Kweli ushamba mzigo

Ila huu ni uongo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aaaaah! Nipo A level na rafiki yangu wakati wa break tukawahi Moshi mjini posta kuchukua pesa tulitumiwa kwa EMS.

Baada ya hapo tukaingia mgahawa wa hadhi kidogo karibu na ile roundabout.
Chai ilivyoletwa kulikua na vipande vya limau, ile unakamulia kwa chai. Mie nilivyomaliza kugonga sambusa na chai baadae nikashushia na tule tulimau ila nilikua nalamba na kuvyonza kama chungwa. Nilijua ni tunda kupata mlo kamili.
 
Na JF uliijuaje sasa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilibandika jagi la umeme la plastic kwenye jjiko la umeme,, nikawasha.
Nilivoskia jagi la umeme nikajua linapikiwa kwenye jjiko la umeme, daa nilishangaa linayeyuka halafu nilikua kwa anko wangu, hakuwepo. Mke wake alinisema sana, niliona aibu, nilikua nimemaliza form four, dah
 
[emoji23][emoji23]yako Kali rafiki
 
Tena ushamba wako ulitakiwa kutolewa kwa kukulamba makofi kama matatu hivi
 
[emoji23][emoji23][emoji23] ulivyosema pesa umenikumbusha mimi siku ya kwanza kutumia ATM nilitumwa kutoa 20,000 kile kiwewe nikatoa 200,000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka sikumbuki kipindi natoka zangu tanga nilikuwa napita pale kibaha picha ya ndege baada kuona picha ya sanamu ya ndege nikajua ndege imenasa abiria walicheka Mie nikawa sielewi namuonyesha tu siku hiyo nilikuwa kaka ila Kaka aliona aibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilienda bonge la party yenye hadhi kule O'bay vikaletwa vinywaji nikamute kwanza. Nikaona wanaomba kuwekewa ice nami nikaomba, wakaweka Amarula fulani ina radha ya maziwa nami nikachukua hiyo kumbe zinapendwa na wamama. Nilikuwa na kilaza mwenzangu yeye akaagiza Sprite nikamcheka yani watu wanakunywa juice za South Africa, whisky na vinywaji vya bei yeye kakalili chupa ya buku. Zikaletwa sambusa na vidude vingine sivijui. Watu wanagusagusa tu, sisi tukasema lazima tule mpaka kieleweke. Tukakaa kidogo wakachukua vyombo wakaleta matunda, hatukuyafagilia hata. Kumbe kuna msosi: wakaleta biliani, kuku, samaki watamu balaa na mazaga mengine. Haki siku ile kuku alizidiwa utamu mbali mno na kila kitu na ubaya tulishiba mapema na introduction. Sasa kuna vitambaa walitanguliza, step zote tulikuwa tunaangalizia lakini msosi ukahamisha akili tukachukua vitambaa tukaweka chini ya sahani. Kila mtu ashaanza kula ndo tunagundua wote vitambaa wamefunga shingoni kuzuia chakula kikidondoka kisichafue nguo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…