Kwenye ekaristi takatifu ni Yesu au Mungu katika nafasi tatu??

Kwenye ekaristi takatifu ni Yesu au Mungu katika nafasi tatu??

tujadili kwa reference ipi maana wakatolik hawafuati biblia peke yake, pia wanachanganya na mila na desturi za kipagani za kirumi au pia wakiamua jambo lolote linakuwa, hivyo kujadili ni kupoteza muda.
Wakatoliki wanasoma biblia kuliko kiumbe yeyote duniani.Ukihidhuria misa mfululizo kwa miaka mitatu unakamilisha biblia nzima kuanzia Mwanzo hadi ufunuo.Kila misa masomo ya Injili,agano la kale,agano jipya husomwa.Si kama.wale.wanaokaririshwa mistari wanayopenda kusikia
 
Kwa wakristo wanaoamini Imani ya TRANSUBSTANTIATION, kwenye mkate na divai, pale ni Yesu peke yake yupo? Maana Mungu ni mmoja na hagawanyiki. Basi tulipaswa kusema pale Yuko Mungu katika ukamilifu wake, katika nafsi zote tatu, ama sivyo basi yupo Yesu katika Hali yake ya kibinadamu tu na umungu wake haupo pale. Tujadili hili Kwa mapana na marefu ya kitheolojia.
Hakuna namna ya kumtenga Yesu na Uungu wake. Pia wakati wa mageuzo anatumia maneno yaliyo very direct, mkate alisema " Huu ni mwili wangu .... " divai akasema " Hii ni damu yangu ..." thamani ya sadaka yake msalabani si sababu ya ubinadamu wake bali Mungu aliyetwaa mwili na ndivyo vinavyowakilisha fumbo la Ekaristi.

Ndio maana Yesu mwenyewe anasema mimi ni mkate wa uzima! Huwezi kuwa mkate wa uzima bila Uungu.

Hii mada haina tofauti na wale wanaoamini Bikira Maria hakuzaa Mungu, hivyo Wakatoliki wanakosea kumuita mama wa Mungu maana Mungu hazaliwi! Lakini ukiwauliza Yesu ni Mungu au si Mungu wanasema ni Mungu!

Mungu ili kukamilisha agano lake la ukombozi ilikuwa lazima awe mtu. Hivyo tafsiri ya Utatu inabakia kiutendaji au namna Mungu anavyofanya kazi lakini haiweki Miungu watatu. Ni namna ya akili na ufahamu wetu unavyoweza kuelewa mambo au mafumbo ya mbinguni.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Hii mada wale wa makanisa ya kipentekoste haiwafai. Hawaamini Ekaristi ni Yesu mzima ktk maumbo ya mkate na divai. Wao yeyote anaweza kuandaa meza ya Bwana na kushiriki! Yeyote as long ameokoka anaweza kufanya mageuzo na wanajilisha wenyewe mkate na divai.

Makanisa ya Kiprotestanti tunatofauti moja juu ya kuamini Ekaristi ni Yesu mzima lakini machafuko mengine yaliyopo makanisa ya kiroho hayapo ikiwemo kila mtu kuweza kufanya mageuzo.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Hawa watu wana IQ kubwa, walichonga hayo mambo kwa makini kiasi Dunia karibu nusu wanaamini. Jamani ni watu wameweka mambo yao, hapo hakuna Mungu. Nakushauri ndugu yangu Mwafrika, Baki na imani ya mababu zako.
Imani ipi??
 
Hakuna namna ya kumtenga Yesu na Uungu wake. Pia wakati wa mageuzo anatumia maneno yaliyo very direct, mkate alisema " Huu ni mwili wangu .... " divai akasema " Hii ni damu yangu ..." thamani ya sadaka yake msalabani si sababu ya ubinadamu wake bali Mungu aliyetwaa mwili na ndivyo vinavyowakilisha fumbo la Ekaristi.

Ndio maana Yesu mwenyewe anasema mimi ni mkate wa uzima! Huwezi kuwa mkate wa uzima bila Uungu.

