Kama mtu hajawahi kupitia kwenye hali ambayo anasimuliwa ni vigumu kuelewa au kukubali.
Mleta mada namuelewa sana, niliwahi pitia hali kama yake.
Siku moja nilikuwa kwenye ofisi moja ya Posta nilikuwa natuma barua, mkononi nilikuwa na hela ya kutuma hela halafu ndio sikuwa na hela ya kula/kutumia na sikuwa najua nitapaje hela kwa siku hiyo.
Wakati nafanya process pale kaunta kuweka makabrasha vizuri, kubandika stamp then ikanilazimu kurudi kukaa kwenye benchi ili nimalizie na kukabidhi. Kurudi tu nyuma kwenye benchi wakati naketi ghafla nikaona elfu kumi imedondoka chini sehemu ya wateja kuandaa hizo nyaraka, moyo ukashtuka nikaokota nikatulia nikaendelea na process.
Uzuri hapakuwa na mteja mwingine zaidi yangu ambaye ningehisi ndio kadondosha, nilipomaliza nikaondoka huku moyoni nikiwa tayari nishaipigia bajeti ya matumizi kwa siku ile.