Kweli Mungu anatenda, nimepata elfu kumi niliyoisahau kwenye begi siku nyingi

hiyo mia nne ilibaki malaika walinunua lambalamba zile za miamia 6 wakala maana ilitakiwa ukutane na 11,000 ndo pesa walioagizwa wakuletee
 
Kuna ujinga mwingi sana, hata Mungu anawasikitikia kwa kukosa maarifa
Wewe bado mtoto mchanga sana kwenye ishu za kiimani, ndo maana huwezi muelewa mtoa mada.
Nyie ndo wale unachokiona ndo umekiona hamnaga macho Wala masikio zaidi ya haya yaliyokaa ka dishi la zuku.!
 
Nimesoma huku mapigo ya moyo yanaenda kasi,, nikajua umekuta minoti imejaa kwenye begi lote aiseee 😁
Mkuu siyo kila mtu anahitaji minoti inayojaa kwenye begi, wengine wanahitaji za kuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku, wewe kama unaminoti iliyojaa mabegi jifunze kubariki wengine hapo mtaani kwako, najua ni wengi tu wanaokutana na adha kama aliyoongea mtoa mada, lakini kuna watu wengi tu wanamapesa hata hawajui wayafanyie nini, mbaya zaidi hawajali kabisa kuwa kuna kundi kubwa kati yao linahali ngumu sana.
 

Sijawahi kupitia ugumu wa maisha kipesa kama unaozungumzia lakini huwa naamini wapo wasio na kitu kabisa na namna ya kupata kuwa ngumu

Hongera na pole kwa kupitia wakati wa namna hiyo
 
Mungu mwema toa zaka!
 
Haukuuliza hata kama kuna mtu medondosha, kwahiyo ukasema, Mungu amenidondoshea
Katika hali niliyokuwa nayo hata ingekuwa wewe ungeshukuru na kuchukua bila kuuliza.
 
Sijawahi kupitia ugumu wa maisha kipesa kama unaozungumzia lakini huwa naamini wapo wasio na kitu kabisa na namna ya kupata kuwa ngumu

Hongera na pole kwa kupitia wakati wa namna hiyo
Basi wewe umekuwa wa tofauti, kwa asilimia kubwa ambao hawajawahi kupitia kwenye misukosuko huwa wanachukulia poa au kutokuelewa kama kuna hali za namna hiyo.
 
Hiyo pesa niliweka mm nilipokuja kumtembelea mkeo.
Next time nikija nitaacha laki moja,lakini mwambie mkeo anihudumie vizuri kwa hali zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…