Ikiwa kapanganga kila kitu, huoni kwamba anatuchezea 'bongo movie?
Kwa nini waandika hivi?
Mungu hupanga lakini ubatili/ukaidi wa mwanadamu na mbinu ovu za shetani huingilia kati...
Kwanini sasa wengine akawaingize mbinguni na wengine motoni?
Mkuu sina uhakika wewe ni mfuasi wa imani ipi lakini nina imani kuwa unafahamu vyema taratibu za hukumu ya haki...
Kwa matendo mtu uhukumiwa, aliye muasi hupewa adhabu sawasawa na uasi wake na mtu mwema hupewa thawabu...
Mwanadamu kapewa fursa ya kuchagua njia moja kati ya mbili, uovu au wema...
How could i act beyond God planning?
Huwezi na wala haiwezekani...
Ikiwa ameshanipangia kutomkubali kwani akaniadhibu by then?
Katika kitabu cha Biblia kuna hii aya;
Mithali 16:4 Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.
Hivyo utaadhibiwa kwa kuwa pamoja na ubaya ulioumbwa nao bado umepewa nafasi ya kukacha ubaya huo na kufanya wema...
Ivi unadhani vitabu vyake vinaweza kunifanya nimkubali wakati alishanipangia kutomkubali?
Mkuu kumkubali Mungu hakutokani na vitabu vyake bali kunaanza na utayari wa moyo...
Moyo usio tayari hauwezi kumkubali na kufuata mafundisho ya Mungu...
Ivi huoni Mungu apangae kila kitu hana uadilifu, upendo, busara na ni mbaguzi!!!!
Sasa mkuu, ataitwaje Mungu kama vitu vingine ataviacha tuvipange sisi?
Huoni kutakuwa na chaos hapo?
Kwanini sasa wengine awapangie wazaliwe walemavu na wengine wazima? Au walemavu hawajapangiwa na Mungu kuwa vile?
Sio walemavu wote huzaliwa hivyo kwa matakwa ya Mungu hata kama ni mpango wake...
Wengine huzaliwa hivyo kwa sababu ya adhabu tu za wazazi au vizazi...
Mungu huwa anapatiliza uovu wa wazazi kwa vizazi...
Inapotokea hivyo basi shetani hupewa mamlaka ya kuharibu...
Kwanini apange wengine wawe tajiri na wengine maskini? kama sio upendeleo ni nini hiko?
Mungu hajaumba madaraja ya watu kulingana na kiasi cha mali, wingi au uchache wa fedha...
Utajiri au umaskini ni matokeo ya mtu kuishi duniani na husababishwa na namna utumiavyo nguvu uliyopewa na Mungu...
Kumb 8:18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Si mapenzi ya Mungu tuwe maskini kwa kuwa yeye mwenyewe ndiye atupaye nguvu ili tupate utajiri! Kama basi Mungu anatupa nguvu za kupata utajiri, ina maana ni wazi kwamba Mungu hapendi tuwe maskini.
Kwanini amempangia shetani kutupotosha?
Hahah...mkuu nadhani unaafiki kuwa huwezi kuvuka darasa pasipo kufaulu mtihani, shetani yupo kutoa mitihani(majaribu) ili imani zetu zipimwe ni kwa kiasi gani tunampenda huyu Mungu aliyetuumba...
Zaidi tambua kuwa mwanadamu ni mkuu zaidi ya shetani, hivyo usiogope sana na ukamuona shetani ana mamlaka kukuzidi hata umuogope...