Mimi nilienda bonge la party yenye hadhi kule O'bay vikaletwa vinywaji nikamute kwanza. Nikaona wanaomba kuwekewa ice nami nikaomba, wakaweka Amarula fulani ina radha ya maziwa nami nikachukua hiyo kumbe zinapendwa na wamama. Nilikuwa na kilaza mwenzangu yeye akaagiza Sprite nikamcheka yani watu wanakunywa juice za South Africa, whisky na vinywaji vya bei yeye kakalili chupa ya buku. Zikaletwa sambusa na vidude vingine sivijui. Watu wanagusagusa tu, sisi tukasema lazima tule mpaka kieleweke. Tukakaa kidogo wakachukua vyombo wakaleta matunda, hatukuyafagilia hata. Kumbe kuna msosi: wakaleta biliani, kuku, samaki watamu balaa na mazaga mengine. Haki siku ile kuku alizidiwa utamu mbali mno na kila kitu na ubaya tulishiba mapema na introduction. Sasa kuna vitambaa walitanguliza, step zote tulikuwa tunaangalizia lakini msosi ukahamisha akili tukachukua vitambaa tukaweka chini ya sahani. Kila mtu ashaanza kula ndo tunagundua wote vitambaa wamefunga shingoni kuzuia chakula kikidondoka kisichafue nguo.