Kweli tunapiga vita ugaidi au ni vita dhidi ya uislam?

Status
Not open for further replies.

Mhe. Rais aliyajua haya ndiyo maana akawawekea IGP muislamu,naamini angekuwa mkristo mngesema hujuma za wakristo.Je sasa muislamu mwenzenu anafanya vita dhidi ya uislamu? mm niwashauri waislamu msiwe wepesi kukimbilia kutaja udini katika matukio ya aina hii. mm siamini kuwa waliotendewa huo unyama ni waislamu peke yao kwani waislamu wana ndugu ambao sio waislamu na wengine hawana dini ambao wengine matukio haya yaliwakumba

mbona hauzungumzii vijiji viwili au vitatu vya Serengeti zilivyofutwa kwa nguvu ya polisi(nyamuma) na haya mnayolalamikia yalifanyika kule? je wakristo nao waamini kuwa ile ilikuwa hujuma dhidi ya ukristo iliyofanywa na waislamu? jibu ni hapana

tukumbuke ripoti ya kamati ya bunge ya juzi watu wametendewa unyama na uovu mkubwa ambao mwingine hata mkoloni asingeweza kuwatendea watu hawa lakini wametendewa. katika watu waliotendewa uovu walikuwemo watu wenye dini na wale wasio na dini. je hapa napo tuamini kuwa hayo yametokea kwasababu ya kutaka kuhujumu dini ya mtu, jibu sio kweli. tatizo naliona liko kwa watendaji wanaotumwa, inaonekana hawana uweledi wa taaluma yao hivyo wanafikiri wakifika wakachoma nyuma na kuwatendea watu uovu watakuwa wamewafurahisha mabosi zao na watapandishwa vyeo

mm niwashauri vijana wenzangu, kuwa udini sio mzuri kuuendekeza mwisho wa siku tutauana kwa madai ya kutetea dini zetu. hakuna vita mbaya duniani kama vita ya udini, mtu anaweza kufanya chochote ili kutetea dini yake

ushauri wangu ni kuwa nchi yetu imekumbwa na matukio mengi ya mauaji na utesaji wa watu na hakuna mtu ambaye hata leo amewajibishwa watu wakaona kweli hatua muhimu zimechukuliwa. la msingi kama nchi tujiulize ni wapi tulipokosea? kubwa zaidi hakuna uwajibikaji miongoni mwetu na viongozi wetu,kwani kuna makosa mengi yanafanyika ambayo watu walitakiwa washitakiwe hata kufungwa kabisa lakini hakuna hatua iliyochukuliwa hadi sasa.

naishauri ccm yenye serikali, iache mchezo kwenye maisha ya watu, kama ilivyoanza kuwashughulikia mawaziri mizigo na watendaji wasiofaa iongeze nguvu haya tunayoyaona yatatoweka kabisa. Lakini ccm ikijisahau wananchi wataendelea kuumia na matokeo yake wataifanya jamii iwachukie na kuwapenda wapinzani

nasema haya unayosema, si haki mtu kutendewa,tuwasiliane na watetezi wa haki za binadamu ili hatua zichukuliwe na wanaohusika wawajibishwe haraka iwezekanavyo. Naamini Mhe. Rais hatayafumbia macho, atachukua hatua ya haraka kama alivyofanya kwa mawaziri waliokiabisha chama, Serikali na Watanzania kwa ujumla. hakika hawa ndugu zangu wanastahili fidia kwa kadiri utu wao ulivyodhalilishwa

kingine tuombe taarifa ya uchunguzi ya kina sio kama ulivyoandika naona imekaa kiuchokozi sana, waandishi wapelelezi wafanye kazi yao kisha watuletee taarifa kwanini hatua hizo zilichukuliwa. unaweza kushangaa wale unaowatetea wao ndio wakawa wenye makosa? tuombe tume ifanyie kazi hili itueleze ukweli bila aibu, ndipo tutakuwa katika nafasi nzuri kuhitimisha mjadala huu
 
Juve2012.
Kwanza kabisa nataka nikujulishe uislamu unapingana na UGAIDI usione hivi vikundi vinavyo jilipua kwa mwamvuli wa kutumia uislamu ukawahukumu waislamu wote.

Ukitaka kujadiliana siku zote mambo ya imani jadiliana kwa kupitia vitabu sahihi vya huyo unaejadiliana nae sio kukurupuka na kuingia kwenye mtandao na kucopy and paste kama wakristo wengi wanavyo fanya huku kwenye mitandao ya kijamii.

Utakuta mtu amechukua hadithi ya mtume Muhamad (S.A.W)na kuileta huku bila hata kujua wanachuoni/maulamaa wa kiislamu wanaizungumziaje hiyo hadithi ni sahihi au dhaifu.

Na katika uislamu kuna somo linaitwa "mustalawal hadithi" ni lazima ujue haya mambo ndio uweze kuelezea mambo ya hadithi na ujue pia kitu kinaitwa "ilmu rijal" ndio utajua mpokeaji wa hadithi hii ni mkweli au muongo na mengineyo.....

