Kweli wanaume wengine kazi ipo ......

Haa haaa,same houc?nani kasema?
Km nimeamua kuwa peke yangu means hata yeye simtaki pia,
Watoto watenda huko kusalimia baba yao ila si kuishi pamoja tena!
Kwangu haiwezekani.

sasa why taking all those troubles kama umeshasamehe?? kwanini awe mbali nawe wakati mnahitaji sasa kuunganisha nguvu na kulea watoto wenu vyema?? hakiwepo nyumba moja nawe kutakuwa na tatizo gani?? au me sielewi maana ya kusamehe hapa??
 
ahsante madabwada. Post yako imenifanya nismile. Kwa kuongezea huyo mume anaweza akawa mume mwema sana baada ya msamaha. Probability ya yeye kurudia madudu yake ni ndogo sana.
 
Well said ndugu yangu, kunya anye kuku tu bata anachafua uwanja!
 
hapo tushaelewana wanaume wengi wana take advantage ya wanawake sana! Kisa their so compassionate kama wewe hutomsamehe ukimfumania. why shouldn't her do that on you? Na wanaume weng tuko hivyo! Maskini most of women walio too dependent ndo hukoma na unyanyasi huu..
 
ahsante madabwada. Post yako imenifanya nismile. Kwa kuongezea huyo mume anaweza akawa mume mwema sana baada ya msamaha. Probability ya yeye kurudia madudu yake ni ndogo sana.

Husninyo, maneno yako machache lakini yamemaanisha jambo kubwa sana na la msingi ... kile ambacho kiukweli hatuna katika ndoa zetu hizi, tumejaa tu ubinafsi na kujipenda sisi wenyewe zaidi! Ubinafsi ni ufisadi ulioota mizizi katika taasisi ya ndoa zetu siku hizi!
 
ahsante madabwada. Post yako imenifanya nismile. Kwa kuongezea huyo mume anaweza akawa mume mwema sana baada ya msamaha. Probability ya yeye kurudia madudu yake ni ndogo sana.

leo uko kwenye mood eti maana ndugu yangu comments zako huwa very short.. sasa naona umeamua
 
okay, mimi na wewe tumeshalitambua hilo ... then tuwe chachu ya kuwashawishi na wanaume wenzetu wabadilike (BPM, TB, TF, ODM, EMT etc mtuunge mkono bana .... lol)
 
sasa why taking all those troubles kama umeshasamehe?? kwanini awe mbali nawe wakati mnahitaji sasa kuunganisha nguvu na kulea watoto wenu vyema?? hakiwepo nyumba moja nawe kutakuwa na tatizo gani?? au me sielewi maana ya kusamehe hapa??
Wala kutakuwa hakuna haja ya kukusanya nguvu,nilishazoea maisha yangu na kuiendesha familia peke yangu,
Nitakuwa wala sihitaji ukaribu naye wa aina yoyote,
Siwezi kuishi naye nyumba moja kwani aliamua kuondoka na kuniacha na shida na watoto,
Nitakuwa nimeshamsaehe na ila sio kurudiana tena kwan hata tukirudiana siwezi kumpenda tena km mwanzo ili nisiwe mnafiki ni bora kuwa wazi ajue na asipoteze mda wake kuwa na mm.
 
kufanya kosa (at first place) sio kosa, kosa kurudia kosa! ameshwasiliana na shetani, akamkana na ndio maana amerudi, wether amerudi na hela or hapana, kwanini usimsamehe??

kifupi nitakuwa nilishasamehe toka alikokuwa, sijaona kwenye thread ya mwanzilishi kama mama alikata mbuga kwenda kumsaka huyo baba huko aliko.alimuacha aendelee na maisha yake naye mama akajipanga upya. Sasa kwa nini aje atuharibie utaratibu wetu wa maisha leo hii, surely tuliweza bila yeye na tutasonga mbele (haa haa..). Na wala sitakataza mwanangu akamsalimie huko atakakokuwa, ila kwa mimi kama mama, hapana kwa kweli, with or without money.
 
kufanya kosa (at first place) sio kosa, kosa kurudia kosa! ameshwasiliana na shetani, akamkana na ndio maana amerudi, wether amerudi na hela or hapana, kwanini usimsamehe??
Lakini inauma sana .Yaani mtu apate pesa akastaqrehe na wengine.Akiishiwa wewe ndio anakurudia,yahitaji kuwa na moyo wa plastiki.Hata nikikusamehe upendo hautakuwa kama ule wa mwanzo.
 
