Kweli tunapiga vita ugaidi au ni vita dhidi ya uislam?

Kweli tunapiga vita ugaidi au ni vita dhidi ya uislam?

Status
Not open for further replies.
Dini zote zinazohubiri kwamba kuna moto baada ya kufa zinahubiri ugaidi.

Kuna hii ya wavaa suti inaruhusu kuuza na kununua binadamu mwenzio kama nyanya kwenye gulio (utumwa)
EPHESIANS 6:5 Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na tetemeko; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo.
 
Lazima mpigwe tena bado,eti wakristo makafiri hao ni watakatifu wa mungu,peleken ugaidi wenu huko Tanzania ni nchi ya aman mnataka kuiharibu kwa kusingizia et mnaonewa...

unafkiria na kujidanganya ww hutakufa?? endelea kuninginiza msalaba shingoni
 
Mzee Mohammed Said na waislam wote nawapeni pole.Pole yangu naitoa iwapo tu tukio hilo ni la kweli lakini hata kama si la kweli bado nitaendelea kuwapa pole waislam kwa kuubeba huu mzigo wa "ugaidi" iwe wanataka au hawataki.Hii ni perception inajengwa duniani kote na watu waislam na wasio waislam kutokana na matendo ya watu fulani wanaojiita waislam na watu fulani wanaojiita anti terrorist experts(U.S n.k).Sijafahamu kama nyinyi waislam mnaujua ukubwa wa tatizo hili lakini mie naliona kubwa sana.Unapogusia jambo linalohusu mamilioni ya watu duniani si jambo dogo hilo na hatupaswi kuliongea kwa maskhara kama wafanyavyo baadhi ya watu hapa.Huwa nakuwa mwangalifu na mambo ya uislam kwa kuwa najua katika kizazi chetu hiki,hata kama ni kwa lazima bila kupenda,kuna uhusiano wa karibu kati ya uislam,ukristo na uyahudi.Wakati sie wenye dini hizi tukipambana kwa doctrines,wapo watu ambao wao ndani ya mioyo yao hawapendi dini hizi zote.Naamini ni kutokana na historia ya dini hizi huko nyuma kutumika kama tool ya kumkomboa mwanadamu toka kwenye mikono ya watawala waovu na hata kuangusha tawala kubwa sana duniani ndio maana hivi leo dini hizi zimewekewa "jicho" ndani yake na nje pia,kwa kudhibiti leadership system yake na hata ikibidi doctrines na tafsiri zake ili ziendane na matakwa ya kitumwa ya wakuu wa dunia hii ambao hujitukuza zaidi ya Mwenyezi Mungu na hapa ndipo ugomvi wetu wanadini na hawa watu unapoanzia.Hivyo kwa mwanadini yeyote kati ya hizi tatu,atakuwa alerted na matatizo ya mojawapo ya dini hizi kwa sababu ya huyu common enemy tuliye naye.Ipo silaha moja kubwa ya kupambana na kashfa na kusingiziwa.Silaha hii ni "kuwajibika kujisafisha" kwa kukaa kwenye kile unachoamini na kukitekeleza kwa uwazi ili watu waone uhalisia wako tofauti na vile unavyozungumzwa.Katika biblia takatifu,kitabu cha imani yangu, kuna fungu linasema hivi,"Having your behaviour seemly among the gentiles,that wherein they speak against you as evil-doers,they may by your good works,which they behold,glorify God in the day of visitation."(1peter 2:12).Katika biblia ya kiswahili inasema hapo,"Muwe na mwenendo mzuri kati ya mataifa,ili,iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya,wayatazamapo matendo yenu mazuri,wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa."Je,katika uislam lipo suala kama hili la muumini kuwajibika kwa maneno na matendo kuonyesha ukweli na uhalisia wa dini yake ili jamii inayozunguka hata kwa wale wasio waislam,wafanye right judgment na kujengewa mtazamo sahihi juu ya uislam?kama jibu ni ndio,swali langu kuu linakuja kwako mzee wangu,nyinyi kama waislam,mnalichukuliaje tatizo la ugaidi na mnafanya juhudi gani kujisafisha na kuutenganisha uislam na shutuma hizi ambazo ulimwengu unaaminishwa hasa tukizingatia kuwa wapo watu wanaojiita waislam na wanatumia jina la uislam kufanya ugaidi(na watu huona damu ya ndugu zao ikimwagika kwa jina la uislam) situation ambayo inaleta legitimacy ya watu kuuhusisha uislam na ugaidi?na katika hili mzee wangu ukumbuke kuwa ni rahisi mbaya wako kutafuta "wajinga" ndani ya nyumba yako ili akumalize na kusema nyumba ile wote wajinga,unafanyaje hapo mzee wangu?kwa ujumla nauliza waislam mkiwa kama watu wenye responsibility ya kwanza kuilinda,kuitetea na kuitangaza dini yenu,mnafanya juhudi gani kuutenganisha uislam na huu "uzushi" wa ugaidi?

