Kwenye ekaristi takatifu ni Yesu au Mungu katika nafasi tatu??

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Kwa wakristo wanaoamini Imani ya TRANSUBSTANTIATION, kwenye mkate na divai, pale ni Yesu peke yake yupo? Maana Mungu ni mmoja na hagawanyiki. Basi tulipaswa kusema pale Yuko Mungu katika ukamilifu wake, katika nafsi zote tatu, ama sivyo basi yupo Yesu katika Hali yake ya kibinadamu tu na umungu wake haupo pale. Tujadili hili Kwa mapana na marefu ya kitheolojia.
 
Kwenye kichwa Cha Uzi ilitakiwa kusomeka Nafsi tatu na siyo NAFASI TATU. Unfortunately hakuna namna ya kurekebisha kichwa Cha uzi
 
Kwa wakristo wanaoamini Imani ya TRANSUBSTANTIATION, kwenye mkate na divai, pale ni Yesu peke yake yupo? Maana Mungu ni mmoja na hagawanyiki. Basi tulipaswa kusema pale Yuko Mungu katika ukamilifu wake, katika nafsi zote tatu, ama sivyo basi yupo Yesu katika Hali yake ya kibinadamu tu na umungu wake haupo pale. Tujadili hili Kwa mapana na marefu ya kitheolojia.
tujadili kwa reference ipi maana wakatolik hawafuati biblia peke yake, pia wanachanganya na mila na desturi za kipagani za kirumi au pia wakiamua jambo lolote linakuwa, hivyo kujadili ni kupoteza muda.
 
Pale alikuwa Yesu peke yake nafsi ya pili ndo maana ukisoma vizuri kitabu unakuta katika mistari inayoendelea baada ya kuwapa damu yake akisema kuwa yeye hatainywa kamwe paka atakapokunywa mpya ufalme wa Baba yake ukija.

Yohana 15:1
Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

Mathayo 26:29
Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.

Hivyo pale alikuwa peke yake.
 
Mbona walioamua Biblia iwe na maandiko Gani?(cannon of scriptures) ni wakatoliki? Kuna kanisa lolote liliweka mkusanyiko wa maandishi unaoitwa biblia zaidi ya Roman church?? Yote yalikuwa ni oral tradion ambazo siku hizi zinaitwa mapokeo.
 
Kulikuwa na sababu za kuchanganya na Mila za kipafani just to win the pagans. Nakiri Kuna sehemu walikoaea japo the intention was good. Kwa mfano Kwa sababu tarehe ya kuzaliwa Yesu haijulikani wakateka tarehe ya wapagani ya kuzaliwa MUNGU JUA wakaibadili kuwa sikukuu ya Christmas. It was just a tactical issue.
 
Endeleeni kulishana sumu, sumu ni nyingi hadi kwamba Petro alikuwa Pope
 
Pale alikuwa Yesu peke yake nafsi ya pili ndo maana ukisoma vizuri kitabu unakuta katika mistari inayoendelea baada ya kuwapa damu yake akisema kuwa yeye hatainywa kamwe paka atakapokunywa mpya ufalme wa Baba yake ukija.

Yohana 15:1
Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

Mathayo 26:29
Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.

Hivyo pale alikuwa peke yake.
Mpya ni upi?
 
Kulikuwa na sababu za kuchanganya na Mila za kipafani just to win the pagans. Nakiri Kuna sehemu walikoaea japo the intention was good. Kwa mfano Kwa sababu tarehe ya kuzaliwa Yesu haijulikani wakateka tarehe ya wapagani ya kuzaliwa MUNGU JUA wakaibadili kuwa sikukuu ya Christmas. It was just a tactical issue.
mkuu watu wana intention zao, ibada ya mungu jua inaendelea, hiyo ni dini, huwezi kuchanganya vitu havieleweki kisa unavuta watu, never
Hapo umesahau kuongelea ibada ya jua -jumapili (sun day)
eti tactical issue
sanamu zipo pale nazo ni tactical
 
Asante mkuu. Mungu alikataza sanamu?? Kama ni hivyo na hicho kitabu chako unachokiita Biblia kichome moto maana nacho ni SANAMU YA MANENO! Hukusoma habari ya sanamu wa Shaba au sanduku la agano???
 
mkuu watu wana intention zao, ibada ya mungu jua inaendelea, hiyo ni dini, huwezi kuchanganya vitu havieleweki kisa unavuta watu, never
Hapo umesahau kuongelea ibada ya jua -jumapili (sun day)
eti tactical issue
sanamu zipo pale nazo ni tactical
Wewe ni MKRISTO au MYAHUDI?? Fuata aliyofundisha Yesu waachie Wayahudi ( Jews ) dini na Imani Yao. Hao Hawamuamini Yesu. Ukiekaa na Imani Yao ndio utapotoshwa na hao manabii na mitume wa Leo wa kukurudisha kwenye mafundisho ya Musa na Eliya wale pesa yako. They cannot even figure out what happened at Mount Tabor ( The mount of TRANSFIGURATION). Hawajaelewa lolote kuhusu KUGEUKA SURA Kwa YESU KRISTO na kuonekana na kutoweka Kwa MUSA na ELIYA.
 
Mambo yaliyotokea mlima TABOR yana maana kubwa sana ambayo hawa theologians uchwara na PH.D zao za makaratasi hawayaelewi. It was not a fan show!
 
Hawa watu wana IQ kubwa, walichonga hayo mambo kwa makini kiasi Dunia karibu nusu wanaamini. Jamani ni watu wameweka mambo yao, hapo hakuna Mungu. Nakushauri ndugu yangu Mwafrika, Baki na imani ya mababu zako.
 
Back
Top Bottom