Kwahiyo muislamu haruhusiwi kumuua mkristo hata kama anaishi nchi iliyo chini ya dola ya kiislamu, mkristo anahaki ya kuishi pale bila kubughudhiwa ilimradi atii sheria zilizoko pale na yeye atafanya ibada zake huko aliko bila ya kudhuriwa.

Kwahiyo haya yaliyotokea Kilindi mimi nilishangaa sana kwataarifa nilizo nazo nasikia ulikuwa ukionekana suruali yako ni fupi na unandevu nyingi unakamatwa unaonekana wewe ni GAIDI.

Napenda kuwafahamisha mtu kufuga ndevu au kukata suruwali sio GAIDI kwasababu haya ni mambo ya kiimani wala hayahusiani na UGAIDI na wakristo wengi wanapenda kuwashutumu watu wenye kukata suruali na kufuga ndevu na kuwaita AL QAIDA hicho kitendo sio kizuri na hakitupendezi sisi ni hayo tu.

Ahsanta.
 
Haya unayoyasema usidhani waislamu wanakurupuka na hii yote inatokana na marekani kwasababu leo hii kila kinachotokea nchi za kiislamu utasikia kuna magaidi kila tukio baya ni waislamu ndio maana utaona waislamu nao wanalalamika.

Yanayoendelea Afrika ya kati unayasikia lakini pale huambiwi ni ugaidi unaendelea na miskiti inachomwa moto wao hilo hata haliwasumbui inasikitisha sana halafu wanajeshi wa Ufaransa kutuliza ghasia!
 
Samahani Mkuu Bilal bin Rabah;

Ebu Naomba Tujaribu kuzichambua Taarifa ya Mleta mada ndugu Mohamed Said na ndugu Bopwe aliyo ileta ya gazeti la Nipashe kisheria!

Sio km nakupinga Mkuu hoja zako ila nachopenda tuangalie haya mambo Kwa pande zote! Ili tuweze kuiona Dhuluma dhidi ya Imani yako Mkuu!

Narudia tena samahani km ntakua nimekukwaza!

Thx!
 
Ntuzu.
Hebu jibu kwanza hayo maswali matano aliyouliza Bopwe kwenye hiyo taarifa kwenye gazetila nipashe halafu tuendelee na "mnakasha"
 
Ntuzu.
Hebu jibu kwanza hayo maswali matano aliyouliza Bopwe kwenye hiyo taarifa kwenye gazetila nipashe halafu tuendelee na "mnakasha"


Mkuu! Kwanza Nakushukuru Kwa hoja zako!

Nimeyapitia hayo maswali ya Mkuu Bopwe! Nimeona kuyajibu Mimi km Mimi ni magumu! Ila ninachweza Kusema km tungepata wataalamu Wa sheria wangetusaidia juu ya hili na kuweza ata kuyajibu hayo maswali ya ndugu Bopwa!

Ila ninachoweza Kusema ndugu Bopwe ameuliza maswali ya mwisho kabisa juu ya kadhia Hiyo na Kwa swala hili km hili lilivyo alikua anapaswa kuanzia mwanzo Yani kwenyechanzo mpk huko Kwa namna gani Polisi walitekeleza Hiyo Oparesheni Yao! Na ni vema kuangalia pande zote mbili!

Thx
 
That is islaam that the world has lived with for centuries until the arrival of Osama bin laden and the likes. Arab and palestinian resistence to occupation has always taken a secular ideology until islamic fundamentalists took the stage and refused to put a difference between western imperialism and christianity and hence starting a hate campaign against christians. So what I am making reference to is the present time.
 
mkuu kinachoandikwa kwenye mainstream media kinakuwa na chembe ya ukweli kuliko conspiracies ambazo hazibebi mainstream thinking na mara zote zimejaa pessimistic views.
pia ujue hata habari inapoandikwa mwandishi naye anayo mapenzi binafsi anaweza kuwa biased. majuzi obama aliruhusu gaidi mmoja maarufu sana na kiongozi kutoka taliban aachiwe huru kwa lengo la kwenda kuwashawishi wenzake waachane na uasi dhidi ya marekani na hii ikiwa na lengo kuwa ni mkakati mpya wa marekani kufikiria kuacha matumizi ya nguvu kupambana na ugaidi kwakuwa ni muda mrefu hayajaonyesha mafanikio.pia kuna swala la kufunga gereza la guantanamo, lakini wapo watakoamini kuwa marekani inashirikiana na magaidi. marekani ndio ilipeleka azimia UN kuhusu vita dhidi ya ugaidi iweje leo tuamini kupitia habari za vichochoroni kuwa marekani ndio wanaopika kilakitu.
 
