Kweli biashara ya ndege ngumu, Kenya Airways na ukubwa wote wamechemka. Ruto kuiuza kwa Wamarekani. ATCL vipi?

Kweli biashara ya ndege ngumu, Kenya Airways na ukubwa wote wamechemka. Ruto kuiuza kwa Wamarekani. ATCL vipi?

MWENDAZAKE alifikiri biashara ya ndege ni kama Bodaboda jioni unaletewa hesabu...huku kwenye ndege kunahitaji uwekezaji wa muda mrefu

Wewe mjinga makufuli aliiweza biashara ya ndege ilikuwa hakuna janja janja wala delay wala kiongozi kutumia ndege kama yake. Itakuwaje hakuna hasara? Maana anaenda Dodoma anarudi Dar kaenda tena Dodoma mara karudi Dar tena yupo peke yake unajua trip moja ya kwenda Dodoma inakula kiasi gani?

Bado makamu wa Rais nae yuko kule na huku wamegawana ndege unajua hasara yake? Hasara yoote bado wanaileta kwa JPM kumsingizia hasara kaleta yeye shubamit.
 
Ni mtu mpumbavu kabisa tu ndio atashindwa kuendesha biashara ya ndege Qatar au Falme za Emirates ambazo zimejaa pesa za gesi, mafuta na ziko eneo la kimkakati katika usafiri wa anga duniani.

Kuna tofauti kubwa kati ya kutegemea kutega maji yanayoshuka mlimani kwa gravity na maji yanayohitaji pampu kufikia watu.
tupe hasara ya ndege za emirates na utupe hasara za ndege ya Qatar air, kama kuendesha ndege ni hasara kampuni mbili hizi zingeuza ndege zake
 
Rais wa Kenya, William Ruto amekutana na viongozi wakuu wa shirika la ndege la kimarekani la Delta katika mpango wa kuwauzia hisa zote 48.9% zinazomilikiwa na Serikali ya Kenya kwenye shirika hilo.

Kenya Airways imekuwa ikitegemea hazina ya Kenya kuweza kujiendesha huku kipindi cha Januari-Juni ikiwa imerekodi hasara ya dola milioni 82 na kipindi kama hicho 2021 kikitoa hasara dola milioni 95.8.

Kwa upande wa Tanzania, ripoti ya mwisho inayopatikana inasema ATCL imepata hasara ya TZS bilioni 36 mwaka 2020/21 kutoka bilioni 60 mwaka 2019/20. Kwasasa shirika hilo ndege zake kubwa inazoziendesha zimepumzishwa huku moja ikishikiliwa kwa madeni.

Serikali chini ya Rais Magufuli iliamua kulifufua shirika la ndege la Tanzania lililokuwa hoi bin taaban kwa kununua ndege mpya na kuliazima shirika hilo.
Biashara ya ndege haikwepeki japokuwa huwa tunapenda kuipaka matope kwa hizi siasa zetu nyepesi za humu jukwaani.

Huwezi kuwa na nchi yenye vivutio vinavyoongoza kwa kupewa tuzo za kimataifa halafu nchi yako ikakosa kuwa na shirika la ndege. Mungu aliyetupa vivutio hivi alikuwa na maana yake kwetu sisi.
 
Rais wa Kenya, William Ruto amekutana na viongozi wakuu wa shirika la ndege la kimarekani la Delta katika mpango wa kuwauzia hisa zote 48.9% zinazomilikiwa na Serikali ya Kenya kwenye shirika hilo.

Kenya Airways imekuwa ikitegemea hazina ya Kenya kuweza kujiendesha huku kipindi cha Januari-Juni ikiwa imerekodi hasara ya dola milioni 82 na kipindi kama hicho 2021 kikitoa hasara dola milioni 95.8.

Kwa upande wa Tanzania, ripoti ya mwisho inayopatikana inasema ATCL imepata hasara ya TZS bilioni 36 mwaka 2020/21 kutoka bilioni 60 mwaka 2019/20. Kwasasa shirika hilo ndege zake kubwa inazoziendesha zimepumzishwa huku moja ikishikiliwa kwa madeni.

