Alikuwa ananitafuta most times kwa ishu za kazi assignments, discussions. We were in the same class, same group of class activities na mie ndio nilikuwa mwenyekiti wa group letu.
Mwanzo wa ku date na huyo ex classmate wangu ni kuwa nilizinguanaga na huyo dogo at first.
Kuna kipindi kimoja cha likizo ya semister ya mwisho first year alianza kunletea mapicha picha alikuwa ameanza kunizeveza maana tulikuwa twawasiliana kwa simu tu kwao Migo Migo kwetu Tabata. Ilitokea akaendaga Mkuranga kusimamia lodge ya dada yake mpya ilianzishwa ila wafanyakazi wakawa na hujuma faida haionekani. Kwa sasa imekuwa kiwanja maarufu kwa wala bata na kikubwa tu inaitwa "Asante".
Alipoenda huko tukawa tunawasiliana freshi mwanzoni ila after a few weeks akawa amepunguza sana mawasiliano. Siku nzima kimya hakupigi. Unamtext hajibu. Ikafikia siu hapokei na akipokea anakwambia kachoka anahitaji kupumzika. Yani ikawa mateso. Mda anaosema analala ukipiga simu number busy mpaka saa 7 za usiku. Saa ingine hapokei simu mpaka umpigie na namba ngeni ila whatsapp unaona yupo online. Unamtext hajibu ila kitu ipo delivered.
Niliteseka mno kujua hatma yangu baadae nikampa ultimatum kuwa kama anaona kuna umuhimu wa mapenzi baina yetu then afanye maamuzi hio hali imenichosha. Siku za kufungua chuo zilikuwa zimekaribia akawa amejirudi ila guts zangu ziliniambia kuwa there was really something wrong behind ile shida alonipa and most likely cheating. Hivyo nikawa nishajikatiaga tamaa nikavuta demu kitaa nikagonga kupooza stess maana nliona kama mbwai mbwai. Yule demu akawa amenipenda mno akawa anantumia mesej za magazet zile kila saa.
Nilipanga siku tunayosafiri nikikutana na huyo dogo kwenye basi tu nimkague simu yake on the spot, na akileta ujeuri tu kunipa ntajua kuna jambo analoficha. Na kweli kama nilivyotaraji akawa mbishi kunipa akafuta meseji ndio akanipa. Mungu si athumani baadae tukiwa njiani jamaa likampigia hakupokea. Likamtumia romantic message ya safari njema nikaiona na kuisoma. Kumuuliza huyo nani akawa anababaika kuwa alikuwa moja ya mteja kule lodge kwao alimzoea tu na alimtaka sana ila hakudet nae. Baada ya kuona simu yake alitaka na yangu aone napo kama kunani na mie kwa makusudi sikufuta text za yule demu wa kitaa ili asijione mjanja sana. Nami nimefanya yangu kipindi alichonipotezeaga.
Katikati ya safari ndio text zikazidi ingia za yule demu wa kitaa. Huyo dogo akawa anaumia sana kuona vile kweli akawa anahisi nimemchit. Ila nilimpooza nkamwambia huyo ni just a friend niliwahi kusoma nae zamani ila sijamchanya koz pa yupo mbali zenji huko tulikutana mtandaoni tu. Dogo akawa ameshindwa kuielewa ile hali nikambembeleza wee na kumwambia kuwa sina kweli uhusiano nae na nitamkataa kama haamini ataona. Tulipofika chuo dogo akawa amenikaushia. Nikamwambia bas kama unahisi nimekukosea sana nisamehe maana pia wewe umenikosea kumbuka. Lets bury this tuendelee na mapenzi. Still hakuwa muelewa. Akaanza toa kauli mbaya kila nikimpigia nabembeleza tusameheane tuendelee mtoto hataki. Mashosti zake sijui wakampa bichwa eti a move on wakati hajawahi na hakuujua mziki. Alikuwa ananipenda mno by that time. Akanisumbua for about two weeks nikaamua nami nimpotezee niendelee na mengine maana alikuwa ana act kama ame move on kibishi ingawa roho iliniuma sana.
Ndipo nilipoanzisha uhusiano na huyo classmate wangu ambaye alikuwa a very close friend of mine, groupmate and she was so romantic and funny. Turns out alikuwa kwenye uhusiano na mtu ambaye hakuwa anamjali so katika process ya sharing of stories tukajikuta tupo in love with each other and thats where all it began. From sex to hiking, to schooling together tukawa kama vipepeo. She gave me love bila kipimo nikawa so obsessed nae.
Shida ikaanza pale dogo alipokuwa over jealous na kile ambacho alikiona baina yangu mie na classmate wangu huyo. She was dying inside kwa wivu na ndipo alipogundua thamani yangu kwake. Kiukweli huyo classmate alikuwa so hottt. Ni mzuri sana in every aspect na alimzidi kila kitu huyo dogo ndio vikaanza vilio sasa kwamba mbona nimempotezea. Akawa anapiga simu kila siku nazipotezea kama yeye alivyofanyaga maana alinionesha kuwa kasha move on. Anawalilia washkaji zangu kuwa she really loves me waniombee msamaha and shit.
Alilia kwa semister nzima the next semister nikamsamehe maana ilikuwa kama kero sasa.Pia nilitaka kuwa exclusive patner kwa yule mate wangu ili nitulie nae mazima maana at that time alikuwa anachepuka tu namimi. Ila msela wake bado anaendelea nae as well ila mate akawa mzito kufanya decision nikampunguza. Dogo nae ndipo shida zilipoanzia hapo akataka tukae wote ili ahakikishe kuwa siendelei na yule classmate wangu. She wanted that to happen so abruptly ila haikuwa rahisi kwangu kukata mawasiliano ghafla cause mate nlikuwa nimemkoleza sana tayari na i was always on her mind. Niliwaza jinsi gani angeumia juu ya hilo ila dogo alinibana to an extent akanipa ultimatum ni either tuendelee or nimcancel mate. Sikuwa na option ila kum cancel mate kutokana na situation ilokuwepo.
Ikawa kero kwa semister nzima ni kushikiwa simu muda wote akute chats zake humo ndio balaa. Alililia sana Amani ya moyo nikaahidi ataipata tu. Nipo serious nitampotezea kabisa after sometime naweka more efforts katika hilo. Mpaka mwisho wa siku nikaweza m cut off yule mate baada ya kukaa nje ya chuo mwaka mzima.
Now ile Amani ya moyo aloitaka nikaweza mpa ajiskie yupo free kwangu. Kilichotokea ndio hayo mapicha picha alonletea mpaka sitamani kupenda tena. Yale yalokuwa yanamkwaza yeye amenifanyia mimi bila huruma wala kujali hata chembe kwa kiburi kuwa mbona hata wewe ulinifanyiaga nilimuuliza is this a revenge? Akawa anakanusha ila akawa anatumia past kama silaha ya kunifanyia ushenzi ingawa tulishaongeaga yakaisha tukasameheana.
Heaven Sent atoto