Hii mada haina tofauti na wale wanaoamini Bikira Maria hakuzaa Mungu, hivyo Wakatoliki wanakosea kumuita mama wa Mungu maana Mungu hazaliwi! Lakini ukiwauliza Yesu ni Mungu au si Mungu wanasema ni Mungu!

Mungu ili kukamilisha agano lake la ukombozi ilikuwa lazima awe mtu. Hivyo tafsiri ya Utatu inabakia kiutendaji au namna Mungu anavyofanya kazi lakini haiweki Miungu watatu. Ni namna ya akili na ufahamu wetu unavyoweza kuelewa mambo au mafumbo ya mbinguni.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Shukrani umejibu Kwa akili japo Kwa kusema Maria alimzaa Mungu si sahihi. Mungu hawezi kuzaliwa at least for the true meaning of the word. Ulisema alivaa mwili uko sahihi.
 
Pale alikuwa Yesu peke yake nafsi ya pili ndo maana ukisoma vizuri kitabu unakuta katika mistari inayoendelea baada ya kuwapa damu yake akisema kuwa yeye hatainywa kamwe paka atakapokunywa mpya ufalme wa Baba yake ukija.

Yohana 15:1
Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

Mathayo 26:29
Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.

Hivyo pale alikuwa peke yake.
Aah kumbe na ufalme wa Wakristo una vileo!

Maana siku zote nililikuwa nawasikia wakibeza waislamu kuwa pepo yao itakuwa na vileo
 
Hakuna namna ya kumtenga Yesu na Uungu wake. Pia wakati wa mageuzo anatumia maneno yaliyo very direct, mkate alisema " Huu ni mwili wangu .... " divai akasema " Hii ni damu yangu ..." thamani ya sadaka yake msalabani si sababu ya ubinadamu wake bali Mungu aliyetwaa mwili na ndivyo vinavyowakilisha fumbo la Ekaristi.

Ndio maana Yesu mwenyewe anasema mimi ni mkate wa uzima! Huwezi kuwa mkate wa uzima bila Uungu.

Hii mada haina tofauti na wale wanaoamini Bikira Maria hakuzaa Mungu, hivyo Wakatoliki wanakosea kumuita mama wa Mungu maana Mungu hazaliwi! Lakini ukiwauliza Yesu ni Mungu au si Mungu wanasema ni Mungu!

Mungu ili kukamilisha agano lake la ukombozi ilikuwa lazima awe mtu. Hivyo tafsiri ya Utatu inabakia kiutendaji au namna Mungu anavyofanya kazi lakini haiweki Miungu watatu. Ni namna ya akili na ufahamu wetu unavyoweza kuelewa mambo au mafumbo ya mbinguni.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Hapo kwenye Mungu si watatu umenena vema kabisa. IT IS ONLY THE WAY GOD MANIFESTS HIMSELF TO US na sisi tumekosa namna nzuri ya kuelezea tukaja na nadharia ya TRINITY. Shukrani Kwa mchango wako
 
Aah kumbe na ufalme wa Wakristo una vileo!

Maana siku zote nililikuwa nawasikia wakibeza waislamu kuwa pepo yao itakuwa na vileo
Hayo ni mafundisho ya Wayahudi siyo ya Wakristo. Wayahudi wanaamini huko MBINGUNI Kuna nyama ya LEVIATAN na mvinyo uliosindikwa miaka 7000 iliyopita. Hayo siyo mafundisho ya kikristo
 
Wakatoliki wanasoma biblia kuliko kiumbe yeyote duniani.Ukihidhuria misa mfululizo kwa miaka mitatu unakamilisha biblia nzima kuanzia Mwanzo hadi ufunuo.Kila misa masomo ya Injili,agano la kale,agano jipya husomwa.Si kama.wale.wanaokaririshwa mistari wanayopenda kusikia
Sahihi kabisa lakini wapo pale kusomewa tu as a ritual. Muulize mkatoliki Biblia ina vitabu vingapi nakuhakikishia asilimia 90 hawajui chochote. Nimezaliwa na kukulia kwenye familia katoliki. Wewe ni mfano wa wale wanaoelewa hat Nini maana ya mwaka A au B wa kanisa.
 
