Nawashangaa sana watz.Nyerere ameshajiondokea zake,aliwakabidhi nchi takribani miaka zaidi ya 25 iliyopita,mmetumiaje muda huu kuijenga Tanzania muitakayo?kwa nini bado mnampiga vita marehemu asiye na impact yoyote kwa maamuzi yoyote mnayochukua hivi sasa?hebu zungumzeni ya kwenu tuwaelewe mnatakaje nchi iwe.Huyu mzee kama hawafai,muacheni,achaneni na sera zake,jengeni taifa jipya mlitakalo."Huyu mzee Nyerere muacheni,kajipumzikia,hawezi hata kunyanyua mdomo tena,what about you?umeifanyia nini Tanzania ambacho ni subject to negative or positive criticism?"ukimuona mtu kucha kuchwa anahukumu matendo ya wengine,ujue yeye hana cha maana anachofanya kinachowafanya watu wamhukumu,naam,hata yeye mwenyewe haoni cha maana kwake,ndio maana hukesha akizungumza na kuhukumu wengine.Watz wa leo tunakesha tukihukumu na kuzungumzia wale waliotutangulia,lakini tukimaliza kuongea hayo na kuulizwa tunataka iweje na tunaifikia vipi hiyo "iweje" yetu,ni bla bla bla blaa kama ilivyo pale Dodoma leo hii!