Serikali chini ya Rais Magufuli iliamua kulifufua shirika la ndege la Tanzania lililokuwa hoi bin taaban kwa kununua ndege mpya na kuliazima shirika hilo.
Wazikodishe kwa precision, kwanini Precision air wameweza?
 
Binafsi sipingi kununua ndege kwani nayo ni kama nembo ya Nchi ila cha muhimu
Kuendesha Shirika la ndege kunahitaji watu wa marketing ambao ni creative, aggressive na profit oriented na wanaofanya maamuzi ya haraka na sio kuendelea kupeleka ndege kwenye miji/viwanja vya ndege ili kufurahisha watu na sio kupata faida
Tunahitaji watu ambao ni very creative na focused kwenye Biashara na sio hawa wa kucopy na kupaste
Muhimu zaidi; huwezi kuendesha Biashara ya ndege ya kimataifa bila kupata Wabia mathubuti (code share)
Yaani unapokea wageni wa ndege A unawapeka sehemu B. na ndicho kenya wamefanya (ila tofauti yake ni kuwauzia kabisa hisa?) Ukijifanya kusimama kivyako vyako, hutoboi...
ATC Ikiwashinda waipe private sector waone kama haitasimama ila wajue kwa Tanzania route zitabakia kama tatu tu ambazo zinafaida kubwa inayomezwa na route nyingine zisizokuwa na abiria/zinazoendeshwa kwa hasara kubwa. Route zitakazobakia ni
1. Kilimanjaro/Arusha to Dar, 2. Dar to Mwanza 3. Dar/Dodoma to Kigoma
Unataka kusema Mbeya hakuna abiria wa kutosha?
 
Ni Habari njema, huoni kuwa ni Maendeleo? Delta waki-invest Kenya Airways how big the airline will be? More revenue for Kenya, bigger worforce guaranteed by first World Economy growth! Stop your communist Thinking! The biggest investor in China is also US of America, what is your problem?

Fikra za mwenyekiti zimewaharibu bongo zenu, you need change, Serikali haiwezi kufanya biashara iwaachie wananchi!!!
Kuna sehemu nimesema ni jambo baya mkuu? Nimesema biashara ya kuendesha shirika la ndege ni ngumu na dunia nzima mashirika mengi ya ndege yamekuwa yanapambana na hasara zisizoisha. Air Tanzania ilijiunga na SAA lakini ngoma ikaishia pabaya.

Kudondoka fastjet ilikuwa makosa makubwa kwani tayari ilikuwa imeshasimama, bora Serikali wangewakopesha waimarike zaidi..
 
Kuna sehemu nimesema ni jambo baya mkuu? Nimesema biashara ya kuendesha shirika la ndege ni ngumu na dunia nzima mashirika mengi ya ndege yamekuwa yanapambana na hasara zisizoisha. Air Tanzania ilijiunga na SAA lakini ngoma ikaishia pabaya.

Kudondoka fastjet ilikuwa makosa makubwa kwani tayari ilikuwa imeshasimama, bora Serikali wangewakopesha waimarike Zaidi..
You are right!
 
