Kwaresma na Pasaka Special Thread

Kwaresma na Pasaka Special Thread

Mkuu mm nina nia ya kufunga ila sielewi kanuni zetu za kufunga tunaanza saa ngapi hadi saa ngapi?
 
Kusudi la mfungo linabakia kwenye ibada zako ikiwa ni pamoja na Sala zako, kitu gan unamwomba MUNGU MWENYEZI akutendee

Lakini ni lazima ujinyime sana na kuacha kuishi kama ulivyo kuwa unaishi miezi mingine
Kwangu inakuwa tofaut kidogo, niwatakie kwaresma njema!

Ramadhani Mubarak kwa waislamu wote
 
Mkuu mm nina nia ya kufunga ila sielewi kanuni zetu za kufunga tunaanza saa ngapi hadi saa ngapi?
Kufunga kwaresma tunaanza kesho ndugu yangu

Kanuni ni kama ifuatavyo

Tunafunga kuanzia asubuh mpaka jion saa kumi na mbili

Lakin kabla hujafungua unasali kwanza

Jitaid kunuia jambo mbele ya MUNGU MWENYEZI iwe changamoto au shukrani

Usifunge bila kusali itakuwa ni sawa sawa na kushinda NJAA tu

Lakin pia siyo unafunga tena usiku unaamka kula hapana hiyo siyo funga

Kama una swali lingine uliza mtumish
 
Kesho mapema ibada ya majivu.

Tuombeane kwa Mungu azipokee toba zetu madhaifu na tabia mbovu tulizozoea kuziishi huko nyuma Kwaresma hii ikaziondoshe kwetu tubaki wasafi hata milele.
Asante sana ubalikiwe mtumish

MUNGU APOKEE Sala zetu

Tuache dhambi maana muda mwingi tunatembea najisi

BWANA YESU KRISTO atuoshe kwa damu yake takatifu
 
Leo nimewahi mapema misa ya kwanza ili niendelee na majukumu..
I hope na wengine mmeshiriki au la jioni msikose misa hii muhimu ya kutukumbusha sisi tu mavumbi na mavumbini tutarudi...
 
Jumatano njema ya majivu
 

Attachments

  • Screenshot_20250301_171653_Instagram.jpg
    Screenshot_20250301_171653_Instagram.jpg
    278.1 KB · Views: 1
Back
Top Bottom