Kwenu wanawake mnaojifanya ma-FBI

Kwenu wanawake mnaojifanya ma-FBI

Proverbs 31:27 She watches over the ways of her household...

Sio tu kuchunguza simu; chunguza kampani yake, wanaongea nini wanafanya nini; hata mkeo akikwambia anaenda kanisa la jirani kwenye maombi hakikisha unajua ni Mchungaji wa aina gani anayeilisha nafsi yake; anamfundisha nini? Hadi magroup ya wasap sijui Vicoba ; know exactly wanachofundishana huko. Usikae kibwege hadi nafsi ya mwenzi wako ikaangamia; Mungu amekuamini na maisha ya mwenzi wako

Muwe mnasoma Biblia yote, sio kuchukua kifungu kimoja kimoja kinachojustify mambo yenu.
Ubarikiwe mpendwa maana unapambana na watu wanaotaka nyeusi iwe nyeupe.
 
ishanitokeaga hii, hawa watu wapuuzi sana aisee. Nilikuta ktukana watu kibao na kisha kawablock
 
Ni vigumu kumchunga mwanaume... tena nasisitiza ni vigumu...

Ukitumia nguvu kumchunguza ndo utazidi kumpoteza...

Kama wewe ni mwanamke na una IMANI na MUNGU umuombee mume wako sana...

Maombi yako yanaweza kumtoa ktk vishawishi...

Uzuri ni ubatili bali mwanamke atakayemcha BWANA ndiye atakayesifiwa.
una akili sana aisee. Natamani ningepata mke kama ww
 
Ningumu kutokagua ila ukiikagua utaenda tafuta danga yaani nakumbuka nilikuwa nafukuzia simu ya mzee napia simu ya mzee yaani tunapiganaga mpaka nilimtoa meno na stuli walahi ila nilikuja waza nikaona kama mama yake amemshindwa akanipasishia mimi iweje mie ndio niumize kichwa kisa simu tu nikaacha waleo nope .
Hata kwahisia tu hapana.
we mkorofi sasa! yaani mm mwanamke wa kunipiga na stuli kesho yake unafungasha virago forever
 
Wewe mwanaume wa hovyo.. nanwi kwakwambia mwanamke awe hivyo!!! Wewe ndio mal**ya, umekujaa uchafu sana.. ni kama jinamwizi.. unafikirwi upo wewe tu duniani.. humwezi ndoa acha mke na nyie hamjaoa.. mwamuona mutenda dhambi huyu!!
aisee umerudi mkuu!! ulitamba sana wakati wa bashite. Ulikuwa na matusi balaaa. Bashite alipotumbuliwa nawe ukatumbuliwa nn?
 
Nilipokuwa 20 to 21 ndio niliona bora nisishike simu ya mzee ila mzee anashika simu yangu wewe eti sikuamini wah huyu naye ..

Sioni sababu ila nawapa elimu hii wanandoa sana sana wanaume .
1. Sio sifa kuwa na michepuko ni mbaya inaleta mikosi ndani ya familia .
2. Usiwe na dharau kwa mwanamke aliyejitoa kwako inamaanisha yule aliyekuona unamfaa katika maisha yake .
Ambaye anakuheshimu, kukujali nakukuvumilia madhaifu yako kukusitiri.
3. Usidhubutu kumwoneshea mkeo kuwa wewe unawanawake njee na yeye ndiye anajikomba wakati kaenda leba kwa ajili ya mbegu yako ili uitwe baba.
4. Heshimu ndoa , muheshimu yeye napenda san kuheshimu familia yako.
5. Daima kumbuka anayekupenda ni mmoja na wawili nanihawa mama na mkeo tu . Ndio wanawake wawili ulionao katika maisha haya jaribu kumuheshimu.
6. Isipite hata siku moja kumtukana mkeo kumtukana umuite maneno ya kipuuzi nahuku ndio analinda familia yako.
Anaihudumia je akikuulia watoto wako , mama yako na ndugu waliokuja kukusalimu kwa sumu utafanya nini??
7. Isipite siku hujawahi mwambia maneno mazuri .
8. Umalaya sio dili tulia tunza familia maisha yenyewe ndoo haya sina jingine usiku mwema
Umemaliza, ujumbe mzuri Sana
 
Cha msingi tuache uzinzi, simu hazina shida yoyote. Na inapofika mahali mwenza wako anakuwa free na simu yake, hata wewe kuna muda unakuwa huna habari nayo kabisa. Sasa mtu akifika tu home simu silent; imagine mume anaweka password ili mke asishike simu. Hiyo ni ndoa au?
Password kama flyover za New York [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa kweli sishiki simu ya mtu ila akitaka yangu ashike tu. Sio tu kushika simu huwa sitaki kujua upande mwingine ambao mtu hajataka kunionyesha. Hii ni kwa ajili ya amani ya moyo maana nikijua baya la baby sitaweza kuvumilia. Nailinda furaha yangu sana kwa kweli nisiyoyaona sitakagi kuyajua kabisaaaaa.
Halafu unashika/chunguza simu ya mwenzio unataka kuona nini? Hamuaminiani? Ukishaona unaweza kumuacha huyo mwenza au unajitafutia kukereka?

Kila mtu ashike simu yake kama ni mhangaikaji utajua tu hata bila kushika simu.
Unaakili nyingi Sana
 
Sababu ya kushika simu yamtu kuanza kuchunguza ni Nini?simuamini au na kma simuamini nikikuta ambacho siwez kustahimili maana yake naweza kumuacha au naendlea kuwa nae?

Kumuamini mtu na kumlinda sio lazima umchunguze kunamengi hayako wazi sio uzinzi tu na huenda yasiwe mabaya lkn unaweza usjisikie vizuri simu inaprivacy nyingi na kushika haina maana ndo utajua kilakitu Bali kumtafutia mbinu za kufanya ashtukiwe mzinzi ni mzinzi tu hata umkague vipi huenda akawa anaenda kubeba Malaya anakruka nao na hana hta namba zao... ukimwi ukopalepale muhimu kuwekana wazi kuelezana ukweli ataesikia na asikie na heshima ifate mkondo wake...
Wanawake wanao jitambua utawajua tu akili zao. Yaani unakuta mtu Hadi anasahau majukumu yake kwenye ndoa kisa kukimbizana na simu ya mtu ...yaani utafikiri ameoa/olewa kwa ajiri ya hiyo kazi
 
Mimi alikagua simu alichokutana nacho usiku mzima alikuwa analia baadae kesho yake nikasikia akijisemea mwenyewe kwa vile unatutunza vizuri mimi nitakuombea tu na mimi niliendelea kukaza kuwa mbishi mpaka leo ila sasa naona mambo sawa

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Yaani hiyo ishu haiwabakizi salama
 
Proverbs 31:27 She watches over the ways of her household...

Sio tu kuchunguza simu; chunguza kampani yake, wanaongea nini wanafanya nini; hata mkeo akikwambia anaenda kanisa la jirani kwenye maombi hakikisha unajua ni Mchungaji wa aina gani anayeilisha nafsi yake; anamfundisha nini? Hadi magroup ya wasap sijui Vicoba ; know exactly wanachofundishana huko. Usikae kibwege hadi nafsi ya mwenzi wako ikaangamia; Mungu amekuamini na maisha ya mwenzi wako

Muwe mnasoma Biblia yote, sio kuchukua kifungu kimoja kimoja kinachojustify mambo yenu.
Alie oa hapa naamini Moto wa kiama ameanza kuufaidi duniani. [emoji38][emoji38][emoji38]
 
Back
Top Bottom