Kweli wanaume wengine kazi ipo ......

hapa kinachokuja kuumiza zaidi ni majeraha ya tatizo ndo yatakayohukumu zaidi
 
sio vizuri kila kitu kumsingizia shetani. lakini kwenye sheria ya mapenzi wanasema bora aunganishae kuliko atenganishae. sitaki kujua kilicho mfanya aondoke na kilicho mrudisha. Hadi amerudi ina maana kajifunza. so kusamehewa na halali yake. Mimi kama figganigga nishaona mengi bora amsamehe ila wakapime UKIMWI kabla ya kufanya lolote.
dawa za kienyeji saa nyingine zinafanya kazi sema zikichuja ndo inakuwa kama hivyo. Mia
 
Dina, ulipata wasaa upi wa kumsamehe wakati hakuwepo?? maisha bila yeye hayakuwa rahisi kama mtoa mada alivyoeleza, mke alipitia machungu mengi! kuendelea na utaratibu wako wa maisha kana kwamba yeye bado hayupo ni kwamba bado hujasamehe hapo!

Madabwada, kwani kutoa msamaha lazima nitamke mbele yake kuwa sasa nimekusamehe unaweza kwenda? Na ndio maisha hayakuwa rahisi ndio maana najiuliza kuwa yeye ataleta urahisi gani sasa kama sio kuniongezea wingu jeusi moyoni? Angekuwepo wakati tunahangaika na mboga zetu ningesema that's my men, kwa shida na raha. Siamini kama nitakuwa nalipa kisasi kama Husniyo alivyosema kwenye mchango wake coz sioni kama kumkatalia kurudi naweza kufananisha na kuondoka kwake. Na je una maana ila msamaha utimie ni kwa kumkubalia arudi kwenye maisha yetu? Kama ndivyo, basi aende bila msamaha.
 
hapa kinachokuja kuumiza zaidi ni majeraha ya tatizo ndo yatakayohukumu zaidi

swali langu ni je pata picha mama yoyoo kakukimbia miaka 7 na amereje anataka umsamehe mrudiane! Utamsamehe? Vp utaishi nae? (uzungumze ya moyoni mwako) na hapo alikukimbia ulipokuwa umefulia but now alaa mambo super..nipe jawabu
 
hapa kinachokuja kuumiza zaidi ni majeraha ya tatizo ndo yatakayohukumu zaidi
Bora umelielewa hilo,
Tatizo ni yeye kutaka kusamehewa,labda angefuta vile nilivyomwambia aondoke na akaondoka,
Akanipa muda mpaka pale nitakapoona au ikitokea moyo wangu ukarudi labda sijui yani hata sijui itokee nn jaman,
Itafutwe namna ya kuweza japo tuwe tunaonea tu na kuwasiliana taratibu na akaweza kunishawishi kuponesha majeraha labda inaweza tokea tukaweza kujadili swala la kuwa pamoja tena,ila nahis inahitaji mda tena labda miaka 7!
 
swali langu ni je pata picha mama yoyoo kakukimbia miaka 7 na amereje anataka umsamehe mrudiane! Utamsamehe? Vp utaishi nae? (uzungumze ya moyoni mwako) na hapo alikukimbia ulipokuwa umefulia but now alaa mambo super..nipe jawabu

kabla ya kutengana ni lazima kuna suala ambalo limepelekea kufikia hatua hiyo na inategemea nani mkosaji maana unaweza ukakosa wewe lakini hatua akachukua mwenzako ... kwa maana hiyo narudi kule kule kidonda / jeraha la wakati wa kuachana ndilo litakalokuongoza kwani hata kama ingekuwa miaka 10 bado kuna mambo wewe binafsi unaweza kuyaangalia na umuhimu na ulazima wa mtu huyo kuwa nae ..
lakini kumbuka nawe unakuwa si malaika hivyo utajikuta umeanzisha mahusiano na hilo nalo litachangia katika maamuzi yako
 
Sasa kwa mwanaume wa aina hiyo c ndio wrong selection yenyewe!
Kwa upande wangu kwa ujaji huo sitaweza kuwa naye,labda aondoke zake mpaka hapo itakapotokea moyo wangu ukafikiri vinginevyo jambo ambalo litakuwa gumu coz bado nitakuwa na majeraha.
 
