Kwanza mwanafunzi asichapwe, pili akipata mimba arudi shuleni, tatu kama ana utovu wa nidhamu pia arudi shuleni. Waoneeni huruma walimu

Wewe unaishi wapi? Mbona wanaume wanaoana toka zamani na wala hawangoji ruhusa yako au ya serikali au mtu wa Mungu.
Mawazo kuwa utajiri unatoka kwa Mungu na sio juhudi zako ndio unawafanya mshinde kwa watu wa Mungu matapeli ambao wanajifanya watakuombea upate utajiri kama utampa kila kitu ulichokua nacho. Haujiulizi kwa nini wakina Kakobe na Gwajima ni matajiri wakati waumini wao wanabembeleza mpaka nauli ya daladala.
Wajinga ndio waliwao.

Amandla...
 
Mkuu naoma unajiita Holy! Hatupo hapa kukariri mistari ya biblia! Makuaambia mimi sipo kujipima na wewe unajua kiasi gani neno la Mungu! Ila lazima uelewe Neno na Mungu ni Neno! Kwa hiyo mambo ya kunizidi mara elfu hayana tija kwangu lakini nakwambia neno la Mungu lina nguvu nalo lazigawanya nafsi na roho na hakuna kilichojificha mbele yake! Ukweli utakuweka huru usipende kudandia mambo kisa kafanya mzungu!
 
Huyo huyo mzungu aliyekuletea huyo Mungu unayemuabudu! Kama hutaki kudandia achana na Mungu wa wayahudi na urudi kwenye matambiko yetu ya asili.
Pathetic creature.

Amandla...
 
Utajiri wa halali ndo unatoka kwa Mungu! Hao akina Kakobe na Gwajima sijawazungumzia! Wewe kama unawaona wanawarakini utajua mwenyewe! Ila ukumbuke sio kila kitu kikifanyika ulaya ndo ticket ya kufanyika bongo! Wajinga tu ndo watakuunga mkono!
 
Holy ni isiyo badirika badirika mkuu, haipo based na matatendo. Sio uzungu zipo njia za malezi ya mtoto iliyo bora sana ipo ki biblia .. tazama blue print za kina Yusufu, Isaka etc huoni mijeredi
 
Nitajie nchi moja Ulaya au Marekani au Australia au Canada ambako mwanafunzi anachapwa, anapimwa mimba na akipata mimba anafukuzwa shule. Nitajie hata nusu nchi. Hata robo nchi.

Amandla....
Tulee watoto kwa utamaduni wetu wa Afrika,mambo ya ulaya tuwaachie wenyewe huko, viboko viwepo kama kawaida
 
Huyo huyo mzungu aliyekuletea huyo Mungu unayemuabudu! Kama hutaki kudandia achana na Mungu wa wayahudi na urudi kwenye matambiko yetu ya asili.
Pathetic creature.

Amandla...
Nani amekwambia Mungu aliletwa na wazungu! Nitajie nabii nani alikuwa mzungu? Hapo Ethiopia tu ukiristo upo hata hao wazungu hawajaja huku tanganyika! Naomba uwe mtulivu hata unaposema mambo ya mizimu zote ni imani ila hapa tunazungumzia Imani ya Kikristo!
 
Utajiri wa halali ndo unatoka kwa Mungu! Hao akina Kakobe na Gwajima sijawazungumzia! Wewe kama unawaona wanawarakini utajua mwenyewe! Ila ukumbuke sio kila kitu kikifanyika ulaya ndo ticket ya kufanyika bongo! Wajinga tu ndo watakuunga mkono!
Anza kwa kuwakana wakina Livingstone waliokuletea hii dini unayojifanya unaijua kuliko vizazi vyao. Au unadhani hizo dini mnazokumbatia zilitoka kwa Mfaranyaki?
Mnasikitisha sana. Ulimbukeni unawasumbua.

Amandla...
 
Holy ni isiyo badirika badirika mkuu, haipo based na matatendo. Sio uzungu zipo njia za malezi ya mtoto iliyo bora sana ipo ki biblia .. tazama blue print za kina Yusufu, Isaka etc huoni mijeredi
Biblia isingeweza kuandika kila kitu eti mpk itaenda walikua wanachapwa viboko vingapi,
Ila imesema usimnyime mtoto fimbo.
 
