Mzee Mohammed Said na waislam wote nawapeni pole.Pole yangu naitoa iwapo tu tukio hilo ni la kweli lakini hata kama si la kweli bado nitaendelea kuwapa pole waislam kwa kuubeba huu mzigo wa "ugaidi" iwe wanataka au hawataki.Hii ni perception inajengwa duniani kote na watu waislam na wasio waislam kutokana na matendo ya watu fulani wanaojiita waislam na watu fulani wanaojiita anti terrorist experts(U.S n.k).Sijafahamu kama nyinyi waislam mnaujua ukubwa wa tatizo hili lakini mie naliona kubwa sana.Unapogusia jambo linalohusu mamilioni ya watu duniani si jambo dogo hilo na hatupaswi kuliongea kwa maskhara kama wafanyavyo baadhi ya watu hapa.Huwa nakuwa mwangalifu na mambo ya uislam kwa kuwa najua katika kizazi chetu hiki,hata kama ni kwa lazima bila kupenda,kuna uhusiano wa karibu kati ya uislam,ukristo na uyahudi.Wakati sie wenye dini hizi tukipambana kwa doctrines,wapo watu ambao wao ndani ya mioyo yao hawapendi dini hizi zote.Naamini ni kutokana na historia ya dini hizi huko nyuma kutumika kama tool ya kumkomboa mwanadamu toka kwenye mikono ya watawala waovu na hata kuangusha tawala kubwa sana duniani ndio maana hivi leo dini hizi zimewekewa "jicho" ndani yake na nje pia,kwa kudhibiti leadership system yake na hata ikibidi doctrines na tafsiri zake ili ziendane na matakwa ya kitumwa ya wakuu wa dunia hii ambao hujitukuza zaidi ya Mwenyezi Mungu na hapa ndipo ugomvi wetu wanadini na hawa watu unapoanzia.Hivyo kwa mwanadini yeyote kati ya hizi tatu,atakuwa alerted na matatizo ya mojawapo ya dini hizi kwa sababu ya huyu common enemy tuliye naye.Ipo silaha moja kubwa ya kupambana na kashfa na kusingiziwa.Silaha hii ni "kuwajibika kujisafisha" kwa kukaa kwenye kile unachoamini na kukitekeleza kwa uwazi ili watu waone uhalisia wako tofauti na vile unavyozungumzwa.Katika biblia takatifu,kitabu cha imani yangu, kuna fungu linasema hivi,"Having your behaviour seemly among the gentiles,that wherein they speak against you as evil-doers,they may by your good works,which they behold,glorify God in the day of visitation."(1peter 2:12).Katika biblia ya kiswahili inasema hapo,"Muwe na mwenendo mzuri kati ya mataifa,ili,iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya,wayatazamapo matendo yenu mazuri,wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa."Je,katika uislam lipo suala kama hili la muumini kuwajibika kwa maneno na matendo kuonyesha ukweli na uhalisia wa dini yake ili jamii inayozunguka hata kwa wale wasio waislam,wafanye right judgment na kujengewa mtazamo sahihi juu ya uislam?kama jibu ni ndio,swali langu kuu linakuja kwako mzee wangu,nyinyi kama waislam,mnalichukuliaje tatizo la ugaidi na mnafanya juhudi gani kujisafisha na kuutenganisha uislam na shutuma hizi ambazo ulimwengu unaaminishwa hasa tukizingatia kuwa wapo watu wanaojiita waislam na wanatumia jina la uislam kufanya ugaidi(na watu huona damu ya ndugu zao ikimwagika kwa jina la uislam) situation ambayo inaleta legitimacy ya watu kuuhusisha uislam na ugaidi?na katika hili mzee wangu ukumbuke kuwa ni rahisi mbaya wako kutafuta "wajinga" ndani ya nyumba yako ili akumalize na kusema nyumba ile wote wajinga,unafanyaje hapo mzee wangu?kwa ujumla nauliza waislam mkiwa kama watu wenye responsibility ya kwanza kuilinda,kuitetea na kuitangaza dini yenu,mnafanya juhudi gani kuutenganisha uislam na huu "uzushi" wa ugaidi?