Yohane 4:7-29
Basi, mwanamke mmoja Msamaria akafika kuteka maji. Yesu akamwambia, “Nipatie maji ninywe.” (Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.) Lakini huyo mwanamke akamwambia, “Wewe ni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezaje kuniomba maji?” (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano na Wasamaria katika matumizi ya vitu). Yesu akamjibu, “Kama tu ungalijua zawadi ya Mungu na ni nani anayekuambia: ‘Nipatie maji ninywe,’ ungalikwisha mwomba, naye angekupa maji yenye uhai.” Huyo mama akasema, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yenye uhai?
LUKA 7:36-50
- MWANAMKE MTENDA DHAMBI AMIMINA MAFUTA KWENYE MIGUU YA YESU
- AFUNDISHA KUHUSU MSAMAHA AKITUMIA MFANO WA MTU MWENYE DENI
Watu wanaitikia kwa njia tofauti mambo ambayo Yesu anasema na kufanya, ikitegemea hali ya moyo wao. Hilo linaonekana wazi katika nyumba fulani huko Galilaya. Farisayo anayeitwa Simoni anamkaribisha Yesu kwenye mlo, labda ili amwone kwa ukaribu mtu anayefanya kazi hizo za ajabu. Huenda Yesu anakubali kwa sababu anaona hiyo ni nafasi ya kuwahubiria wale waliopo, kama alivyokubali pindi nyingine alipoalikwa kula pamoja na wakusanya kodi na watenda dhambi.