C heri pia umeelewa maana kama ulikuwa na jeraha kubwa la kuachana unaweza kujikuta unachukua shoka na unamaliza ghadabu zako zote
 
hapo ndipo haswa, my dia ... ndio maana nasema kusamehe sio jambo rahisi, its a sacrifice, lkn ni rahisi tu kama upendo "usiochakachuliwa" upo!
 
hapa kinachokuja kuumiza zaidi ni majeraha ya tatizo ndo yatakayohukumu zaidi

BPM, healing is gradual process, ni kama kuuguza kidonda chochote kile mwili, maumivu hupungua kadri muda unavyokwenda, hatimaye hupona. Utabakia na kovu, lakini maumivu hayatokuwapo tena!!
 
Sasa kwa mwanaume wa aina hiyo c ndio wrong selection yenyewe!
Kwa upande wangu kwa ujaji huo sitaweza kuwa naye,labda aondoke zake mpaka hapo itakapotokea moyo wangu ukafikiri vinginevyo jambo ambalo litakuwa gumu coz bado nitakuwa na majeraha.

lakini acha kuwa so rude mpaka naogopa dah..Easy cantalisia jamani..chonde chonde
 
Sasa kwa mwanaume wa aina hiyo c ndio wrong selection yenyewe!
Kwa upande wangu kwa ujaji huo sitaweza kuwa naye,labda aondoke zake mpaka hapo itakapotokea moyo wangu ukafikiri vinginevyo jambo ambalo litakuwa gumu coz bado nitakuwa na majeraha.

the good news is, utakuwa na majeraha but with time utapona. na kwa hakika, nadhani furaha ya kupona kidonda huwa unaijua, hhuitaji nikuelezee hilo ... only sky will be the limit!!
 
BPM, healing is gradual process, ni kama kuuguza kidonda chochote kile mwili, maumivu hupungua kadri muda unavyokwenda, hatimaye hupona. Utabakia na kovu, lakini maumivu hayatokuwapo tena!!

unaweza kuuguza kidonda lakini kila ukikiangalia na jinsi ulivyokipata unawez akuumiza zaidi
 
unaweza kuuguza kidonda lakini kila ukikiangalia na jinsi ulivyokipata unawez akuumiza zaidi

hahahhaaaaa ... ni kweli, lakini with time utasahau tu. Furaha ni siku utakapo pona kabisa!
 
hahahhaaaaa ... ni kweli, lakini with time utasahau tu. Furaha ni siku utakapo pona kabisa!

hakuna time limit maana hata ukisema kidonda kimepona bado kovu litakuwepo na unaweza kujikuta jambo dogo tayari umeshachukua hatua kwa haraka kitu ambacho si kizuri kuishi kwa tahadhari au kwa kudhania jambo
 
Lakini ujue si wanaume tunapenda hawa wenzetu watusamehe lakini sie huwa wagumu kweli na matusi juu
ANGALIZO: ukimtelekeza mwanamke mwenye kipato chake ukirudi umeisha jela nje nje umkute kwenye silent mode labda
 
wakati wa kuachana kuna mambo ambayo huongoza katika hatua harisi nayo ni kiburi, dharau majivuni etc sasa nini unatarajia ukirudi???
 
C heri pia umeelewa maana kama ulikuwa na jeraha kubwa la kuachana unaweza kujikuta unachukua shoka na unamaliza ghadabu zako zote

Hiyo kitu ni ngumu sn,tena ashukuru amemkuta angekuta kaolewa je angemwombaje huo msamaha!alafu wanaume mnateteana ingekuwa ni kinyume chake dah cjui huu uzi ungekuwa page ya ngapi!mie hapo ni kumfukuza tu akaendelee na maisha yake tu ujio wake utanitonesha maumivu upya!
 
C unaweza ukawa umeoa au kuolewa baada ya kukimbiana lakini hukumu ya ukaribu au walau uwepo wa mtu unategemea na huyo uliyenaye maana naye atakupa msukumo kisaikolojia
 
mh! Hapo kumshauri nashindwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…