Kweli ni ipi hapa kuhusu hekalu alilojenga Suleiman?

Kweli ni ipi hapa kuhusu hekalu alilojenga Suleiman?

Lakini mkuu naonaga pia wakristo wanasema kuna maandiko yanasema katika biblia kuwa kuna siku lazima Israel itapigwa na kutekezwa kabisa.

Yaani wanasema ili kiama kije (mwana wa adamu arudi) ni lazima israel ipigwe kwanza.

Huwa wanatumia maneno ya Yesu aliposema kwamba "pale mtakapoona Yerusalem imezungukwa na majeshi basi jueni mwisho wake umekaribia".

Sasa najiuliza ili Israel ipigwe wa kumpiga atakuwa nani, maana wote wanaompa back up wana nguvu kubwa
Hao waliotafsiri hivyo pia hawaelewi Yesu alichomaanisha!

Yesu hakumaanisha Israel itapigwa!
Mana yake ndo haya unayoyaona ss,vita hivyoo.....

Lkn kuhusu hekalu litarudishwa,msikiti utaondoshwa....
Ili hekalu litarudi hapo km likivyokua awali hata walinde vipi ....
 
Dini ya kiislam ni dini iliyojengwa kwenye propaganda nyingi sana za kuchanganya ukweli kidogo na uongo mwingi, ujenzi na ubomolewaji wa hilo hekaru ulitabiliwa na kuandikwa wenye vitabu vya torati na kila kitu kilienda kama ilivyotabiliwa.

Sasa ili kuweza kuaminisha umma wa kiislam kama dini yao imetokana na ibrahim,ilibidi kuanza kutunga historia za uongo kutoka katika torati na zaburi,hii pia ikaenda sambamba na kuvamia na kupora maeneo na miji ya wayahudi na kujimilikisha ikiwepo kujenga kwa huo msikini wa al qwasa mjini Jerusalem.

Ukiacha propaganda za kiislamu,bado hiatoria na ukweli uko wazi juu ya umiliki halali wa hilo hekalu na ardhi ya israel kwa Wayahudi.
Kumbuka pia dini ya Kiislam imekopi vitu vingi toka Ukristu, yaani ni dini ya kimkakati.
 
Suluhu ya huo mgogoro inapaswa itoke kwenye kufungamana na Iman yoyote kati ya hizo.. ukiniuliza mie nitakupa jibu rahs ingawa najua haliwezekana sababu ya wahafidhina wa pande zote mbili ( Wayahudi na Waislam)..

kwanza ujue mgogoro huo ni mgumu sababu shida sio tu hilo eneo shida imekwenda mbali zaid.. kuna mambo mawili

Imani na Aili ya watu kijografia

PALESTINES SUPPORT

Islam world
kinachowaleta Waislam wotekuwa nyuma ya Palestine ni swala la kiimaani .. maana kwa iman yao hiyo sehem ni takatifu kwao haipaswi kukaliwa na watu wa iman tofauti achilia mbali kujengwa kitu hapo .. so swala la kuuvunja huo msikiti si swala ambalo kwa waislam yaani sio tu haliwezekan hata kulifikiria ni haram

Arab World and Others
Jamii ya kiarabu na wengineo wachache wako nyuma ya palestina sababu kiasili palestine wanamizizi ya o hapo toka enzi na enz.. so kwa Waraab na wengineo wanaamini sio haki kwa Israel kuatak kujimilikisha hilo Eneo.

JEWS SUPPORT

Some christians denominations

kuna baadhi ya madhehebu ya kikristo wanasuport Israel, sababu wanaendesha iman zao kitofaut kidogo na majority ya christianity denomination. wao wanafanana kiasi na jews.. ingawa wanaamini katika Kristo Yesu na Jews hawaamini. ila supoprt yao iko imeegemea kwenye maeneo sababu wanaamini ni Holy place kwa wakristo na sio Dini zingine. kwa madhehebu kama wakatoliki, Walutheri na Walokole.. Eneo hilo ni Eneo Takatifu kiimani ila hawana itikadi kuwa haipaswi dini ingine kuishi hapo ndo maana unaona kama wako 50/50 yaani hawalichukuliii kwa imani kali kama waislam wanavyochukulia

