NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Kuna kusaidia wanafamilia hii inaeleweka inabidi ujitoe, lakini sasa kuna hawa ndugu nao huwa wanajikuta sawa na familia tena akilini mwao wanajipa hadhi ya lazima wasaidiwe,
Huwa naona kuna baadhi ya koo na makabila yani wakiona ndugu yao katoboa basi wanachofikiria ni kwamba ni lazima ndugu yao awe na jukumu la kuwasaidia hasa kiuchumi.... mbaya zaidi wakianza kusaidiwa wanaacha ama kupunguza kufanya shughuli walizofanya zamani, wanaridhika kwamba kuna msaada wa uhakika.. hata kama walikuwa wanaamka kuuza maandazi asubuhi wanaacha, mzigo wao wote wanamsukumia ndugu yao
Ikitokea ndugu hawasaidii ama anawasaidia kidogo wanalalamika sana na kumpa lawama ndugu yao kwa kila shida waipatayo..