Kweli Mungu ni muweza wa yote?

Kweli Mungu ni muweza wa yote?

Kwa nini waandika hivi?
Bongo movie or movies ingeneral save XXX movie ndio hupangwa matukio yote katika movie husika. It has no reliable effects kwa wahusika/actors there to in a sense that huwezi kusemea vile walivyoact ndivyo walivyo. Hata kama aliua apart from that movie huwezi kumshtaki kwa murder.

Hii itakwenda sawa ikiwa na Mungu amepanga kila kitu. kwa lugha nyepesi mtu akipangiwa na Mungu anakuwa anaact under God's will by then Mungu hawezi kuja kuhukumu au kuuliza kwa kitu ambacho amekipanga mwenyewe.

Mungu hupanga lakini ubatili/ukaidi wa mwanadamu na mbinu ovu za shetani huingilia kati...

How come mpango wa Mungu unakuwa interfered na mind ya mwanadamu and/or shetani???

How could you limits god's power?

Mkuu sina uhakika wewe ni mfuasi wa imani ipi lakini nina imani kuwa unafahamu vyema taratibu za hukumu ya haki...

Im Muslim, though rationalist, never believe in blind! I know kila mtu atahukumiwa kutokana na matendo yake. TONAPOPISHANA NI PADOGO TU, Kwamba Mimi naamini Mungu hajapanga KILA kitu, na hivyo alivyovipanga neither mwanadamu nor shetani anaweza pangua. Ila najua anajua kila kitu, ie jana, leo na kesho. Hope unawaeza kutofautisha kati ya KUPANGA na KUJUA.

Hiyo theory kwamba Mungu kapanga kila kitu iko hata katika bongo za waislamu tena wengi tu!!!!

Kwa matendo mtu uhukumiwa, aliye muasi hupewa adhabu sawasawa na uasi wake na mtu mwema hupewa thawabu...

Mwanadamu kapewa fursa ya kuchagua njia moja kati ya mbili, uovu au wema...

Si umeona hapo?
Kivipi mtu achague wakati alishapangiwa? eg: Mungu ameshanipangia ubishi na kutomkubali, then ntawezaje kutokua mbishi na kumkubali? Mimi nnauwezo gani wa kiasi cha kupangua mpango wake? Kama anapanga kila kitu kwanini asipange watu wote tumkubali na kutmukuza?

Huwezi na wala haiwezekani...

Katika kitabu cha Biblia kuna hii aya;
Mithali 16:4 Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.
Kufanya kitu kwa kusudi lake hiyo iko sahihi. hapo "hata wabaya kwa siku ya ubaya" sijaelewa. Can you tell me amepangia baadhi ya watu ubaya ili akawaadhibu? Or anamakusudi gani kupangia wengine ubaya then akaleta vitabu ili watu waokoke? Dont you God atakuwa anajikontradict hapo?

Au ndio ...UPU.MBAVU WA MUNGU UNAHEKIMA ZAIDI YA WANADAMU...? Wakorinto 1. 1:25.

Cc: Mkuu wa chuo kwa ufafanuzi zaidi.

Hivyo utaadhibiwa kwa kuwa pamoja na ubaya ulioumbwa nao bado umepewa nafasi ya kukacha ubaya huo na kufanya wema...

Ivi unadhani ni sawa kupangiwa ubaya na kuumbwa na ubaya? Then, kwanini Mungu ametuumba na ubaya?

Mkuu kumkubali Mungu hakutokani na vitabu vyake bali kunaanza na utayari wa moyo...

Moyo usio tayari hauwezi kumkubali na kufuata mafundisho ya Mungu...

Huo utayari unatokana na mipango ya Mungu au free will ya mwanadamu inayoambatana na reason/s?

Sasa mkuu, ataitwaje Mungu kama vitu vingine ataviacha tuvipange sisi?

Huoni kutakuwa na chaos hapo?

Lazima nifanyekitu kwa matakwa yangu ndio unihukumu, huwezi kunipangia kunyume mwenyewe then uniadhibu.