Political Pychology
Hapa Israel support yake inatokana na faida za kisiana na kiuchumi hawa wanaomsapoti wanaitaka ( Ulaya na Marekani) its all about Dominance, ni katika kuhakikia wanakuwa na grip kwenye Arab world by any mans neccessary.

na kwasababu wanatofautiana kimitazamo na Arab world basi wanahakikisha kuwa soem hao kuko destablized ili waendelee kuwa na laverage

HITIMISHO
kwa mtazamo wa kijographia na Uasili Arabs wako biased sababu hata Israel wana mizizi hapo enzi na enzi infact toka karne za nane huko hilo Eneno lilikuwa linakaliwa na mataifa 2, Hebrew tribes, philistines baadae makabila ya Kiebrania yakagombana zikagawanyika na kuzaliwa tawala za Moab, Amon, israel, judah na mengine ( mind you sio Palestines maana hakukuwa na Nchi au Eneo linaloitwa palestine).

Na eneo hili ( Lavent, maana yake The East ndo jina la Eneo hilo au kama tunavyoita sasa eastern Mediterranean shores ila jina halisi ni CAANAN na waliokuwa wanakaa hapo kabla walikuwa wanaitwa Caananites) limekuwa likipitia kwenye umiliki wa falme mbali mbali wakibadilishana umiliki katika nyakayti tofauti.. kuanzia mapharaoi wa misri, wakaja kina mfalme nebu na babylon, wakaja kina Saladin na kina ASyria. wakaja kina Alexanders na Romans . na ofcourse kama mnavyojua kila zama inaacha vimelea..

So Hata hao wapalestina kiasili ni mchanganyiko wa Philistines ( watu kutoka Greece, na masalia ya wa caanan na hao wafilisti waliletwa huko baada ya kushindwa vita na wamisri na kukimbiolia caanan ku sattle ) ingawa baada ya Roma kuja kuangusha tawala za Philistines na baadaye na yeye kuangushwa na Ottoman kuja kuchukua basi jamii ya kizaz cha sasa cha Palestines kina asilimia kuwa ya Arab DNA sababu Ottoman alitawala kwa kipindi kirefu na eneo kubwa zaidi.. ila toka Enzi na Enzi hata kipindi cha Ottoman Jews walikuwepo..

So baada ya utawala wa Ottoma kuanguka na Ulaya kuja kushika hatam, kina uingereza France na wenzao ndo walishape na kutengeneza mipaka inayotumiak leo.. na ndio waliotoa uhuru kwa nchi za kiarabu... lakini ndio walileta Agendana kuisimmaia kwa nguvu kwa Israel kupewa Nchi yao

pendekezo la kwanza lilikuwa eneo ligawanywe kwa nchi tatu Palestine, Jordan na Jews, baada ya Jews kupewa sehem ya Uganda kukataliwa. na the iron on this is.. vikao vya majadiliano haya vilifanyika kati ya Ulaya na Arab leage yaani nchi za kiarabu ikiwemo iran, saudia na wengineo na wakakkubali kwa shart kuwa wao wapewe uhuru wa kujitawala. yaan waarabu wenzao wagawanywe ila wao wapate uhuru kamili.. na ikawa hivyo wakapewa uhuru na palestine ikagawanywa.. ingawa israel akwa anajiaribu kuiba Ardhi taratibu kila kukicha ..

cha ajabu wakat Israel anapewa utaifa walikuwa hawazi hata laki moja na wakawa wanaleta vurugu na kupora ardhi nashindwa kujua kwa nini palestine walikuwa wanawaangalia tu na wanakubali kuonewa... yaani hawakujiundia hata Jeeshi kujilinda..

