jogoolashamba
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 348
- 71
:lock1:Miezi michache iliyopita vyombo vya habari vilisheheni taarifa ya magaidi waliokuwa katika vijiji vya Handeni.
Taarifa zilifika Tanga kuwa kulikuwa na magaidi wanaishi katika mahandaki na operesheni maalum ilikuwa ikifanyika kuwateketeza.
Propaganda ikaenezwa kuwa walikuwa hawaitambui serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Habari zilivuja Tanga mjini na vitongiji vyake kuwa kuna vijiji vimeteketezwa.
Kwa hakika kuna watu waliletwa Hospitali ya Bombo wakiwa na majeraha ya risasi.
Kwa watu waliofika Hospitali ya Bombo kwa kweli waliwaona vijana waliokuwa wamefungwa pingu wakiwa katika vitanda vyao huku wakilindwa na askari.
Taarifa zikafika vilevile kuwa kuna watoto wadogo wamefikishwa Tanga baada ya kukutwa porini.
Watoto hawa walikuwa wamehifadhiwa katika moja ya shule za hapo mjini.
Katika hali kama hiyo vilevile zikafika taarifa tofauti kwa Waislam wa Tanga kuwa hao walioletwa Hosptali ya Bombo na watoto waliookotwa porini ni Waislam wa vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande walioshambuliwa na askari pasi na sababu.
Juhudi za Umoja wa Taasisi za Kiislam Tanga (SHITA) chini ya Mayor Omari Guledi na Katibu wake Ahmed Mustafa kukutana na Mkuu wa Mkoa Chiku Galawa kupata ukweli zikagonga mwamba.
Hali ikawa tete baada ya Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso mmoja katika masheikh vijana mjini Tanga kukamatwa na kuwekwa rumande kisha kuhamishwa Handeni ambako alifunguliwa kesi ya ''kushawishi mauaji.''
Ikavuma kuwa patakuwa na maandamano kushinikiza kuachiwa kwa Sheikh Chanmbuso.
Askari wa FFU walizingira misikiti kadhaa Ijumaa hiyo lakini hapakuwa na maadamano yoyote.
Alipopata dhamana na kuachiwa Sheikh Chambuso alikuja Tanga na habari za kutisha kuhusu dhulma iliyopita katika vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande.
Habari hizi alielezwa na mahabusi wendake katika hivyo vijiji vilivyoshambuliwa.
Sheikh Chambuso katika hotba aliyotoa katika moja ya misikiti maarufu Tanga aliwafahamisha Waislam kuhusu misikiti iliyovujwa na kuchomwa moto, Qur'an zillizochoiwa moto na nyumba za Waislam zilizoteketezwa kwa kisingizo cha ugaidi.
Wananchi jioneeni wenyewe yote hayo katika hizi picha.
PS: Weka cursor kwenye picha click utapata na maelezo ya picha.
Waislamu wa Tz wana matatizo yao na wanaishi nayo huko huko wanakokutana na matatizo yao mengine. Matatizo yao ni siri kubwa mpaka wanapohisi wamejulikana au anayewajua anataka kuwaumbua. Ukikumbuka maandamano ya Waislamu wa Chamazi eti kuna mtoto wa Mkristo amekojolea Koran utaelewa nasema nini. Tukio kama hilo lilikuwa la kughushi ili kutishia umma usijue hofu yao halisi ya mtu mmoja wanayemwogopa maisha yao kwa miaka ishirini na zaidi sasa. Wakachoma makanisa ili tu kupoteza lengo na kuwavuruga wasiojua ili waendelee kudhani Waislamu wana hoja ya dini yao, kumbe ni maovu yao yamekithiri hawataki yakajulikana.
Siri zao ni nyingi mno mpaka huwezi kuwaelewa mpaka ujue mikakati yao wanayopanga usiku na mchana miongoni mwao. Ukitaka kujua siri zao soma matusi na majigambo wanayoandika kwenye vitako na nyuma ya magari yao ya kubebea mizigo na abiria. Wao hapo wana namna ya magazeti na radio za siri muhimu sana za kuwasiliana miongoni mwao ili walioko Tanga wakisoma wajue walioko Mkuranga na Lindi na Mtwara wamefikia hatua zipi katika malengo yao ya pamoja.
Hivyo ukikuta wanamlazimisha Chiku Ghalawa aseme nao ujue wanatafuta mahali pa kuficha visiri vyao ili mgongo wa Ofisi ndiyo ujulikane kuhusu wanalotaka kuficha. Chiku Ghalawa akikataa wanajitangaza wanaonewa na kutangaza jihadi. Wote mmeshuhudia kelele za Mahakama ya Kadhi. Wanaambiwa Serikali haina utaratibu wa kuingia misikitini kwenda kuanzisha taratibu na miongozo ya kidini, nendeni mkasome Koran yenu mfuate yanayoagizwa humo, kama na Mahakama ya Kadhi sawia haya, hakuna atakayekuja kuwakataza. Lakini bado mmeshuhudia makelele yalivyokwenda mpaka Waziri Mkuu (Mkristo masikini Mizengo PETER Pinda) akalazimishwa kukutana na Waislamu. Eti tu wajulikane wao wamekutana na Serikali kwa NGUVU.
Mhhhh! Nisiseme mengi mno mtaniona nawachukia hawa jamaa lakini matatizo yao huwa wanakuwa nayo huko huko, ukiwaona wanakuja hadharani ujue wanatafuta wenye shida tu ya kuyaona katika sura ya uongo wanaokuwa wamepanga huko huko.