Binafsi sipingi kununua ndege kwani nayo ni kama nembo ya Nchi ila cha muhimu
Kuendesha Shirika la ndege kunahitaji watu wa marketing ambao ni creative, aggressive na profit oriented na wanaofanya maamuzi ya haraka na sio kuendelea kupeleka ndege kwenye miji/viwanja vya ndege ili kufurahisha watu na sio kupata faida
Tunahitaji watu ambao ni very creative na focused kwenye Biashara na sio hawa wa kucopy na kupaste
Muhimu zaidi; huwezi kuendesha Biashara ya ndege ya kimataifa bila kupata Wabia mathubuti (code share)
Yaani unapokea wageni wa ndege A unawapeka sehemu B. na ndicho kenya wamefanya (ila tofauti yake ni kuwauzia kabisa hisa?) Ukijifanya kusimama kivyako vyako, hutoboi...
ATC Ikiwashinda waipe private sector waone kama haitasimama ila wajue kwa Tanzania route zitabakia kama tatu tu ambazo zinafaida kubwa inayomezwa na route nyingine zisizokuwa na abiria/zinazoendeshwa kwa hasara kubwa. Route zitakazobakia ni
1. Kilimanjaro/Arusha to Dar, 2. Dar to Mwanza 3. Dar/Dodoma to Kigoma
Service nzuri ni marketing tosha. Kwa kweli abiria wanapanda ATCL kwa kuwa hamna option. Kama fastjet angekuwepo hadi sasa ATCL wangekuwa wansafirisha viongozi wa serikali pekee.
 
Wewe mjinga makufuli aliiweza biashara ya ndege ilikuwa hakuna janja janja wala delay wala kiongozi kutumia ndege kama yake. Itakuwaje hakuna hasara? Maana anaenda Dodoma anarudi Dar kaenda tena Dodoma mara karudi Dar tena yupo peke yake unajua trip moja ya kwenda Dodoma inakula kiasi gani?

Bado makamu wa Rais nae yuko kule na huku wamegawana ndege unajua hasara yake? Hasara yoote bado wanaileta kwa JPM kumsingizia hasara kaleta yeye shubamit.
Mkuu kwa hiyo unataka kusema enzi za JPM ATCL ilikuwa haipati hasara, au sijakuelewa!
 
Ni Habari njema, huoni kuwa ni Maendeleo? Delta waki-invest Kenya Airways how big the airline will be? More revenue for Kenya, bigger worforce guaranteed by first World Economy growth! Stop your communist Thinking! The biggest investor in China is also US of America, what is your problem?

Fikra za mwenyekiti zimewaharibu bongo zenu, you need change, Serikali haiwezi kufanya biashara iwaachie wananchi!!!
Naunga mkono serikali haiwezi kufanya biashara. Wapewe wananchi serious kama Bakhressa alivyopewa NMC mbona maisha yanaenda na hakuna kelele, watu waambie ukweli ujamaa umeshindikana. Cabin crews watashona uniforms Indonesia kwa per diem za serikali kesho sijui nini? .kuna shirika private linaenda hivyo? CAG atahesabu hasara kila mwaka.
 
Tunaenda kwa Data; Ingia online
Tafuta seat za kutoka hayo maeneo niliyopendekeza kuanzia kesho tar 21 Dec hadi 26 Dec kama utapata seat ngapi zimebaki; Ila ukitafuta seat ya kutoka mbeya kuja dar, hata seat za leo unapata
Ninachomaanisha, Mbeya abiria wapo ila huwezi kulinganisha na huko nilikotaja LAKINI sipingani na wewe kwani ikionekana panalipa patakuwepo. Suala hapa nikufanya Kibiashara na sio kupeleka ndege ya abiria 78 ipate abiria 12 na hivyo kuishia kula faida yote iliyopatikana route zingine
Kwanza sipo Mbeya lakini naangalia Mbeya ni jiji
 
Binafsi sipingi kununua ndege kwani nayo ni kama nembo ya Nchi ila cha muhimu
Kuendesha Shirika la ndege kunahitaji watu wa marketing ambao ni creative, aggressive na profit oriented na wanaofanya maamuzi ya haraka na sio kuendelea kupeleka ndege kwenye miji/viwanja vya ndege ili kufurahisha watu na sio kupata faida.

Tunahitaji watu ambao ni very creative na focused kwenye Biashara na sio hawa wa kucopy na kupaste
Muhimu zaidi; huwezi kuendesha Biashara ya ndege ya kimataifa bila kupata Wabia mathubuti (code share)
Yaani unapokea wageni wa ndege A unawapeka sehemu B. na ndicho kenya wamefanya (ila tofauti yake ni kuwauzia kabisa hisa?) Ukijifanya kusimama kivyako vyako, hutoboi.