Anyway kama nilivyosema suliuhisho ni mapak wakubwa wakikubali.. maana kama imewezekana sudani kugawanywa kwa nini ishindikane na kuendelea kuachwa taifa moja likibinywa... maana yake kuna watu wanafaidikia na huu mgogoro, the sad thing ni kuwa palestine wanashidnw akujua hilo hata watu wa asili yao Waarab wenzao nao ni sehem ya tatizo.. ikiwa walifanya mkutano kuwagawa toka mwanzo .. Waarab wangekuwa na nia ya kuikomboa palestien au kuleta Amani wangeweka shinikizo ikaweka miapaka na wao wakasaidia kulinda hiyo mipaka .. ila Israel anajiamulia anavyotaka
Umejieleza vema sana, shida kubwahujaigusa" imeandikwa adui wakwanza ni wana wa Israel waueni hata kama wamejificha chini ya mawe" kila kukicha linafundishwa na linasisitizwa lazima litekelezwe, ni amri ya mnyaaziMungu.
 
Habari wana JF.

Binafsi mgogoro wa wayahudi na wapalestina umenifanya nitafti vitu ambavyo hapo awali sikuwa na shida ya kuvijua.

Na hivyo vitu ambavyo nimetaka kuvitafti nimeishia njia panda tu bila kujua jibu sahihi ni lipi.

Ukiachana na mgogoro wa ardhi ulioko sasa kati ya wayahudi na wapalestina, kuna hili la HEKALU nalo ni kaa la moto.

Wayahudi wanaliita HEKALU,

WAKRISTO wanaliita KANISA na

Waislam wanaita MSIKITI

Yaani ki-ufupi wote watatu wanamaanisha kitu kile kile ambacho pia kinaonekana kuleta utata.

Sasa DINI ya KIYAHUDI na UKRISTO nitaiunganisha nitakapokuwa naelezea hili (maana tofauti ya dini hii huwa ni ndogo sana) lakini kwa UISLAM nitaielezea kitofauti kabisa.

KWA WAKRISTO : MCHUNGAJI MOSES MAGHEMBE anasema kwamba : HEKALU alilojenga suleiman liliharibiwa kwa mara ya kwanza na mfalme NEBUKADREZA kutoka Babeli mwaka 586 BC, kabla ya kuzaliwa YESU.

Alafu likaja kujengwa mara ya pili na DAUD nafikiri, lakini likaja likaharibiwa tena mara ya pili na Jenaral TITUS wa roman empire mwaka 70 AD baada ya kuzaliwa YESU.

Lakini mchungaji MAGHEMBE anaendelea kusema kwamba biblia imetabiri unabii wa kujengwa kwa HEKALU mara ya tatu kabla ya YESU kurudi tena.

Anaendelea kusema kuwa tayari mipango ya ujenzi imushawekwa tangu mwaka 1989 ambapo kuna kampuni ya kiyahudi imejipanga kwa ajili ya hilo, na anaesimamia mipango ya ujenzi wa HEKALU alimataja kwa jina sema nimemsahau kidogo ila ni kama RABI FRAIMAN nadhani nnavokumbukia.

Na anaendelea kusema kwamba tayari vitu vyote vilivyokuwa ndani ya HEKALU wayahudi washavitengezaga imebaki tu kusimamisha jengo.

Lakini kamalizia kwa kusema kinacho chelewesha ujenzi wa HEKALU hilo hadi sasa ni "kuna jengo la dini nyingine limejengwa pale lilipokuwa HEKALU la SULEIMAN" 😃😃😃

Hapana nadhani alimaanisha MSIKITI WA wa AL-AQSA sema aliogopa kutaja wazi.

Na kasema wayahudi hawawezi kujenga jengo HEKALU sehemu nyingine tofauti na pale lilipo hilo jengo la DINI nyingine (Bila shaka ni MASJID AL AQSA ana maanisha).

TUJE KWENYE UISLAMU sasa : Kwa mujibu wa SHEKH AL-HAJI SULLE yeye hatumii neno HEKALU bali anatumia neno MSIKITI.

SHEKH SULLE anasema kwamba MSIKITI ulijengwa na nabii Suleiman na ukaja kuharibiwa na NEBUKADREZA mwaka 586 BC.

Anaendelea kusema kwamba Msikiti huo baada ya kuharibiwa na NEBUKADREZA ulikuja kujengwa tena mara ya pili lakini ukaja ukaharibiwa tena jenaral TITUS wa RUMI Mwaka 70 AD.

