Mimi nitashea mawazo yangu japo sio sheria. Mtizamo wangu uko hivi, zamani miaka ya 2005 kurudi nyuma Ulaya kulikua na vipaji vingi sana vya soka kiasi kwamba ilifika hatua watu kama kina Giovane Elber wanakosa namba timu ya taifa ya Brazil ila pale Allianz Arena anakiwasha kweli kweli. Sasa ilikua ngumu kwa wachezaji wengi wa kiafrica kupenya na kucheza Ulaya, so wachezaji wengi wazuri walioshindwa kupenya Ulaya walikua wanabaki Africa kiasi ambacho Ligi ya Mabingwa (zamani kombe la washindi barani Africa) na kombe la shirikisho (kombe la caf) ilikua ngumu sana maana wababe walikua wengi kweli kweli. West Africa tulikua na Asec Mimosa, Stella Abidjan, Canon Younde, Cotton Sport, Hearts of Oak, Enugu Rangers, North Africa unakutana na Raja& Wydad, Esperance de Tunis, Etoile du Sahel, USMA, Zamalek, Al Ahly. South Africa hao Orlando Pirates na Kaizer Chiefs walikua hawagusiki. Kwahiyo ilikua sio ajabu timu zetu kutolewa tena kwa vipigo vikubwa vya aibu. Kwa sasa zama zimebadilika mno, Ulaya inazalisha vipaji vya soka vya kawaida mno kiasi ambacho ni rahisi sana kwa wachezaji wengi wa kiafrica kupata nafasi huko. So kinachotokea wachezaji wengi wazuri wanakimbilia Ulaya kucheza soka la kulipwa huku Africa wanabaki wa kawaida ambao viwango vyao wala havipishani sana kiasi icho. Mchezaji anaecheza Botswana ama Zambia hapishani sana na anaecheza Morocco au Tunisia ama South Africa ama Egypt tofauti ni facilities tu za timu na mishahara lakini viwango wanakaribiana sana. Zamani ni ngumu kwa vilabu vyetu kusajili wachezaji wanaojeza timu za taifa lakini leo hii inawezekana kabsa tena wapo wengi tu wa kutosha. Zamani ukikutana na hawa warabu basi ujue wanakupiga nje ndani tena kipigo kikubwa cha aibu. Leo hii matokeo ni probability hakuna uhakika wa 100% wa mwarabu kukupiga home&away.
So tusishangae sana Wydad kupigwa mechi mbili consecutively na timu zinazoonekana za kawaida ukweli ni kwamba viwango vya wachezaji wa hizi timu zote vinakaribiana sana tofauti ni mishahara na facilities tu. Naomba kuwasilisha