Mkuu Umetoa mchango mzuri sana juu ya hii Dhana ya UGAIDI na binafsi Kwa matukio ya Humu nchini mwangu nasita kidogo kuyajadili Kama ugaidi maana yanachanganya sana! Lakini ile Dhana ya Ugaidi iliyosukumwa na America Hiyo ninaweza nikaichangia. Na niseme Ivi kuna mambo mengi yamejificha ndani ya hii Dhana ya UGAIDI inaitaji hekima na maarifa kuyatambua! Na kubwa Zaidi ni UASI dhidi ya Watu Wa Mungu Au dhidi ya Ibada ya kweli! Jinsi tutakavyoendelea Kuishi hapa Duniani yatatokea mengi ndipo ule mwisho ufike!

Kuna kitabu kinaitwa Islam and Terrorism Hichi kitabu kinajaribu kuuelezea uislam Yani kinautoa ktk hii Dhana ya ugaidi! Kwa watakaopenda kujua wanaweza kukitafu!
 
Mwenye Nguvu mpishe.Huoni hata Tanzania wenye Pesa wanavyopeta?

Nguvu za Makafiri haishindi nguvu za Allah ndo mana wamejaribu kuchoma moto quran walisahau kama Quran imo ndani ya vifua vya waislamu., uislam upo ndani ya damu za waislam na utaendelea kuwepo Mungu ameahidi kuulinda.,
 
Hii ni Vita Dhidi ya UGAIDI na MAGAIDI.Kama unaona ni Vita dhidi ya Uislamu Jaribu kulianzisha uone Moto wake.Mwenzio Shekh Ossama alitamani ardhi ipasuke.

Kijana usiombee tukafika huko, hapa inatolewa indhari kwa wenye macho wajionee, wenye masikio wasikie. Usifikiri hapa panafanyika mzaha. Ujuwe ni damu ya ndugu zetu iliyomwagwa na ujuwe ni ndugu zetu waliobambikiwa kesi.

Hivi huko vijijini kuna ugaidi upi? tunaomba mtufahamishe. Au neno ugaidi ni kisingizio cha kutuulia ndugu zetu, kutuchomea Qur'an yetu na kutuchomea misikiti yetu? kwa lipi haswa tulilowakosea?
 
Mafinyofinyo,
Kweli magaidi lazima wapigwe.

Lakini hao wana vijiji wa Madina na vijiji vya jirani hawakuwa magaidi.
Kama upo ushahidi wa ugaidi na uletwe uonekane.

Waliouliwa wamezikwa kimya kimya na waliobaki wamefunguliwa mashtaka
mahakama ya Handeni.

Katika mashtaka yao hakuna kosa la ugaidi.
Sheikh Chambuso anajulikana kama mwalimu wa madras Tanga.

Yeye shitaka lake ni kama nilivyoeleza awali.
Sheikh Chambuso kafunguliwa kesi ya ''kushawishi mauaji.''

Dhulma kama hizi zinasikitisha sana na hazitajenga taifa letu bali
kuleta chuki.

Kwa ajili hii tunapochangia mjadala kama huu ni muhimu sana kuwa
makini.

Gaidi anaweza kuwa wa dini yoyote. Tatizo ni kuwa akitokea gaidi ambaye ni muislam, wengi wenu ama mnakataa na kudai kuwa huyo muislam hahusiki, au mnahalalisha aliyoyafanya kwa kudai anapigania haki.fulani na mara nyingi mtampa "a hero status" . Mara moja moja, ushahidi ukiwa mkubwa, mnajaribu kum-dissociate huyo mtu na uislam.

Labda nikuulize Mohamed Said, kuna makundi kama ya alshabab, boko haram, abusayyef, alqaeda, na jamaat islamiya. Ushahidi upo mwingi tu wa makundi haya kijihusisha na ugaidi. Lakini je kuna kundi ambalo wewe binafsi unakubali kuwa ni la kigaidi?
 
Last edited by a moderator:
Nani mbunge wa sehemu hiyo?,kwanini watu wameuawa halafu issue imeisha kimyakimya kama kwamba wameuawa kondoo?
 