Nilicho furahi hapa ni kwamba MAELEZO ya SHEKH SULLE yameenda sambamba kabisa na ya mchungaji MAGHEMBE bila kutofautiana hata kidogo ila tu tofauti ipo kwenye huyu anatumia neno HEKALU na mwingine anatumia neno MSIKITI 😂😂😂

Lakini nikaona tofauti za majina siyo isssue kubwa kwa sababu zote ni nyumba za IBADA 😂

SASA KUBWA KULIKO NI HII HAPA : Mchungaji maghembe anasema HEKALU la tatu bado halijajengwa ila mipango ya kulijenga imeshakamilika shida ni moja tu, mahali lilipokuwa hekalu pana jengo la dini nyingine 😅 (masjid Al Aqsa) na wayahudi hawawezi kujenga hekalu tofauti na hapo.

Lakini SHEKH SULLE anasema MSIKITI wa Tatu ushajengwa tayari na ndiyo huo unauona sasahivi MASJID AL AQSA ambao uko Jerusalem.

Anasema msikiti huo ulijengwa kwa mara ya tatu na KHALIPHA kutoka MADINA, SAUD ARABA mwaka 689-691 aliyeitwa ABD AL-MALICK 😁😁😁

Sasa hapa nishachanganyikiwa nashindwa kutambua ukweli uko wapo 😁😁😁

Kwa Wayahudi na Wakristo HEKALU/KANISA kwa mara tatu bado halijajengwa ila ndiyo lipo kwenye maandalizi ya ujenzi, na kinachokwamisha ujenzi huo hadi sasa ni uwepo wa jengi la dini nyingine, yaani msikiti wa AL-AQSA.

Lakini kwa waislam MSIKITI huo alio haribiwa na RUMI chini ya jenerali TITUS tayari umeshajengangwa kwa mara ya tatu na KHALIPHA ABD AL-MALICK kutoka MADINA tangu mwaka 689-691 AD.

Sasa kina nani wapo sahihi ? Huu mgogoro ni mgumu sana kwa kweli.

Je, wayahudi watakuwa tayari kuubomoa msikiti wa AL-AQSA ili wajenge hekalu lao ? yatakuwa maamuzi magumu na ni hatari yanayoweza kusababisha umwagaji damu mbaya sana, maana ni mgongano wa imani tofauti.

Lakini Je, Waislam watakubali msikiti wao ubomolewe na wayahudi ili wao wajenge HEKALU lao ?

SHEKH SULE anasema waislam wote duniani wapo tayari kuulinda huo msikiti kwa gharama yeyote ile.

Hapo ndipo kitendawili kilipo .
H. kuna kitu kama hicyo. Ni hadithi za kutunga ambazo zimekuwa zikilindwa kwa uongo na vitisho
 
Umejieleza vema sana, shida kubwahujaigusa" imeandikwa adui wakwanza ni wana wa Israel waueni hata kama wamejificha chini ya mawe" kila kukicha linafundishwa na linasisitizwa lazima litekelezwe, ni amri ya mnyaaziMungu.

kaka huko sasa utazidi kuchochea.. nimekwambia tuweke iman pembeni ndo suluhu itapatikana.. tukianza kufukua makaburi kwa kufata vitabu hivi vilivyoandikwa na ancestors basi hautakwisha
 
Linafundishwa wapi, msikitini au kanisani
 
kaka huko sasa utazidi kuchochea.. nimekwambia tuweke iman pembeni ndo suluhu itapatikana.. tukianza kufukua makaburi kwa kufata vitabu hivi vilivyoandikwa na ancestors basi hautakwisha
Kuna muda huwa nakaa na kufikiri kwamba "kwanini Mungu anaitwa wa Upendo hufanya watu wauane" huwa sipati majibu kwa kweli.

Wapalestina wanat teseka sana kwa kweli.

Sasahivi GAZA ni kama jehanum.

Lakini ninacho shangaa waziri mkuu wa zamani wa israel (RAPHAEL BANNETI) anasema kwamba "suala la wapalestina kuteseka huko GAZA wao haliwahusu na wala si suala lao, kama ulimwengu una wahurumia basi uka wasaidie" .

Na kauli moja ya hovyo sana jamaa ametoa na viongozi wa dunia wanapiga kelele tu kuwa tunasimama na Israeli 🥲
 
Hao waliotafsiri hivyo pia hawaelewi Yesu alichomaanisha!

Yesu hakumaanisha Israel itapigwa!
Mana yake ndo haya unayoyaona ss,vita hivyoo.....

Lkn kuhusu hekalu litarudishwa,msikiti utaondoshwa....
Ili hekalu litarudi hapo km likivyokua awali hata walinde vipi ....

Duuuh...mambo ni mazito haya.
 
😅😅😅

Haya mambo ya imani ni magumu sana.

Wao (waislam) wanasema Quruan ni correction ya Biblia kwa sababu kwenye Biblia ukweli ulipotoshwa na warumi
Na kwenye Qur'an kuna haya za Shetani alizopewa Mohammed ziitwazo Satanic Verses zimefutwa makusudi tu ili kupotosha watu....sema tu watu haswa Waislam si watu wapendao kusoma na kutaka kujuwa ukweli wakiamini kuwa Qur'an ni kitabu cha Mungu na hakina makosa wakati si ukweli hata kidogo, Na hii ndiyo athari ya kutokusoma. Waislam wengi wanaamini kuwa Mohammed alikuwa mtu mwema wakati si ukweli hata kidogo, wanashindwa kujiuliza kwanini Wayahudi walimuua na Waarab wenzake walikuwa wanamuwinda kumfanyia umafia pia.
 
Hivi kumbe mohammed aliuliwa na wayahudi 🤔

Lakini kinachonishangaza zaidi ni wanaposema kwamba "Quran ni kitabu kilicho shushwa direct na Mungu kutoka mbinguni kama kilivyo leo" kwamba hakikuandikwa na mwanadamu.
 
Suala la Mashariki ya kati limenijenga Imani yangu mala Mbili.

Nimekoma sana kiroho na imaniyangu IMEKUWA kamili machoni Mwa Bwana.

LIMENIFANYA NIMUAMINI MUNGU KWA UTIMILIVU WOTE.

Vijana JifunzeniMambo ya mashariki ya kati mtafika hatuna mtaanza kumuona Mungu.

Na nyinyi WA makobazi njooni kwa Yesu.
Limekujengaje kiimani mkuu. We una nuru nzuri kiroho ila haupo serious. Nisaidie nami nijue limekujengaje?
 
Hata mimi najua ramani ya namna jengo la hekalu litakavyokuwa wanayo.

Ila kipengele ni kuibomoa Al-Aqsa ili ujenge hekalu, hapo ndipo itakuwa vita
Hilo mbona lipo wazi japo watasema tunawakashfu. Dini ya kiislama.ni dini ya Mpinga Kristo. Ni dini iliyojengwa juu ya Uyahudi na ukristo na imejengwa katika mwili. Wana mafundisho mazuri ya kustaarabisha na kumfanya mwanadamu amjue Mungu. Ni kweli imejengwa kwenye mafundisho ya kutenda matendo mema na utoaji. Hilo ni kitu kizuri ila wamekosa kitu kimoja. Kumkiri Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi wa Maisha yao. Wamekosa kumkiri na kumjua kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Wao wanamchukulia na kumdharau kuwa si kitu.

Biblia inasema wazi kuwa Roho ya Mpinga Kristo ni ile Roho inayopinga kuwa "Yesu hajaja kwa Jinsi ya mwili I.e kupinga uungu wa Yesu". Mpinga Kristo au "Masih Dajali" wanavyosema wao atakapodhihirika katika mwili atakuja kusuruhisha na kupatanisha kati ya mataifa baada ya kuvunjwa kwa huo Msikiti. Tukio hilo litatokea baada ya Unyakuo wa Kanisa. Biblia ipo wazi kuwa atafanya Amani na Patanisho kwa miaka 3.5 na kisha baada ya hapo atawageuka Wayahudi na wakristo walioachwa kwenye Unyakuo na ndio kutakuwa na dhiki kuu kwao kwa miaka 3.5

Baada ya hapo, Kristo atakuja mawinguni akiwa na watakatifu wake naye atafanya vita dhidi ya Islam waliojikusanya kupambana na wayahudi ili kulifuta taifa la Israel katika uso wa duniani. Jeshi la watu zaidi ya 20M waliotoka pande zote za nchi watakusanyika kwenye bonde la Megido kwa ajili ya siku ya Bwana. Naye Kristo atawakatilia mbali hao watu na Mpinga Kristo na Nabii wa uongo watakamatwa na kisha kutupwa kwenye ziwa la Moto.

Kwa mtini jifunzeni na muyaonapo hayo jua bwana yu karibu kurudi. Yajayo hayafurahishi hata kidogo.
 
Hata mimi najua ramani ya namna jengo la hekalu litakavyokuwa wanayo.

Ila kipengele ni kuibomoa Al-Aqsa ili ujenge hekalu, hapo ndipo itakuwa vita
Yes
Actually Kuna vita Bado itakuja, inaitwa vita ya 'Almagedon'
Hapo ndo watakaposhuhudia muumba wa mbingu na nchi akitimiza aliyoyanena....
 
Hilo mbona lipo wazi japo watasema tunawakashfu. Dini ya kiislama.ni dini ya Mpinga Kristo. Ni dini iliyojengwa juu ya Uyahudi na ukristo na imejengwa katika mwili. Wana mafundisho mazuri ya kustaarabisha na kumfanya mwanadamu amjue Mungu. Ni kweli imejengwa kwenye mafundisho ya kutenda matendo mema na utoaji. Hilo ni kitu kizuri ila wamekosa kitu kimoja. Kumkiri Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi wa Maisha yao. Wamekosa kumkiri na kumjua kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Wao wanamchukulia na kumdharau kuwa si kitu.

Biblia inasema wazi kuwa Roho ya Mpinga Kristo ni ile Roho inayopinga kuwa "Yesu hajaja kwa Jinsi ya mwili I.e kupinga uungu wa Yesu". Mpinga Kristo au "Masih Dajali" wanavyosema wao atakapodhihirika katika mwili atakuja kusuruhisha na kupatanisha kati ya mataifa baada ya kuvunjwa kwa huo Msikiti. Tukio hilo litatokea baada ya Unyakuo wa Kanisa. Biblia ipo wazi kuwa atafanya Amani na Patanisho kwa miaka 3.5 na kisha baada ya hapo atawageuka Wayahudi na wakristo walioachwa kwenye Unyakuo na ndio kutakuwa na dhiki kuu kwao kwa miaka 3.5

Baada ya hapo, Kristo atakuja mawinguni akiwa na watakatifu wake naye atafanya vita dhidi ya Islam waliojikusanya kupambana na wayahudi ili kulifuta taifa la Israel katika uso wa duniani. Jeshi la watu zaidi ya 20M waliotoka pande zote za nchi watakusanyika kwenye bonde la Megido kwa ajili ya siku ya Bwana. Naye Kristo atawakatilia mbali hao watu na Mpinga Kristo na Nabii wa uongo watakamatwa na kisha kutupwa kwenye ziwa la Moto.

Kwa mtini jifunzeni na muyaonapo hayo jua bwana yu karibu kurudi. Yajayo hayafurahishi hata kidogo.
Naamini kapata mwanga
 
MImi bhan kwenye suala la dini huwa nipo neutral sana.

Sina maana ya kwamba siamini uwepo wa Mungu, hapana.

Neutrality yangu ipo kwenye "Dini ipi ni sahihi kwa Mungu (perfect religion)" hapo ndipo U-neutrality wangu ulipo.

By the way nakubaliana zaidi na hizi dini tatu (Uyahudi,Ukristo na uislam) kwa maana ndizo naona huamini katika Mungu mmoja (Yehova/Allah), lakini ukinambia ni dini zipi kati hizi tatu ni sahihi zaidi, huwa nabaki neutral sana ani.

Hii ni kwa sababu tofauti ya hizi dini tatu huwa ni ndogo sana.

Ukristo umejengwa mizizi yake ya imani kutoka dini ya kiyahudi isipokuwa tu wametofatiana kwenye Yesu/Messiah.

