Deo Benjamin
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 308
- 92
- Thread starter
- #41
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unajuaje jike na dume
Hao katika picha sio kwale .kwale wana fahamika .hao ni jamii nyingine tu ya ndege
Mkuu VisaGold
Asante kwa kupitia thread hii, ningeshauri upanue wigo wa ufugaji wako kwa kuwa ufugaji mara nyingine ni misimu, so kwa upande mwingine usiache biashara ya kuku wa mayai. Kwa upande wa Kwale ningeshauri uanze na wa siku moja kwa kuwa gharama yake ni nafuu na utawatunza kwa week sita tu then wataanza kutaga mayai (kwa kuwa wewe siyo mgeni kwenye ufugaji wa vifaranga una utaalamu wa layers tayari) gharama za vifaranga wa week nne ni kubwa na huna haja kwa kuwa tayari unauzoefu wa ufugaji, mara nyingi wanaochukua vifaranga wa week nne au tano ni wale wasio na uzoefu wa ufugaji au wale wenye majukumu mengi na hawana muda wa kutunza vifaranga. Kuhusu risk ni kuwa Kwale ni ndege mwenye kinga kubwa, na mara nyingi husumbua kidogo week mbili za kwanza hasa kwenye kukadilia joto lakini baada ya hapo vifo huwa ni adimu sana.
Myhem usijekuta wewe ndo mbulula
Kaka Deo asante sana kwa ushiriano wako, vifaranga wetu wote 1000 wamefika salama salmini, jana niliwapatia glucose kama ulivyoshauri, leo wote wameamka safi kabisa na wamechangamka sana, tutawasiliana kama nitahitaji chochote.
Naomba mnambie uchanganyaj wa chakula kwa ndege hawa kuanzia wik ya5
Njia nyingine ya kuwatambua majike na madume ni kwa kuwaangalia nyuma makalioni! Madume wanakuwa wamevimba na ukiwabinya wanatoa povu(shahawa) ila majike wao hawavimbi wala hawana povu!Kujua jike na dume ni rahisi sana kwa kwale wenye madoa na michirizi lakini ni vigumu kidogo kwa kwale weupe.
Kwale jike huwa anakuwa na madoa au michilizi mwili mzima na kwale dume huwa hana madoa au michirizi shingoni, anakuwa na madoa sehemu nyingine lakini shingoni huwa hana madoa.