Ataitwa Mungu kama mfalme wa mbingu, alieumba dunia kwa mfano wake na kuratibu mifumo mizima ya upumuaji, huku akitupa akili huru za kupambanua mambo then akaleta vitabu tujue ukweli na kuchagua wapi tufate ili mtu asijeakasema mimi sikupata ujumbe.

Kwa mantiki hiyo Mungu hapangi kila kitu na bado ataendelea kuwa Mungu.

Sio walemavu wote huzaliwa hivyo kwa matakwa ya Mungu hata kama ni mpango wake...

Wengine huzaliwa hivyo kwa sababu ya adhabu tu za wazazi au vizazi...

Mungu huwa anapatiliza uovu wa wazazi kwa vizazi...

Ivi kumbe na Mungu ni .... wa VISASI?
Ivi na Mungu anaadhibu mtu kwa kosa la mtu mwengine???
Kwanini awaumbe walemavu watoto kwa makosa ya wazazi wao?

Inapotokea hivyo basi shetani hupewa mamlaka ya kuharibu...

Mungu hajaumba madaraja ya watu kulingana na kiasi cha mali, wingi au uchache wa fedha...

Utajiri au umaskini ni matokeo ya mtu kuishi duniani na husababishwa na namna utumiavyo nguvu uliyopewa na Mungu...

Kumb 8:18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

Si mapenzi ya Mungu tuwe maskini kwa kuwa yeye mwenyewe ndiye atupaye nguvu ili tupate utajiri! Kama basi Mungu anatupa nguvu za kupata utajiri, ina maana ni wazi kwamba Mungu hapendi tuwe maskini.

Hahah...mkuu nadhani unaafiki kuwa huwezi kuvuka darasa pasipo kufaulu mtihani, shetani yupo kutoa mitihani(majaribu) ili imani zetu zipimwe ni kwa kiasi gani tunampenda huyu Mungu aliyetuumba...

Zaidi tambua kuwa mwanadamu ni mkuu zaidi ya shetani, hivyo usiogope sana na ukamuona shetani ana mamlaka kukuzidi hata umuogope...

Mmh! ok Watu8 Im on my reseach kuhusiana na hizi hadithi za Dini na Mungu. Zinachanganya sana hizi, then kila kundi linajiona liko sahihi na makundi ya dini ni zaidi ya mia tano Duniani.

Nashindwa kukubali hao wote ni wakweli licha ya kwamba hoja zao zinaconvise sana.

PAMOJA.
 
Last edited by a moderator:
Nawe hukomi na maswali ya kutoto huku ukijiita mwanasayansi ?
Wewe unaamini uwepo wa Gravity , uwepo wa Umeme nk nk nami natetea imani yako sasa kwa nini Mimi ninayeamini Mungu kwa kuwa najua Jema na Baya unione sina maana lakini unayeamini Gravity na Umeme ujione mjanja ?.
Ulimbukeni huo unatokana na nini ?

Maswali yangekuwa ya kitoto ingekuwa rahisi kuyajibu.

Maswali hujayajibu, unauaitaje ya kitoto?
 
Maswali yangekuwa ya kitoto ingekuwa rahisi kuyajibu.

Maswali hujayajibu, unauaitaje ya kitoto?

Nithibitishie uwepo wa Gravity na Umeme
Niletee kanuni unayitumia kutambua wema na ubaya ?
Unataka ujibiwe sawa na ulivyomuumba mungu kichwani mwako ?
 
Sio walemavu wote huzaliwa hivyo kwa matakwa ya Mungu hata kama ni mpango wake...

Wengine huzaliwa hivyo kwa sababu ya adhabu tu za wazazi au vizazi...

Mungu huwa anapatiliza uovu wa wazazi kwa vizazi...

Hapa sijapapenda hata kidogo

Hapa sijapapenda hata kidogo
 
Hapa sijapapenda hata kidogo

Hawa watu wanatapatapa tu.

Look at this.

Sheria ya binadamu haina upendo wote, ujuzi wote wala uwezo wote.

Lakini karibu dunia nzima nchi zinazofuata misingi ya utawala wa sheria misingi ya sheria inakataza mtoto kuhukumiwa kwa kosa la mzazi. Au mzazi kuhukumiwa kwa kosa la mtoto.

Kwa sheria zenye upeo wa haki za kibinadamu tu, mtu hahukumiwi kwa makosa ya mwingine.

Nilitegemea mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote awe na haki iliyo na viwango vya juu zaidi ya sheria za kibinadamu.

Kama sheria za binadamu zinakataza kuhukumu mtoto kwa kosa la mzazi, nilitegemea sheria za mungu ziwe nzuri zaidi ya hizo.

Sasa naambiwa sheria za mungu zinahukumu mtoto kwa makosa ya mzazi. Hata vizazi na vizazi.

Huyu mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote imekuwaje akawa na sheria ambazo zimepitwa viwango na sheria za kibinadamu?

Yupo kweli au ni hadithi za zamani zimetungwa na watu tu enzi hizo za ujinga ambapo kumhukumu mtoto kwa kosa la baba ilikuwa sawa?
 
Mungu ni muweza wa yote ndiyo ila siyo kwenye Dunia hii. Kwenye Dunia hii muweza wa yote ni Shetani Ibilisi na kipindi chake alichopewa kuitawala hii Dunia ni kifupi.

Kama ni muweza wa yote lakini si kwenye dunia hii, basi si muweza yote huyo.

Maana hawezi yote kwenye dunia hii.
 
Hawa watu wanatapatapa tu.

Look at this.

Sheria ya binadamu haina upendo wote, ujuzi wote wala uwezo wote.

Lakini karibu dunia nzima nchi zinazofuata misingi ya utawala wa sheria misingi ya sheria inakataza mtoto kuhukumiwa kwa kosa la mzazi. Au mzazi kuhukumiwa kwa kosa la mtoto.

Kwa sheria zenye upeo wa haki za kibinadamu tu, mtu hahukumiwi kwa makosa ya mwingine.

Nilitegemea mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote awe na haki iliyo na viwango vya juu zaidi ya sheria za kibinadamu.

Kama sheria za binadamu zinakataza kuhukumu mtoto kwa kosa la mzazi, nilitegemea sheria za mungu ziwe nzuri zaidi ya hizo.

Sasa naambiwa sheria za mungu zinahukumu mtoto kwa makosa ya mzazi. Hata vizazi na vizazi.

Huyu mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote imekuwaje akawa na sheria ambazo zimepitwa viwango na sheria za kibinadamu?

Yupo kweli au ni hadithi za zamani zimetungwa na watu tu enzi hizo za ujinga ambapo kumhukumu mtoto kwa kosa la baba ilikuwa sawa?

Usichukulie kama advantage. aliesema hivyo ni binadamu na sio Mungu. mwanadamu kukosea ni kawaida, yule mdau ni mkiristo na anafuata biblia. biblia inapinga yale maneno. Kuna aya zaidi ya tatu zinazopinga mzigo wa mwengine kubebeshwa mwengingine.

ukitaka nakuekea hizo aya.
 
A rather exposing question.

Bertrand Russel, mwanahisabati na msoni wa mantiki wa kutoka Uingereza alishawahi kusema kwamba akifa na kukuta kuna mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote, na akihukumiwa kwa kutoamini mungu, atamhoji mungu huyo kwa nini hajumpa akili za kumjua.

Kwani Alikuwa Hana Akili ya Kusikiliza Mahubiri na Kusoma Biblia
 
Usichukulie kama advantage. aliesema hivyo ni binadamu na sio Mungu. mwanadamu kukosea ni kawaida, yule mdau ni mkiristo na anafuata biblia. biblia inapinga yale maneno. Kuna aya zaidi ya tatu zinazopinga mzigo wa mwengine kubebeshwa mwengingine.

ukitaka nakuekea hizo aya.

Kwa hiyo Biblia inajipinga?

Maana Biblia hiyo hiyo ina aya zinazosema mungu anawapatiliza hukumu vizazi na vizazi kwa makosa ya wazazi wao, na binadamu wote tumerithi dhambi ya asili ya Adam.

Kimsingi Biblia na Quran vyite vinajipinga.

Hapa unaambiwa mungu ndiye mtoa neema zote, pamoja na za kumjua. Huwezi kumjua mpaka akujaalie mwenyewe.

Kule unaambiwa usipomkubali mungu (ambaye huwezi kumkubali mpaka atake mwenyewe) unachomwa moto.

How absurd.
 
Kwani Alikuwa Hana Akili ya Kusikiliza Mahubiri na Kusoma Biblia

Akili yake imeangalia biblia na kujuta biblia ina makosa kibao.

Na akiki hiyo ndito mnasema kapewa na mungu.

Sasa hapa kama kuna aliyekosea ni yeye aliyeitumia akiki yake vizuri au mungu aliyempa akiki ambayo imeona makosa katika biblia?
 
Kwa hiyo Biblia inajipinga?

Maana Biblia hiyo hiyo ina aya zinazosema mungu anawapatiliza hukumu vizazi na vizazi kwa makosa ya wazazi wao, na binadamu wote tumerithi dhambi ya asili ya Adam.
Im not christian so i cant defend it.

Kimsingi Biblia na Quran vyite vinajipinga.

Hapa unaambiwa mungu ndiye mtoa neema zote, pamoja na za kumjua. Huwezi kumjua mpaka akujaalie mwenyewe.

Kule unaambiwa usipomkubali mungu (ambaye huwezi kumkubali mpaka atake mwenyewe) unachomwa moto.

How absurd.

Thibitisha.
 
Kwanza kabisa Quran umeisoma kwa undani gani, maana swali lako linanipa shaka kama umeisoma.

I know kuna such kind of verses, but not in a manner that you are trying to explain here.

He who assert must proof. hiyo burden usitake kunibebesha mimi wakati wewe ndie ulieallage.
 
I know kuna such kind of verses, but not in a manner that you are trying to explain here.

He who assert must proof. hiyo burden usitake kunibebesha mimi wakati wewe ndie ulieallage.

If you know kuna such verses, unahitaji proof ya nini?

Uendeleze ligi tu?
 
"Allah has set a seal on their hearts and their ears, and over their eyes is a covering; and for them is a great punishment"

Al-Fatinah

Ukianza kusoma Quran tu, verses kama nane into Al-Fatinah unakutana na habari hiyo inayo m contradict mungu wa upendo na haki.

Mungu wa upendo na haki atawahukumu vipi watu aliowazuia mwenyewe kumjua kwa kutomjua?

Huyu Allah mbona ana visa hivi?

Yeye ndiye mwenye uwezo wote, halafu anawafunga watu mioyo wasimjue, na kwa kuwa yeye ndiye mwenye uwezo wote, alishakufunga moyo usimjue, huna namna ya kuweza kumjua.

Halafubusipomjua (kwa sababu mwenyewe kafunga moyo wako usimjue) atakuhukumu kwa kutomjua.

Huyo ndiye mungu mnayetaka tumuamini?
 
You have failed to testify.
 
Kuna hili swala la kusema Mungu kashatupangia kesho yetu ipoje pia anajua wewe utafanya nini kesho kwa mantiki hiyo, Mungu ni muweza wa yote hata sisi atheist kashapanga tusikubali uwepo wake kama hajapanga na hivi tunafanyavyo tunajiamulia, basi tumtoe katika kundi la mpangaji wa yote. Hii ina maana hajui kesho yangu.

Naeleweka hivi!

Mkuu! Mbona Kujua na Kupanga ni vitu viwili tofauti? Unavihusianishaje kufikia kuja na hii hoja?

Tatizo ni fikra za kutaka Mungu angeumba A man like robot-Conditioned man, Mungu asingeshindwa kuumba kiumbe aina hiyo, lakini huo haukuwa Mpango wake.

Jambo jema kujiuliza, uwe hivi ama vile, u wa thamani gani katika ukuu na uwepo wa Mungu? U nani wewe katika Ukuu na Uwepo wa Mungu?
Anaita sasa!
 
Back
Top Bottom