Kwenu Wanaume mnaopigwa na wake zenu. Hii ni fedheha mnajiabisha

Kwenu Wanaume mnaopigwa na wake zenu. Hii ni fedheha mnajiabisha

nakumbuka tukiwa wadogo, kila kitu ukionesha uzembe unaambiwa unashindwa hadi na msichana ....

Hivyo basi ikawa ni kesi ya jinai kwa mwanaume yoyote kupigwa na msichana maana ingeashiria udhaifu wa hali ya juu
Hii nikweli swali la kujiuliza wenzetu wamekulia mazingira Gani hayo Hadi unakalishwa na mwanamke
 
Shauri yako.Mimi siyo mbegu zenu mbilikimo zilizofubaa.Na hata hivyo,kupigwa na mwanamke ni uzwazwa uliopea uhalisia.Kwa nini upigwe?
😂😂😂 Uzuri sijawah pigwa na mwamke Mimi nakumbuka nilkuwa napigana na dada yangu nae mufuata mara3 lkn alikuwa anakimbia maana anapiga kunisukuma na kunitupa huko lkn nikinyanyuka kazi anayo
 
ndo nimetoka kumtandika hapa,,eti ananiachia 5000 ya meza
 
Dah basi... Nitajitahidi kusoma komenti tu bila kuview profile... Namtakia shemeji asubuhi njema...
Sawa ila hakufaham na sitamwambia mkuu. Koloni lazima lilindwe Kwa gharama yyte

Hakuna kuingiliwa koloni la mwenzako

Berlin conference 1884
 
Tusipende kubeba makurumbembe tujikadirie tunaowamudu.

Kuna pisi ilijichanganya kunitest, ndio siku pekee nilijua hana macho madogo...
 
Japo sio rahisi kusema lkn wapo wanaume wengi sana wanopokea kipigo kutoka Kwa wake zao.

Kwa macho yangu shangazi yangu alikuwa anakung'uta vilivyo mmewe.

Siku akiliazisha Hadi alikuwa anakimbia na kwenda kujificha kabisa.

Kuna mama mwingine alikuwa muuza gongo (pombe) akasikia fununu Kwa walevi kuwa mmewe ana Mla kimasiahara msimbe mmoja (single mother/mwanamke aliyeachika Kwa mmewe).

Basi muda sio mrefu jamaa akawa amefika hapo kijiweni alipokea kipondo hadharani na akadharaulika sana hapo kijijini.

Shangazi yeye alijua ufalme ni wake siku zote kumbe kadiri anavyozeeka na nguvu Zina muisha.

Siku Tena alilianzisha akijua ndo zilezile zama zake kumbe zama zimebadirika kitambo.

Jamaa alimpiga kama Ngoma huku akiji mwambafai kuwa nilikuwa nimekuangalia tu Kwa kipindi kirefu sana😂😂

Hadi naleta kisa hiki kwenye Saba Saba tu hii Tena jamaa kapokea
Mkong'oto wa maana mbele yetu.

Huku akituomba msaada kuwa tumsaidie maana Hali ni mbaya kama amepigwa Hivi kitaa vipi akifika kwakwe yamkini atapigwa kama dufu.

Japo inachekesha ama kufurahisha lkn ni aibu na fedheha kubwa Kwa mwanaume kupigwa na mke wako!

Kwakweli thamani Yako inakosekana kabisa asee.

Umewahi ona mwanaume anapigwa na mke wake?
kipindi nipo mdogo kuna jamaa mmoja alikuwa jirani na nyumbani... haipiti siku 3 au 4 nasikia kichapo kinatembea... ila alikuwa anapiga kelele yeye huku anasema JAMANII EEEHHH NAUA HUKU! lakini nikitafakari kwa kina, nahisi kabisa zile kelele za maumivu na kama anaua mbona mke wake apigi kelele? aaahhh! siku zika zuka tena hizo kelele... kwenda kuchungulia jamaa anakula mikanda yeye na machozi huku yakimtoka... hahahahahahahahah!!! nikakumbuka nyimbo ya bushoke nikasema daaah! nikweli mume bwege huyu!!!! na anaweza msindikiza hata mke wake guest na kumsubiria nje akisubiri nje akiamini kuwa mule guest kaingia kuongea mambo ya business hahahahahah!
 
Wanaume sampuli hiyo ni wa kuhurumiwa sana
 
Back
Top Bottom