinishike; sijaenda bado juu kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu uwaambie: Naenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.”
Yesu ni Mungu mwana sio baba. Yesu anaitwa Mungu maana ndie mwana pekee wa Mungu na ndie Mungu alimtumia kuumba vitu vyote. Ni kama vile Mungu anavyowatumia wazazi kupata mtoto
 
Naamanisha hivi species ya mwanadamu,utaita mbuzi au kondoo?...ukweli ni kwamba atakuwa mwanadamu tu...Yesu kristo ni species inayotokana na Mungu..sasa utamuitaje mwanadamu?
Wakati alipokuwa duniani alikuwa mwanadamu halisi. Ndio sababu aliona njaa, alisikia kiu, alilia nk. Lakini wakati huohuo alikuwa Mungu. Ndio sababu aliweza kutembea juu ya maji, kubadili maji kuwa divai..matendo ambayo mwanadamu wa kawaida hawezi kuyafanya.

Umetumia neno: "species"
Hatuwezi kusema "Yesu ni species inayotokana na Mungu," kwa sababu neno "species" linahusu jamii ya viumbe wa aina moja katika muktadha wa kisayansi au kibaiolojia.

A species is a biological classification of organisms that share common traits and can reproduce. Since God is not a created being and Jesus is fully divine, describing Him as a species from God is incorrect. Biblical teaching affirms that Jesus is of the same divine nature as the Father, not a separate category of being.
 
Ukumbuke biblia imetafsiriwa huenda kilichoaanishwa kwenye lugha chanzi sio kilichopo kwenye lugha lengwa 100%.

Jaribu kusoma maandiko hayo

1. Marko 8:27-38​

2. Mt 6:9-10
3. Mk 10:18
4. Yn 14:2-3
5. Mt 24:36-51
 
Yesu ni mwana wa pekee wa Mungu hivyo huitwa Mungu kwa sababu roho yake imeungana na Roho mtakatifu wa Mungu hivyo hakuna jambo lolote Roho wa Mungu baba atapanga kufanya pasipo Roho wa Mungu mwana kujua.
 
Ukumbuke biblia imetafsiriwa huenda kilichoaanishwa kwenye lugha chanzi sio kilichopo kwenye lugha lengwa 100%.

Jaribu kusoma maandiko hayo

1. Marko 8:27-38​

2. Mt 6:9-10
3. Mk 10:18
4. Yn 14:2-3
5. Mt 24:36-51
Tafsiri hazijabadili maana. Kwa mfano hilo andiko la Marko 10:18 Yesu hakuwa anakataa kwamba Yeye ni mwema au Mungu, bali alikuwa anamuuliza mtu huyo kama kweli anatambua maana ya kile alichosema. Kama Mungu pekee ndiye mwema, na mtu huyo anamwita Yesu "mwema," basi swali ni je, alitambua kwamba Yesu ni Mungu?

Kwa Kigiriki, lugha ya awali, andiko hilo linatumia neno ἀγαθός (agathos), linalomaanisha "mwema" kwa kiwango cha Uungu. Tafsiri za Kiswahili zinaleta maana hiyohiyo sawa na zilivyo tafsiri za Kiingereza kama vile King James Version (KJV): Why callest thou me good? There is none good but one, that is, God.

Tafsiri hizi zote zinafanana na ya Kiswahili. Kwa hiyo, hoja kwamba Kiswahili huenda kimetoa maana tofauti si sahihi, kwa sababu tafsiri zote zinabeba ujumbe huohuo.
 
Uhusiano wa Neno na Mungu: Yohana 1:1 inaonyesha kuwa Neno alikuwa "kwa Mungu," na si kwamba Neno alikua Mungu mwenyewe. Hii inaweza kueleweka kama kuwepo kwa tofauti kati ya Mungu na Neno, huku Neno likiwa na uhusiano wa karibu na Mungu lakini si Mungu mwenyewe.
Soma vizuri naye Neno ni MUNGU hapakufanyika kitu chochote isipokuwa yeye hebu soma ISAYA9:6 anaitwa MUNGU mwenye nguvu
 
Back
Top Bottom