Kweli ndoa ngumu, binti anataka kuolewa na boda boda

Kweli ndoa ngumu, binti anataka kuolewa na boda boda

Kwahiyo bodaboda🤔.... na wengine kina nani✍✍, mniambie mapema kabla December haijaisha😌😌
 
Nasikiliza mazungumzo ya mama na binti yake hapa.

Binti anajaribu kumshawishi mama yake amruhusu aolewe na dereva boda boda.

Binti: lakini mama huyu ni muelewa.

Mama : kwanini usitafute kijana msomi kama wewe.

Hivi kweli biashara zao zinaweza kuendesha kweli??

Binti ni pisi kali mno.

Naamini boda boda anajituma mno.

Haya wazazi kazi kwenu kazi kwa vijana zilizobakia ndio hizi za boda na ndio hao wakwe zenu.
Kwani bodaboda hana haki ya kuoa? Au kinachogomba ni nini hapo? Elimu kitu gani? Mwanamke awe na elimu asiwe nayo anabaki mwanamke tu. Jukumu lake kubwa ni kuzaa, mengine mbwembwe!
 
Halafu utakuta anae mponda bodaboda ni mwalimu anae lipwa laki Saba take home laki nne .

Ambayo in average amalipwa elfu 15 kwa siku ambapo sawa na boda anae beba vichwa 20 kwa siku
Mwalimu wa 700K anapata hio pesa kiurahisi most in soft works kazini ila Boda kupata hip 700K kwa mwezi atazunguka DSM mzima akibeba watu na kukoswakoswa kutolewa utumbo na mafuso

Mwalimu wa 700K ana mafao zaidi ya 60Million huyo boda hana fao hata la shiling kumi

Mwalimu wa 700K anaweza kopa zaidi ya 20Million bank akanunua hizo boda zaidi ya 10 huyo boda kukopeshwa 50K tu mtiti

Mwalimu wa 700K Hana risk kubwa ila huyo boda muda wote yupo kwenye hatari ya kupata ajari, kutolewa utumbo, kupata kilema, kupigana na watu balablani

Nk Nk

Itakuwa vizuri tukiendelea kumpambania bodaboda tu kwenye huu uzi kwa kusema "Kwani bodaboda sio binadamu" ila tukiingiza watu wengine kama mwalimu mwenye maisha Bora mara 100 ya huyo boda ni kumlowaza tu huyo boda

Bodaboda wenyewe vijiweni wanakwambia hii sio kazi wewe unawatetea nani
 
Huyo huyo mradi kuwe na upendo wa kweli kwa pande zote na hofu ya Mungu
 
Bodaboda wapo ambao wana kipato na maisha bora kuliko hata graduates
 
Bodaboda wana stereotype moja kwamba wote ni wahuni. Cha msingi ni kutambua watu hawafanani.
 
Una mawazo ya kizee sana.
Bodaboda ni kazi ya mpito tu.
Kesho huyo boda ni mtu mwingine kabisa
Inategemea na target ya boda mwenyew na huyo mwanamke atakuw na wazo gan juu ya kesho yao
 
Back
Top Bottom