Umesema kweli mkuu.
Kinachosumbua waislam ni INFERIORITY Complex, baasi. It is pathetic kwamba mtu anayejiita msomi Mohamed Said naye amejoin- hiyo bandwagon. Maandiko yote ya Said ni KULALAMIKA tu, kuwaona waislam ni wanyonge, dhaifu, etc. Tujiulize: lengo la kufanya hivi ni nini? Lengo ni kutaka waislam sasa wapewe upendeleo fulani au favours maalum na serikali (outside of merit!!). Pamoja na 'usomi' wake Said hajui kuwa suala la waislam kupewa upendeleo maalum haliwezekani na halijawahi kufanyika popote duniani.
Hawa wanaolalamika yaliyotokea Tanga, hawausemi ukweli kuwa hawa waislamu waligomea kulipa ushuru, wakampiga mpaka kumuua mgambo aliyekuwa akisimamia sheria, tena muislam mwenzao. Sasa wanasakwa na kukamatwa, wanadai ni kwa sababu ya uislam wao; this is stupidity of the highest order...Ndio maana hata RC Chiku hakutaka hata kusikiliza upuuzi wao.
The moment waislam wataachana na INFERIORITY COMPLEX ya akina Mohamed Said na kujikita katika solution based actions (kusomesha watoto wao, kufanya personal enterprise, etc) is the moment we will see them rising up.
Hebu angalia, wapo waislam wengi wasio na mentality ya M.Said
, wanajiamini, wanajua wao wenyewe ndio wako Responsible na maisha yao, hawamlaumu mtu au historia, etc mbona maisha yao ni mazuri kabisa? Ina maana hao MFUMO KRISTO haukuwaona?
Kwa mentality na approach hii waislamu wataishia kupata virungu na kuozea magerezani; like Ponda & co) bila kufanikisha ajenga yoyote au lolote wanalodai. Halafu bado wanasem ".. inshallah uislam utatawala dunia..!!"..labda Venus..
Kwelitupu,
Unanisoma kinyumenyume hata siku moja sijapata kuwaeleza Waislam
kuwa ni wanyoge.
Wala historia ya Waislam Tanzania kuanzia Vita vya Maji Majihadi kuja
kupigania uhuru nimewaeleza Waislam katika historia yao ya mapambano.
Vitabu vyangu na papers zangu zipo kote zitafute usome.
Historia kama hii ''inferiority complex'' itaingia wapi?
We unaniona nimeingia hapa uwanjani kwa jina langu kamili bila ya kujificha.
Hii ni dalili ya unyonge au uoga?
Mimi silalamiki.
Kulalamika neno hilo linatokana na ulalamishi.
Mimi silalamiki mimi nasomesha historia ya wazee wangu iliyofichwa kwa
zaidi ya nusu karne ikapachikwa na kuwapa watu heshima zisizozao.
Mimi silalamiki mimi naweka bayana dhulma na uchafu mwingine
wanaotendewa Waislam wa Tanzania.
Mimi najiamini sana na nimesimama kwingi duniani katika majukwa
ya kigeni nikiwa peke yangu na nikazungumza yote niliyotaka na
kujibu maswali yao.
Hii si dalili ya mtu asiyejiamini.
Una shaka kuhusu utukufu wa Uislam?
Angalia mfano wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nani waliongoza mapambano yale?
Nani waliasisi TANU nani walitoa fedha za kupambana na Muingereza?
Isome historia hii utapata jibu.
Angalia hii picha hapa chini.
Chiku Galawa hakutaka kusikiliza upuuzi...
Hakutaka kusikiza upuuzu upi?
Unajua kuwa tatizo la ushuru lilitokea Kilindi alipouliwa mgambo?
Je unajua kuwa hao watoza ushuru walikwenda kudai ushuru nyumbani
kwa mtu na si sokoni?
Je unajua kuwa Madina hawakuhusika na yaliyotokea Kilindi?
Je unajua kuwa Sheikh Hamisi Msuri kauliwa mbele ya msikiti Madina
na hakuwa na habari yoyote kuhusu ushuru wa hiliki?
Je unajua kuwa Lwande nako msikiti ulivunjwa na matofali yake yakapelekwa
kujenga zahanati ya serikali?
Je unajua kuwa vibarua walikataa kuchukua kazi ya kuhamisha matofali ya
msikiti kwenda kwenye kiwanja cha serikali kujenga zahanati?
Unajua kuwa propaganda iliyokuwa inavumishwa ni kuwa ati Waislam wa
huko walikuwa wanaishi katika mahandaki?
Nani mpuuzi?
Msemakweli kipi kimekufanya utumie neno hili ''upuuzi?''
Sisi wapuuzi?
Anevamia na kuchoma na misikiti na kuvunja nyumba au yule anetaka haki
isimame?
Mbona kama kulikuwa na magaidi kazi ilikuwa ni ndogo tu ya kuwakamata?
Nani mpuuzi?
Yule anaepeleka askari kuua na kuchoma misikiti na nyumba na kuiba mali zao?
Angalia picha ya msikiti mabao haupo msingi umechimbwa.
Msikiti na ushuru wa hiliki kuna uhusiano upi?
Nani mpuuzi?
Nani mpuuzi?
Nani mpuuzi kuiko yule aneamini ati Lwande kulikuwa na mahandaki ya Al Shabab?
Hii inaitwa cock and bull story.
Chiku Galawa...
Msemakweli ahsante kwa kuniletea jina hili.
Kajiingiza vizuuuri katika historia.
Believe this and you will believe everything.
Nani mpuuzi?
Yule anetoa amri kuwa yeyete aliyevaa kanzu na kuonyesha athari za
Uislam ashushwe kwenye basi na airuhusiwe kuingia Handeni...
Unajua kuwa hizi ni mbinu wakitumia Manazi wa Hitler dhidi ya Wayahudi
wakati wa Vita Kuu ya Pili?
Haya leo wanafanyiwa Waislam tena wa vijijini...
Kisha unawaita wapuuzi.
Chiku Galawa...
Ziko picha nyingi In Sha Allah tutaziweka hapa.
Msemakweli huenda ulikuwa hujui.
Kanzu za Waislam ndizo zilizopigania uhuru wa Tangnayika na ushahidi ni
hiyo picha.
Wangefufuka hawa wazee wetu wakaiona nchi walioikomboa kuwa
inachukia kanzu wangesema, ''Au tumefufuka nchi nyingine?''