Wengi tunaamini ukiwaua watu wasiokua na hatia yoyote ni ugaidi na kama ni muamini wa dini yoyote ni dhambi kwa mwenyezi mungu
 

pengine ni kwa maslahi ya taifa katika kuzuia machafuko ya kidini nchini yanayojitokeza nchini, labda chiku akajaribu kubadilisha kauli kwa kutumia lugha za kisiasa, ama hawakuwa wametaarifiana, japo sina hakika kwamba wananchi wanatakiwa waamini kauli ya nani kati ya mkuu wa mkoa na mkuu wa polisi. ushauri wangu hapa ni kuwa huyu shekh na wenzake warudi wakamuulize tena bi chiku aseme alichokisema mwanzo na ahojiwe kuwa mbona kauli yake inatofautiana na ya mkuu wa polisi?
pia nilishaeleza chiku sio afisa upelelezi ni mwanasiasa tu sitegemei atoe habari za kiuchunguzi. Ni daktari tu na mtoto mdogo wanao uwezo wa kutoa ushahidi utakaoaminika kwa wananchi kwani unakidhi vigezo vya kiupelelezi zaidi na sheria za kimahakama. na ikumbukwe kwenye lile tukio walikuwepo watoto waliodaiwa kuwakana wazazi wao kuwa sio waislamu halisi.
mwisho nilitoa maelezo nilihitimisha kuwa vyovyote vile hata kama jeshi la polisi lina makosa kiasi gani bado halina lengo la kupambana na uislamu.
 

mkuu labda nifafanue, ni kawaida source zinazoaminika duniani mbali na kuaminika huko pia zina weza kutofautiana kimtazamo. mfano CNN,BBC, SKY NEWS zinaweza kutofautiana kwa mtazamo na Aljazeera, CCTV. though they all credible sources.
lakini kutumia conspiracies kama source ya kupata habari mfano wakina david icke, huu utakuwa ni upuuzi. watu makini wanaheshimu mainstream thinking na sio skepticism from minor. mwenzako amenielewa hapa. mtu makini anaweza kutambua credible sources, na anajua hizi sources zinatabia ya tofautiana pia hata katika habari ya aina moja.
 

Crabat,
Umeyaweka sawa kabisa.

Hakika hiyo ndiyo Tanga waijuayo wengi.
 
Umekosa cha kukanusha hapo umeishia kutoa kejeli tu, huu ni ukweli usiopingika.
Uenezaji wa uislamu sio persuasion, ni kuforce.

Nimeipenda hii;
Waislamu wakiwa

1%, utawaona ni wapole sana, huku wakirecruit mionr groups, jail hadi street gangs,
Wakifika 5%, wanaanza kudai halal food, inawapa ajira ya kuandaa vyakula,
8%, wanaanza kudai wajitawale kwa sharia zao tu,
20%, hapa tegemea maandamano na vurugu,
40-50%, ubaguzi na chuki dhidi ya wasio waislamu,
80%, hapa ni genocide na non believer cleansing, uchomaji wa makanisa na mauaji ya mapadre na wachungaji ni jambo la kawaida katika asilimia hii mpaka ifikie 100%waislamu.
Lengo likiwa ni kusilimisha dunia nzima na kuweka sharia.

Haya ndio malengo halisi ya uislamu, ndio maana malalamiko wa waislamu hayawezi kukoma mpaka dunia nzima itakapo silimu.
We kiumbe wa ajabu sana!
Unatuwekea SOURCE FROM "CIA" Halafu unaweka swali mbele yake!!

We ulivyo msukule unategemea CIA wataongea mambo MAZUUURI KUHUSU WAISLAMU SIO??

Elimu za kata ni janga kuu!!
Akili za ku copy and paste huwezi kuzigeuza.
 
My Dear Kmbw hope u r OK; Hakuna ukweli kuwa tuna hate Christians !! NO NO and big NO !! The last wife of our prophet SAW was a Christian.... Muslim are respecting the CHRISTIANS and for year they live side by side. Mkuu acha kunukuu kama kasuku maneno ya WACHONGANISHAJII waisilamu wema na Waumini Islam wa kweli hujua Obligations za Dini zote zilizoteremka. Asilimia kubwa tumesoma as one nation na tunaiishi as One humankind. Heshima za kijamii zinadhihirisha uaadilifu wetu juu ya wakiristo na dini za mbinguni..... Tafadhali fungua kifua uone uzuri na amani ya wenzio... usijifunge na kubobea chuki zilizopikwa. Kwa miaka mingi nchini tunasafiria Mtumbwi au Meli moja "sasa kama kuna wabaya wanaanza kutoboa mgongo / kizingiti wa chombo chetu, Basi tutazamaa majini. Mungu apishe mbali... With love and prospects together. Good Luck and stay in peace.
 
Its good to read such kind words. Thanks
 
hakika maneno ya msingi sana hayo
 
Jamani huu ni upumbavu. tutakao bahatika kuishi miaka 10 mbele mtakataa kama mliwahi kujadili huu upumbavu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…