Kwa dini ya kiyahudi Yesu/messiah hajaja bado wanamsubiri mpaka leo, ila kwa wakristo Yesu alishakuja na akakataliwa na wayahudi.

Hiyo ndiyo tofauti yao kuu kati ya uyahudi na ukristo, ni kuhusu Yesu/Messiah tu.

Lakini pia Ukristo na Uyahudi una tofautiana sehemu moja tu kwamba "Uyahudi na Ukristo hazimtambui au kumzungumzia Mohammed kuwa ni mtume wa Mungu, nikiwa na maana hajaandikwa kabisa kwenye vitabu vya dini hizi mbili (Biblia ya kikristo au kiyahudi hazijamzungumzia mtume Mohammed).

Na muda huo huo waislam wanaamini Mohammed ndiyo mtume wa mwisho wa Mungu.

Lakini ukitoka Mohammed, mitume ambao wako kwenye dini zote ni wale wale, sijui kina Ibrahim, Musa n.k.

Ila tatizo kubwa sasa liko hapa "mitume na manabii hao waliopo kwenye hizi dini wamezungumziwa katika matendo tofauti sana"

Mfano : Ukristo unasema Yesu alizaliwa kwenye hori/zizi la ng'ombe, Uslam unasema Maryam alimzaa Yesu jangwani chini ya mtende tena akiwa peke yake bila msaada wowote, then kukatokea miujiza ujiza pale.

Ukristo unasema Yesu alisubuliwa akafa alafu akafufuka na kupa mbinguni, Uislam unasema Yesu aliondoshwa na Mungu ki-miujiza akapaishwa mbinguni then watu waka-msulubu Yuda wakijua ndiyo Yesu 😅

Ukristo unasema aliyetaka kutolewa na Ibrahimu kuwa Sadaka alikuwa ni Isaka na eneo ilikuwa ni Yerusalem lilipo jengwa HEKALU la Suleiman, Uislam unasema aliyetaka kutolewa na Ibrahim kuwa sadaka alikuwa ni Ishmael (ismail) na eneo ilikuwa ni Mecca ilipojengwa Al-kaaba leo hii 😅😅😅

Utofauti wa stori ni nyingi nikisema niandike hapa nitajaza page, nimeamua tu niseme baadhi.

Lakini nilichotaka kusema ni kwamba "Utofauti wa hizo hadithi za matukio bado hazitoshi kumfanya mwanadamu asiamini uwepo wa Mungu".

NB : Mimi ni Mkristo na namwini Yesu kama mwana wa Mungu ila simwamini Yesu kama Mungu, maana Yesu ndiye aliyesema yeye ni mwana Mungu na hakusema yeye ni Mungu.

Japokuwa waliokuja kuandika kuhusu Yesu badae ndiyo waliokuja kuonesha kana kwamba Yesu alikuwa ni Mungu, japo mimi siamini katika hilo kwa sababu moja keamba "hakuna mahali kwenye Biblia Yesu amesema yeye ni Mungu, bali amesema tu Yeye ni mwana wa Mungu aliyegumwa na Baba (Mungu) kuyatenda mapenzi ya Mungu.

Na hata alipopaa alisema "naenda kwa Baba kuwaandalia makao ili nilipo mimi nanyi muwepo, maana nyumbani mwa Baba yangu mna makao Mengi".

Sasa huwezi kulazimisha kusema Yesu ni Mungu wakati yeye mwenye alikataa kuwa siyo Mungu.

Japo waliokuja badae kuandika kuhusu yeye kama kina TITO walikuja kuonesha Yesu alikuwa ni Mungu.

Lakini pia mimi siamini kama Uislam unamdharau Yesu, ni kwamba tu wana mwamini kama nabii na alikuwa na nguvu kuliko hata Mohammed.

Na hata wanasema Quran imetaja jina la Yesu mara nyingi kuliko la Mohammed, so mimi sidhani kama anadharauliwa na uislam au waislam.

Ni vile tu wame-base kwa Mohammed kwa sababu ndiye mtume wa Mwisho wa Mungu kwa mujibu wa imani yao.
 
Back
Top Bottom