Gaidi anaweza kuwa wa dini yoyote. Tatizo ni kuwa akitokea gaidi ambaye ni muislam, wengi wenu ama mnakataa na kudai kuwa huyo muislam hahusiki, au mnahalalisha aliyoyafanya kwa kudai anapigania haki.fulani na mara nyingi mtampa "a hero status" . Mara moja moja, ushahidi ukiwa mkubwa, mnajaribu kum-dissociate huyo mtu na uislam.

Labda nikuulize Mohamed Said, kuna makundi kama ya alshabab, boko haram, abusayyef, alqaeda, na jamaat islamiya. Ushahidi upo mwingi tu wa makundi haya kijihusisha na ugaidi. Lakini je kuna kundi ambalo wewe binafsi unakubali kuwa ni la kigaidi?

Mkuu kabla hajajibu ndugu Mohamed Said Hilo Swali ningependa tukaweza kufahamu nini harakati za hayo makundi Je wanatetea nini? Au wanafanya vurugu tu?

Nimeona tujue harakati zao kwanza ili huu mjadala uwe mpana Zaidi!
 
Last edited by a moderator:
Brother Mohamed haya hufanywa makusudi na ndio sera rasmi kabisa ya jeshi hata kata kama rais na makamo ni waislam .huwa hawana nguvu dhidi ya mfumo huu wa dhulma na akienda kinyume na matakwa ya mfumo atahujumiwa hadi ashindwe kutawala na ndio tunayo yaona leo kwa serikali ya kikwete.
Kule mtwara walifanya haya haya na ushenzi wa hali ya juu watu walihama makazi yao na ili kuwabamiza wakapachikwa ugaidi na hii ndio mbinu yao kuwaua na kuhujumu uislam ma mali zao.
Walifanya pemba ambapo watu zaidii ua 40 waliuliea watu kuwa raped wengine kwa mamia kuwa vilema ma wakimbizi
Huu mtindo wa collective punishment hufanywa maeneo ya waislam tu. Huwezi kuona arusha moshi au iringa hata wakiua askari 100 basi suala hilo lita chukuliwa la kawaida
Kuna operation ttokomeza majangili hii ingeekuea imefanuika lindi au mafia au mtwara au tanga kusengekua na tume
Huu ni ukweli na ndio hali hali halisi ya nchi yetu
Lakini nini cha kufanya ? Jee tuendelee kuwa wanyonge maisha katika nchii hii?
Jawabu hapana hatuwezi kuachia hii ikaenndelea
Mambo mawili yanaweza kuondoa haya
Kwanza kabisa kwa vile bakwata haituanganishi imekua ikitumiwa lazima ifanyiwe mabadiliko ..jee ni rahisi kuivaa bakwata? Sio rahisi lakini hii ni taasisi ya waislam tufanye nia kuwaondosha viongozi waliopo hapa nazungumzia one million muslim march wapewe muda wa miezi 6 waitishe mkutano na viongozi wa taasisi zote za kislamu ili katiba ibadilishwe na uitishwe uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya watakao waongoza waislam.
Wakikataa kuitisha mkutano huo wapewe ultimatum juu ya kuwandoa kwa nguvu ndani ya miezi 6 na tarehe iwekwe wazi waislam watayarishwe kwa maandamano makubwa sana ya kihistoria kuwaondoa bakwata
Serikali waarifiwe kuwa haya hayawahusu ni masuala ya waislam na taasisi yao walinde amani basi
Kitu kimoja kwa uhakika Kikwete haridhishwi na bakwata lakini hana cha kufanya
La pili ni kura... kura za waislam zisitumike kuwachagua viongozi au vyama vyenye kuwaonea waislam .kabisa iazishwe kampeni ya nguvu.wenzetu wakiambia kwenye misa zao wanafata maelekezo kwa nimi sie tusi fanye kama wao
Mpaka tutapoingiza masheikh ndani bunge kama mapadri na wachungaji waliomo hatuwezi kupata haki zetu lazima vijana wahamasishwe kugombea nafasi za ubunge na masheikh pia
Hakika inawezekana
 
