Kweli mapenzi ni uchafu. Wewe ungefanyaje?


Kawaida sana ,mpaka huyo mke unayemuoa ujue anajaza coaster na wengine wanasimama ,haina makombo.
 
Umeshajiuliza akija kufahamu ulikua unajua na ulikaa kimya unafikiri urafiki wenu hautavunjika?
Atajuaje kuwa nilikuwa najua alafu nimekaa kimya.....nani atamwambia....btw haya mambo hayana maana ndugu.... unaweza ukafanya wema ukaonekana mbaya
 
Atajuaje kuwa nilikuwa najua alafu nimekaa kimya.....nani atamwambia....btw haya mambo hayana maana ndugu.... unaweza ukafanya wema ukaonekana mbaya
Unachokifanya sasa hivi ni kitu cha kikatili sana. Yani wewe na huyo shemeji yako ni kitu kimoja mnawang'ong'a washikaji zako(mnawachora). Hivi hakuna kitu kinakusuta ukiwa na washikaji zako)
 
Mwenyewe nimeshangaa kwa alichokifanya. Kakaa kimya kabisa???

Huyu hafai kuitwa rafiki.
 
Unachokifanya sasa hivi ni kitu cha kikatili sana. Yani wewe na huyo shemeji yako ni kitu kimoja mnawang'ong'a washikaji zako(mnawachora). Hivi hakuna kitu kinakusuta ukiwa na washikaji zako)
Mimi siwezi kumuacha mwanangu namuona anapotea. Nitamsanua tu! Akini mind poa! Asipo ni mind poa tu vilevile.

Kikubwa nimeshamfikishia habari.

Kuna mwanangu mmoja nilimuelewa mwanamke mmoja anafanya naye kazi ofisi moja. Nikamuuliza vipi hapo? Kuna usalama? Nikamwambia wazi nimemuelewa. Jawabu lake mwanangu mimi sijui tunaonana tu ofisini ila ni dada anayejiheshimu. Nikajua mwanangu hawezi kuniangusha nikatia vocal.

Lakini nikajiongeza zaidi kuna mwanangu mwengine nilisoma naye anafanya kazi kwenye hiyo Taasisi nikamuelezea bhana fulani shemeji yako huko!

Kumbe kesho yake mshikaji akaenda ofisi ya mwanangu huyo ambaye huyo demu ni Co worker wake. Akamuuliza fulani si mshikaji wako? Jamaa anajibu ndiyo? Akamuuliza huyu demu si unamjua jinsi alivyo? Akajibu ndiyo? Akamuuliza kipi kinachokufanya usimwambie mshikaji ukweli? Akabaki anajiuma uma?

Yule mwanangu niliyesoma naye akanipigia simu. Akaniambia mwanangu ukiamua kunichukia nichukie, ila yule demu siyo piga chini haraka. Akaniambia nimemfuata yule Co worker wake ambaye unayefahamiana naye na nimemuuliza kabisa fulani si mshikaji wako? Kipi kimekufanya usimwambie?

Nikamwambia babu, kabla sijaingia mazima nilipitia kwa huyo huyo mshikaji yeye akaniambia hajui chochote mara huyo demu ametulia na hapa za pale! Nikampa big up nikamwambia mwanangu nimekuongezea vyeo! Sijakuchukia wala nini!

Nikamgeukia yule mwana mwengine nikamwambia mwanangu, hivi unaniachaje mimi nateketea? Akaanza kuleta sababu kama za huyu mleta Uzi.

Nikamwambia umenikosea pakubwa sana! Ukimwangalia ni mshikaji ambaye akikwama hata kwenye mambo yake ya kifamilia huwa mimi ndiyo kimbilio lake. Nikamwambia wazi kuwa umezingua sana!

Washikaji wa aina hii ni wanafiki! Yule demu nilipiga chini siku hiyo hiyo! Halafu nilikuwa namuandaa awe mke.
 
Kweli kabisa wana kama huyu mtoa mada ni watu wabaya sana. Yani anamuacha mshikaji wake anateketea kwasababu za kipumbavu Sana.
 
Demu anashida gan?
 
Mapenzi hayashauriki
 
Mnamlaumu bure tu mtoa mada mkizama kwenye penzi mnakuwaga matahira kweli ya nini kujichosha
 
kwaiyo ukamwacha mshkaji wako aendelee kupigwa tu so ndio eeh???
ndiyo maana wazungu wana majina mengi ya mahusiano, sijui associate, acquitance, friend. Zama hizi treat peopla kama app ya facebook yaani "people you may know" 😆
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…