Kweli Mungu anatenda, nimepata elfu kumi niliyoisahau kwenye begi siku nyingi

Kweli Mungu anatenda, nimepata elfu kumi niliyoisahau kwenye begi siku nyingi

hiyo mia nne ilibaki malaika walinunua lambalamba zile za miamia 6 wakala maana ilitakiwa ukutane na 11,000 ndo pesa walioagizwa wakuletee
 
Kuna ujinga mwingi sana, hata Mungu anawasikitikia kwa kukosa maarifa
Wewe bado mtoto mchanga sana kwenye ishu za kiimani, ndo maana huwezi muelewa mtoa mada.
Nyie ndo wale unachokiona ndo umekiona hamnaga macho Wala masikio zaidi ya haya yaliyokaa ka dishi la zuku.!
 
Nimesoma huku mapigo ya moyo yanaenda kasi,, nikajua umekuta minoti imejaa kwenye begi lote aiseee 😁
Mkuu siyo kila mtu anahitaji minoti inayojaa kwenye begi, wengine wanahitaji za kuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku, wewe kama unaminoti iliyojaa mabegi jifunze kubariki wengine hapo mtaani kwako, najua ni wengi tu wanaokutana na adha kama aliyoongea mtoa mada, lakini kuna watu wengi tu wanamapesa hata hawajui wayafanyie nini, mbaya zaidi hawajali kabisa kuwa kuna kundi kubwa kati yao linahali ngumu sana.
 
Kama mtu hajawahi kupitia kwenye hali ambayo anasimuliwa ni vigumu kuelewa au kukubali.

Mleta mada namuelewa sana, niliwahi pitia hali kama yake.

Siku moja nilikuwa kwenye ofisi moja ya Posta nilikuwa natuma barua, mkononi nilikuwa na hela ya kutuma hela halafu ndio sikuwa na hela ya kula/kutumia na sikuwa najua nitapaje hela kwa siku hiyo.

Wakati nafanya process pale kaunta kuweka makabrasha vizuri, kubandika stamp then ikanilazimu kurudi kukaa kwenye benchi ili nimalizie na kukabidhi. Kurudi tu nyuma kwenye benchi wakati naketi ghafla nikaona elfu kumi imedondoka chini sehemu ya wateja kuandaa hizo nyaraka, moyo ukashtuka nikaokota nikatulia nikaendelea na process.

Uzuri hapakuwa na mteja mwingine zaidi yangu ambaye ningehisi ndio kadondosha, nilipomaliza nikaondoka huku moyoni nikiwa tayari nishaipigia bajeti ya matumizi kwa siku ile.

Sijawahi kupitia ugumu wa maisha kipesa kama unaozungumzia lakini huwa naamini wapo wasio na kitu kabisa na namna ya kupata kuwa ngumu

Hongera na pole kwa kupitia wakati wa namna hiyo
 
Nilikuwa katika shida kubwa ya kiuchumi kazi hakuna sikuwa na chochote siku moja nimeamka sijui hata familia itakula Nini ndanii nilikuwa na mkaa tu wa buku, basi Ili kupoteza mawazo nikaona nikusanye nguo chafu pamoja na begi la mgongoni nikafue basi nikatoa vilivyokuwemo kwenye lile begi na sio mara ya kwanza kulifua huwa ninalipekuwa na kulikagua mara nyingi tu lkn sijawahi kuona kitu ambacho sikutarajia.

Basi nilivomaliza nikiwa nimeshika lile begi nikamuomba Mungu kama utani vile nikamwambia Mungu hebu tenda muujiza nikikagua hili begi nikute pesa basi nikapekua we maajabu nakuta Noti ya elfu 10 pamoja na silver za mia nne nilishangaa sana.
Mungu mwema toa zaka!
 
Haukuuliza hata kama kuna mtu medondosha, kwahiyo ukasema, Mungu amenidondoshea
Katika hali niliyokuwa nayo hata ingekuwa wewe ungeshukuru na kuchukua bila kuuliza.
 
Sijawahi kupitia ugumu wa maisha kipesa kama unaozungumzia lakini huwa naamini wapo wasio na kitu kabisa na namna ya kupata kuwa ngumu

Hongera na pole kwa kupitia wakati wa namna hiyo
Basi wewe umekuwa wa tofauti, kwa asilimia kubwa ambao hawajawahi kupitia kwenye misukosuko huwa wanachukulia poa au kutokuelewa kama kuna hali za namna hiyo.
 
Hiyo pesa niliweka mm nilipokuja kumtembelea mkeo.
Next time nikija nitaacha laki moja,lakini mwambie mkeo anihudumie vizuri kwa hali zote.
 
Back
Top Bottom