sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Mama ni moyo ana mapenzi ya dhati yaliyovuka mipaka kwa mwanae, leo hii hata mama yako ukimwambia unataka kuwa msanii hata kama hujui kuimba atakupa sapoti, mapenzi haya kwa mtoto kuna muda huwa yanapofusha kushindwa kuona uhalisia.
Baba ni kichwa, mlinzi na mtafutaji, leo hji ukimwambia unataka kuwa msanii atatafakari na kuona mbali maana ukiwatoa kina Diamond, Kiba, Harmonize na wasanii wengine wachache waliofanikiwa, kuna lundo kubwa sana la wasanii miaka nenda rudi wamesota na wengine waliwahi kuvuma ila leo hii wamechuja na hata kiuchumi wanatia huruma, atakupa makavu na hatakusapoti kwa sababu anahofia unaweza usipate maendeleo ya uhakika kwenye muziki, atakwambia ni bora akufanyie connection kwa rafiki yake fundi seremala ama fundi ujenzi ujifunze hio stadi nawe uwe fundi ama hata akutaftie shamba ukalime uwe na uhakika wa kujitegemea.
Hapo ukitumia hisia utaona mama anakupenda ila ukitumia akili unaona baba anakujali.
ila kadri umri unavyoenda mtoto wa kiume akiacha kuwa tegemezi na kuanza kujitegemea, kuhama, kujitaftia ridhiki, kuwa na familia, n.k basi hapo ukaribu kwa baba unaongezeka maana wanaanza kufanana, mtoto na baba wote wanajitaftia ridhiki, mtoto na baba wote wameoa, mtoto na baba wote walihama kwao kujitegemea, n.k.
yote kwa yote wote wana umuhimu, ukipatwa na tatizo mama atakuwa karibu na wewe sana huku mzee akihangaika huko nje kukunasua kwenye tatizo kadri ya uwezo wake wote, hapo ndipo wengi wanakosea wanadhani mama ndie mwenye umuhimu zaidi lakini wanasahau baba yupo nje anapambana ili kuwanasua kwenye matatizo ya ujinga kwa kuwapa mahitaji ya elimu, kuwaondolea njaa kwa kuwalisha, kuwasitiri kwa kuwavisha, kuhakikisha hamlali nje kwa kulipia kodi ya nyumba au kujenga, kuwatoa uvivu kwa kuwapa kazi za kufanya nyumbani, kuwanusuru katika maamuzi mabaya yanayoweza kuwapeleka jela kwa kuwatia adabu tangu mkiwa wadogo, n.k.
mchango wa baba ukitaka kuujua kama wewe ni mtoto wa kiume anza kujitegemea nakwambia utaujua tu, tena ukija kuoa na uwe na familia utapata picha nzuri zaidi... ila kama bado unaishi kwenu bado hujawa mwanaume wa kuondoka kwenye kiota ukajitegemee hapo itakua kazi kuona mapenzi ya baba.