Kwaresma na Pasaka Special Thread

Tumebakiwa na siku masaa machache sana kesho jumatano tarehe 5 tutaanza kipindi cha kwaresma kwa mfungo tukianza kwa jumatano ya majivu
 
Ratiba ya kufunga kula inakuaje mkuu?
Ratiba inakuwa kama ifuatavyo

Tunafunga chakula yaan tunafunga kula siyo kula kidogo

Unapoamua kufunga wewe funga siyo ule kidogo hapana

Na mwisho wa kula ni mda wa usiku siyo unaamka tena usiku saa 11 unaanza kula daku hapana, huko kutakuwa ni kubadilisha ratiba ya kula tu wala siyo kufunga

Na kufungua tunafungua saa 12 lakin jitaid kabla hujafungua kwa chakula unapiga hata Sala kidogo

Usipende kufungua chakula kabla hujasali

Asante mtumish
 
Mnajishindisha njaa tuu hamna kufunga wala nini!! Nyie Kuleni kitimoto na pombe ndo Vitu vyenu nyie na kufunga Wapi na wapi bhnaaa
 
Kwaresma, Majivu, Ijumaa kuu vyote ni church politics, haviko kwenye Biblia kuwahusu wakristo wa leo.
Yesu alishateswa, kusurubiwa, kufa, kufufuka na kupaa zake mbinguni zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kilichobakia kwa sasa Injili ipigwe kwa kwenda mbele na Yesu ainuliwe milele.
 
Sisi tunafunga ndugu yangu karbu tuungane kwa mfungo
Tunafunga ili iweje? yesu amesha tukomboa Hatuna dhambi,... alafu tayari yesu amesha jua nani ataenda motoni na nani ataenda kwa roho mtakatifu kama umesha wekwa kwenye kundi la motoni hata ufunge kizazi hautoboi
 
Kwahiyo ijumaa kuu yaan mateso ya YESU ni kinyume na injili yaan siyo injili?

Kwahiyo na kufunga nako si injili mtumish?

Unaielewaje injili wewe binafis
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…