Holy ni isiyo badirika badirika mkuu, haipo based na matatendo. Sio uzungu zipo njia za malezi ya mtoto iliyo bora sana ipo ki biblia .. tazama blue print za kina Yusufu, Isaka etc huoni mijeredi
Kwa hiyo Unahisi walikuwa hawana njia za kuonya watoto wao? Mbona biblia imeandika? Si kila kitu kiliandikwa na sio kila kisichoandikwa hakikutendwa!
 
Biblia isingeweza kuandika kila kitu eti mpk itaenda walikua wanachapwa viboko vingapi,
Ila imesema usimnyime mtoto fimbo.
Umejuaje kuwa hiyo fimbo ni fimbo unayo fikiria wewe na wakati picha ya mafumbo imetumika sana kwenye biblia kwa mfano Mungu aliposema atafumua marinda unajua alikuwa na maana gani ?
 
Tulee watoto kwa utamaduni wetu wa Afrika,mambo ya ulaya tuwaachie wenyewe huko, viboko viwepo kama kawaida
Na msiishie hapo. Wakiugua wafungeni vijikamba mikononi mwao na muwapeleke kwa mganga ili awachanje kwa sababu wanaumwa dege dege.

Amandla...
 
Anza kwa kuwakana wakina Livingstone waliokuletea hii dini unayojifanya unaijua kuliko vizazi vyao. Au unadhani hizo dini mnazokumbatia zilitoka kwa Mfaranyaki?
Mnasikitisha sana. Ulimbukeni unawasumbua.

Amandla...
Tuache tuendelee na dini zetu wewe endelea kuabudu hao wazungu!
 
Tuache tuendelee na dini zetu wewe endelea kuabudu hao wazungu!
Hiyo dini unayoiabudu ni ya kizungu au ya kiarabu. Tamaduni zetu watoto walikuwa wanafunzwa mambo yote haya kwenye jando na unyago.

Amandla...
 
Na msiishie hapo. Wakiugua wafungeni vijikamba mikononi mwao na muwapeleke kwa mganga ili awachanje kwa sababu wanaumwa dege dege.

Amandla...
Kama wa kwako hutaki achapwe, mhamishe mpeleke ulaya akakae huko wanapolea watoto kama mayai.
 
Kwa hiyo Unahisi walikuwa hawana njia za kuonya watoto wao? Mbona biblia imeandika? Si kila kitu kiliandikwa na sio kila kisichoandikwa hakikutendwa!
Mkuu malezi ya mtoto na makuzi ya mtoto yana amuliwa na maisha harisi ya mzazi, mtoto huchukua kutoka kwa mzazi. Kama wewe mzazi unatumia lugha chafu na mambo ya hovyo hovyo, tegemea mtoto atakuwa hivyo, na akiwa hivyo kwanini umbutue na mafimbo kabla wewe mzazi hujabadirika ? watoto hujifunza kutoka kwenye mazingira na jamii .. muepushe na mazingira na jamii ambayo ni negative
 
Hiyo dini unayoiabudu ni ya kizungu au ya kiarabu. Tamaduni zetu watoto walikuwa wanafunzwa mambo yote haya kwenye jando na unyago.

Amandla...
Na kwambia achana na mimi abudu hiyo mizimu yako na mimi niache nimwabudu Mungu kupitia Yesu kiristo!
 
Hii ni project kubwa sana ya kuporomosha maadili na kutengeneza vijana wazembe kwakiwango cha sgr, matokeo yake titayaona baada ya miaka 10 ijayo. Watasoma wajawazito tupu ambao baadae watakua tegemezi wote,tutakosa nguvu kazi ya vjana baadae, kumbukeni vjana ndo taifa lijalo
 
Umejuaje kuwa hiyo fimbo ni fimbo unayo fikiria wewe na wakati picha ya mafumbo imetumika sana kwenye biblia kwa mfano Mungu aliposema atafumua marinda unajua alikuwa na maana gani ?
Kwani kwa tafsiri ya marinda ni nini?au kwa upumbavu wenu mnageuza maana.yaani leo hii eti marinda ni kimekua kitu cha kushangaza, wewe unadhani marinda ni nini sasa?

Kama unampenda sana mwanao kuliko wazazi wengine, muhamishe kabisa mpeleke huko ulaya akakae huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…