Magaidi lazima yapigwe kwa nguvu zote! Haijalishi ni waislamu au watu wa dini nyingine. Wapigwe tu tumechoka. Nasema wapigwee tu..!
Ndani ya moyo wako humanishi ugaidi wala humaanishi wapigwe magaidi bali wapigwe waislam lakini yalifanyika nigeria sieralone cameroon afrika ya kati yalifanyika mali na sehemu nyengine haya ya kuwadhulumu waislam..na hakika waislam ni wastahamilvu sana ni wavumilivu sana kwani wanambiwa Innalahha maasabiriin...basi sisi tunavumilia lakini pia tunafundishwa tusidhulumu nafsi wala mali ya mtu. Lakni pia tunafundishwa tusikubali kudhulumiwa.hivo tunapolalamika musione tu wajinga.
mnafanya collective punishment ya vijiji vya waislam kwa kosa la mtu mmoja mnachoma misikiti mnachoma Quraan mnakamata masheikh na kuwasingizia ugaidi hakika waislam ni wenye kuwa na subra .lakini mwisho wa subra ndio unayo yaona nchi nyengine yote asili yake ni dhulma na wakiambiwa mnatudhulumu basi husingizia ugaidi
Tusifike huko hakuna faida yoyote
 
Haitwi ossama. Bali ni SHEIKH OSAMA MWANA WA LADEN!
Ametingisha mataifa zaidi ya 50 ya makafiri!
Kawarudisha makafiri kwenye body bags kwa maalfu!
Ni one man army! Wamepiga kila kona ya afghanistan na Pakistan kwa zaidi ya miaka zaidi ya 10 na ziada lkn wapi!
Kwa hio unapotaka jina lake MPE HESHIMA yake!

Dude, what are your view on preventing terrorism?
 
Hii ni chuki juu ya uislamu na waislamu kwa ujumla jamani tujihadhari sana tusije tukafika pabaya
 
Kuonewa, kuonewa, kuonewa, kuonewa. Kuhujumiwa, kuhujumiwa, kuhujumiwa....na nani!??? Na makafiri, sijui hao makafiri ndio sisi wakristo--- sina hakika maana nasikia tena mfumo kristu, mke mmoja, Ndoa za jinsia moja, madawa ya kulevya, nk...vyoote wakristo, Ooo mara Vatican...
Jamani jamani.... ADUI YETU NI MMOJA TU- SHETANI.
KUNA MPANGO MAALUM WA HAWA WATAWALA WA DUNIA WA KUZUIA KUONGEZEKA NA KUPUNGUZA NGUVU KWA HIZI DINI KUBWA, UISLAM NA UKRISTU. NA NJIA RAHISI KWAO NI KUTUGOMBANISHA TUKIDHOOFISHANA WAO WANAFANYA FINISHING TUUU- WANAPIGA NDEGE WAWILI KIRAHISI KABISA.
Wana jeshi lao...wengine wamo miongoni mwetu, tunasali nao na wengine mnaswali nao... Tukubali tuu kwamba hii ni vita ngumu.
Tuweni watulivu wakati tunapambana nao.
 
Tatizo ni dini hii ilianza kwa ushauri wa mganga wa kienyeji, kitabu cha maisha ya muhamad uk.7. tatizo lilianzia hapa. unategemea nini matokeo ya wafuasi wake kama si kuwa na hakili za kiganga ganga?. nauliza tu.
 
Mkuu kabla hajajibu ndugu Mohamed Said Hilo Swali ningependa tukaweza kufahamu nini harakati za hayo makundi Je wanatetea nini? Au wanafanya vurugu tu?

Nimeona tujue harakati zao kwanza ili huu mjadala uwe mpana Zaidi!

Ntuzu,
Umepanua uwanja wa majadiliano.

Hapa mimi nimeleta taarifa za watu ambao hata gazeti la siku hawasomi.
Watu wa vijijini ambao hawajamdhuru mti yoyote wala hawajui ugaidi ni kitu gani.

Nina uwezo wa kjadili hayo na kwa kweli nimepata kutoa mada ya ugaidi katika
Afrika Mashariki Chuo Kikuu cha Ibadan.

Lakini hapa si mahala pake.
 
Nani mbunge wa sehemu hiyo?,kwanini watu wameuawa halafu issue imeisha kimyakimya kama kwamba wameuawa kondoo?

Elungata,
Mbunge ni Beatrice Shelukindo.

In Sha Allah tunategemea iko siku atazunguza si yeye tu bali wote
waliohusika na dhulma hii.
 
Elungata,
Mbunge ni Beatrice Shelukindo.

In Sha Allah tunategemea iko siku atazunguza si yeye tu bali wote
waliohusika na dhulma hii.
Mbunge mkristo hatowasaidia.na hili tayizo jengine la waislam bado tunaendelea kuwachagua hawa !! Lazima tubadilike iwe fundisho sehemu za waislam kuwa na mbunge mkristo hatawasaidia hata siku moja
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom