Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Natumia msingi wa fasiri ya maneno hayo mawili ya Uthibitisho na UshahidiUnatumia msingi gani?
Siku hizi nimekuwa ni mtu wa kusoma baadhi ya post tu na kuandika mara chache sana kwasababu hakuna haja ya kuandika kwasababu mijadala ya hapa inayohusu Mungu imekuwa ya kiubishi zaidi ya kujifunzaKile ambacho kinadaiwa kiwepo ambacho hakipo na hakijawahi kuwepo ni mungu wenu huyo.
Nimeshaonesha kwamba isea ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe, na hivyo hawezekaniki kuwapo.
Sioni haja ya kuingia kwenye ubishi kwasababu haina faida kwa afya ya ubongo,kila leo tunalijadili hili na watu ukiwemo wewe mmekuwa mkiamua tu kukana kuwa hamjajibiwa kwasababu una uwezo wa kuandika chochote kwenye simu au tarakilishi yako
Yaani unaamua tu kukana bila sababu za msingi,hii inachesha sana
Hapa unarudia kitu kile kile tu kila siku,unadai kitu hakipo bila kusema ni kwa vipi hakipo na ushahidi hakuna
Mungu sio idea na hujaweza kuonesha kwamba anajipinga na maswali yako nimeshayajibu yote na kama kawaida yako umeamua tu kukana kuwa hayajajibiwa,kuna sababu gani ya kuendelea na huu mjadala?
Usijisumbue kunitaka nikuoneshe nilipojibu kwasababu nishafanya hivyo na hakuna kitu cha maana ulichojibu
Lakini cha ajabu ni kwamba kile ambacho wewe unakiona kinajipinga unadhani ndivyo kilivyo wakati inawezekana kabisa hujakielewa tu,lakini hata hili umeshindwa kulitafakari na unahitimisha tu kuwa kinajipinga
Kingine ni kwamba,ni wapi kitu kikijipinga kinakuwa hakipo?
Yaani nikitoa taarifa mbili za ajali na zikakinzana ajali inakuwa haipo kwasababu ya mimi kujikinza kwenye taarifa za ajali hiyo?
Interesting ...........!!