halafu naona wanawake wenzangu kama wengi hawatosamehe sababu ya kulipiza kisasi. Kwenye posts zao wengi wanasema kama wangekuwa ni wao huyo mwanaume angesamehe! Sijui nawaelewa vibaya au?
 
leo uko kwenye mood eti maana ndugu yangu comments zako huwa very short.. sasa naona umeamua

hahahahahaha! Siku zote huwa nipo kwenye mood nzuri kashengo ila kwenye hii topic nimeamua kuwa serious zaidi. Na usiwe chanzo cha kunifanya nianze kuchakachua thread. Lol
 
okay, mimi na wewe tumeshalitambua hilo ... then tuwe chachu ya kuwashawishi na wanaume wenzetu wabadilike (BPM, TB, TF, ODM, EMT etc mtuunge mkono bana .... lol)

BPM iko janja sana iko kimbia swali angu aisee
 
Canty, tukubali tu yakuwa kusamehe kwa wengi ni kugumu ... hapo utakuwa haujamsamehe ... thats the plain truth and lets not run circles!
Na ndio maana uwepo wake karibu yako waona kero sababu utakuwa bado unalo dukuduku moyoni ... ningekuelewa kama ungesema ungehitaji muda zaidi wa kukaa peke yako kwanza sababu u now have to cope with him (being around) na kuzishinda hisia zako za upweke na hasira, then ataratibu mngaliweza kuanza ku-entergrate pamoja through normal interactions za watoto na mambo mengineyo yanayowaunganisha pamoja ... healing/forgiveness is longtime process!!
 
Dina, ulipata wasaa upi wa kumsamehe wakati hakuwepo?? maisha bila yeye hayakuwa rahisi kama mtoa mada alivyoeleza, mke alipitia machungu mengi! kuendelea na utaratibu wako wa maisha kana kwamba yeye bado hayupo ni kwamba bado hujasamehe hapo!
 
FL1,

Mwambie huyo mama afuate mfano wa Clintons na hasa wimbo wa STAND BY YOUR MAN by Tammy Wynette.

X-Mas hii inakuja, itakuwa poa akiwa na mtu wa kumsugua mgogo wakati wanaoga, hihihiii, kwa dodoki laini ati 🙂

Last edited by a moderator:
Lakini inauma sana .Yaani mtu apate pesa akastaqrehe na wengine.Akiishiwa wewe ndio anakurudia,yahitaji kuwa na moyo wa plastiki.Hata nikikusamehe upendo hautakuwa kama ule wa mwanzo.

Ni kweli Jomse, siku hizi hatuna upendo wa kweli kabisa katika ndoa zetu, tunaamua tu kuishi pamoja sababu ya mali au kazi au uzuri wa mtu fulani unayetaka kuwa naye, na kwa tafsiri yetu hiki ndicho twakiita ndoa siku hizi ... hapana, ndoa ni zaidi ya hilo! kuwa tayari kujitoa sadaka kwa ajili ya furaha ya maisha yako na mwenzako, na moja kati ya vitu hivyo vigumu ni kusamehe makosa na mapungufu ya wenzi wetu!
 
Unajua kiukweli na kibinadam hebu angalien ingekuwa hayo kayafanya mwanamke ingekuwaje jaman?
N huo udhaifu wa miaka saba ni wa aina gani huo?
Je angekufa huko ingekuwaje?au angenikuta mataizo aliyonisababishia yameniua je angerudi wapi?
Achen bwana,ninawacwac km ulishawahi kupenda tena kwa moyo wako wote alafu ukaumizwa na ukaujua uchungu wake wakati hapo hakuna ndoa,watoto wala mimba!
Alafu hapo mlishapitia magumu mengi labda ndio mmefanikiwa alafu ndio akakimbia!
Kwahilo kwangu ni ngumu sana na hapo tutadanganyana tu hata tukirudiana kamwe sitaweza kumpenda tena,
Labda tuishi kinafiki na binafsi huwa siwezi maisha ya maigizo ni bora niishi kwa shida peke yangu na si kuigiza!
 
kutendwa sio sababu ya kutopenda tena, kwanini umulike ulipoangukia na usimulike ulipojikwaa?? bado tunarudi pale pale, hatuchagui wenzi wetu kutokana na upendo wa kweli but merely from other minor factors, uzuri, kazi nzuri, fedha, etc ... sasa hapo wakati wa misukosuko ya ndoa kwanini msiangukie pua?? hakuna miujiza hapo ... its purely a wrong selection from the scratch!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…