Mabibi na mabwana na hasa wapenda Haki, Uhuru na Maendeleo.
Haki zetu, Uhuru wetu na Maendeleo yetu haviwezi kuwa sehemu ya mjadala wa kuwa tupewe au tusipewe.
Hivi ndiyo vinavyotafsiri utu wetu kama binadamu. Hivi ni mali yetu na ni vya kupiganiwa na kulindwa kwa nguvu zetu zote.
Ni heri ya kufa tukivipigania au tukivilinda, kuliko kuendelea kuishi utumwani bila hivi vitatu.
Pemba wameonyesha dhamira zao za dhati - kuwa sasa basi.
Heko Maalim Seif na ACT. Heko Lissu na CHADEMA kwa ujumla. Mmeonyesha njia na kwa hakika hamko peke yenu.
Jitihada hizi ni za kuungwa mkono sana. Ikiwa chini ya mwamvuli mmoja itapendeza zaidi ili watesi wetu wajue tumedhamiria!
Kwamba basi hii ni basi kweli kweli.
Masomo ya Mbagala, Kawe, Segerea, Arusha, Pemba, na Zanzibar yatoshe kabisa kumwonyesha bwana yule nini tunataka.
Anao uchaguzi wa kubadilika sasa na bila ya kuchelewa au kama hataki akatupisha na kwa amani tu.
Haupo muda ulio bora wa kumfikishia salamu hizi kwa kujipanga pamoja vilivyo, sisi na washirika wetu, kuliko sasa.
Kwa vile hataki habari mbadala zisikike kupitia katika vyombo vya habari vya ndani vilivyopo kikatiba. Haiwezi basi kuwa haramu kutafuta fursa zingine zozote kokote ili kukabiliana naye.
Tuunganishe nguvu zetu kupigania haki, uhuru na maendeleo yetu.
Kwa hakika "sasa basi!"