ATC Ikiwashinda waipe private sector waone kama haitasimama ila wajue kwa Tanzania route zitabakia kama tatu tu ambazo zinafaida kubwa inayomezwa na route nyingine zisizokuwa na abiria/zinazoendeshwa kwa hasara kubwa. kwa mtazamo wangu, route zenye faida kubwa ni;
1. Kilimanjaro/Arusha to Dar, 2. Dar to Mwanza 3. Dar/Dodoma to Kigoma na pengine moja ya kusini.
Uko sahihi kabisa kwa mtazamo wako, Air Tanzania inatakiwa ijiendeshe kibiashara!, Inatakiwa iwe na board na management inayoelewa mambo ya usafiri wa anga. Hii habari ya wanasiasa kuingiza mikono kwenye chungu cha kitaaluma ndio chanzo cha kufeli hasa kwenye biashara ya inayohusisha ndege.
Kukosekana kwa mameneja magwiji katika kuendesha makampuni ya usafisaji wa ndege ndiyo kiini cha kuyumba katika biashara hiyo. Kenya Airways nao wana matatizo kama ya kwetu kwenye nyanja hii. Tujikumbushe tulivyoiuzia South African Airways hisa za ATC, pia ilikuwa kutapatapa kama anavyotaka kufanya KQ kwa Delta Airways.
Pamoja na usiri unaoendelea inaonekana manunuzi ya Airbus 220-300 yana utata, sijui Boeing lakini aliyetuuzia hizo ndege yaani Bombardier aliishaiuza kampuni kwa Mitsubishi.... Sasa hapa kama Airbus wanatengeneza Series za A319 na A320 ambazo hazitofautiani sana na A220-300, hizi tulizonunua kwa nini zisiletewe zengwe la engines?
Kwa mtazamo wangu Kampuni yetu ya ndege inapaswa kusukwa upya kwa kuiweka huru na mikono ya wanasiasa, iorodheshwe kwenye soko letu la hisa, ili watanzania tununue hisa ili kampuni ijiendeshe yenyewe kibiashara. Yupo Kimei kule bungeni anapoteza muda adhimu wa maisha yake kugonga meza, huyu mtu alikoitoa CRDB hadi ilipo leo, ana mbinu na uwezo wa kuisimamisha Air Tanzania ikasimama.
 
Ilikuwa ni hitaji la mwendazake na sio watz
yani wabongo bwana na ndio mana mnajikuta mtaani mnafungua biashara ya aina moja kisa jirani kakwambia inalipa kakupigia na hesabu za uongo na kweli,suala la ndege kwa Taifa ni la msingi sana wakulaumiwa ni walioliua na kushindwa kulisimamia na sio kulaumu au kuamini kwa sababu ni ngumu lisifanyike
 
Biashara ya usafirishaji abiria kwa ndege ni ngumu.Hasara kwa dunia yote ya kampuni za ndege kwa miaka 2020, 2021, 2022 ni $137.7bn, $42bn, $6.9bn mtawalia. Kwa mwaka 2023 inatarajiwa faida $4.7bn. Naipongeza serikali ya Kenya ( sio Raisi Ruto kipekee) kama imeamua kuwauzia Waamerika Kenya Airways.
Kwa waliosisitiza umuhimu wa kuwa na menejimenti mahiri kui vusha Air Tanzania,na sio kutoa vyeo vya juu kisiasa au "kiuzalendo" watazame timu ya uongozi wa juu wa Qatar Airways- Mtendaji Mkuu ni Mhindi, Kuna wazungu Sr. VP, na VP. Emirates, president ni Sir Tim Clark -British, CFO(fedha) ni Mjeremani. Mashirika hayo yanaendeshwa kwa ufanisi mkubwa. Na Waarabu kama sisi ni wazalendo pia.
 
Back
Top Bottom