Hawa watu wana IQ kubwa, walichonga hayo mambo kwa makini kiasi Dunia karibu nusu wanaamini. Jamani ni watu wameweka mambo yao, hapo hakuna Mungu. Nakushauri ndugu yangu Mwafrika, Baki na imani ya mababu zako.
Sasa ndugu nikikuuliza imani ya mababu zangu ni ipi unaweza ukaniambia hapa?

Tuelewe kila mtu anatafuta amani na atatulia pale anapoona hiyo amani ipo no matter wapo watakaosema amepotea muhimu yeye ameona panamfaa.
 
Kwa wakristo wanaoamini Imani ya TRANSUBSTANTIATION, kwenye mkate na divai, pale ni Yesu peke yake yupo? Maana Mungu ni mmoja na hagawanyiki. Basi tulipaswa kusema pale Yuko Mungu katika ukamilifu wake, katika nafsi zote tatu, ama sivyo basi yupo Yesu katika Hali yake ya kibinadamu tu na umungu wake haupo pale. Tujadili hili Kwa mapana na marefu ya kitheolojia.
Wakiristo hawana utambuzi wa Mungu ukitaka kuamini wasikilize vizuri tu
 
tujadili kwa reference ipi maana wakatolik hawafuati biblia peke yake, pia wanachanganya na mila na desturi za kipagani za kirumi au pia wakiamua jambo lolote linakuwa, hivyo kujadili ni kupoteza muda.
Ukirisito kweli ni upagani ukitaka kuamini wafatilie kuanzia hawa wanao jiita mitume mapadri ndio kabisa kazi kuriwatwi watoto
 
mkuu watu wana intention zao, ibada ya mungu jua inaendelea, hiyo ni dini, huwezi kuchanganya vitu havieleweki kisa unavuta watu, never
Hapo umesahau kuongelea ibada ya jua -jumapili (sun day)
eti tactical issue
sanamu zipo pale nazo ni tactical
Bila kusahau jumamosi, saturday ilikuwa ni siku ya Mungu saturn. Moja ya Mungu wa kirumi na Baba wa jupiter. (Saturday = saturn + day)
 
Mbona walioamua Biblia iwe na maandiko Gani?(cannon of scriptures) ni wakatoliki? Kuna kanisa lolote liliweka mkusanyiko wa maandishi unaoitwa biblia zaidi ya Roman church?? Yote yalikuwa ni oral tradion ambazo siku hizi zinaitwa mapokeo.
Kuna biblia mbili,ya vitabu 65 na 72,hapa unazungumzia ipi!?..agano la kale ni kitabu Cha wayahudi,kimekopiwa tu Yale yaliyohitajika
 
Hakuna namna ya kumtenga Yesu na Uungu wake. Pia wakati wa mageuzo anatumia maneno yaliyo very direct, mkate alisema " Huu ni mwili wangu .... " divai akasema " Hii ni damu yangu ..." thamani ya sadaka yake msalabani si sababu ya ubinadamu wake bali Mungu aliyetwaa mwili na ndivyo vinavyowakilisha fumbo la Ekaristi.

Ndio maana Yesu mwenyewe anasema mimi ni mkate wa uzima! Huwezi kuwa mkate wa uzima bila Uungu.

Hii mada haina tofauti na wale wanaoamini Bikira Maria hakuzaa Mungu, hivyo Wakatoliki wanakosea kumuita mama wa Mungu maana Mungu hazaliwi! Lakini ukiwauliza Yesu ni Mungu au si Mungu wanasema ni Mungu!

Mungu ili kukamilisha agano lake la ukombozi ilikuwa lazima awe mtu. Hivyo tafsiri ya Utatu inabakia kiutendaji au namna Mungu anavyofanya kazi lakini haiweki Miungu watatu. Ni namna ya akili na ufahamu wetu unavyoweza kuelewa mambo au mafumbo ya mbinguni.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Yesu taita,nyota kibao, Mungu yeye,mwana wa Mungu yeye...mikato flan karata tatu,kekundu keusi
 
Yesu peke yake??? Maana alishasema MIMI NA BABA TU MMOJA
Yohana 14
1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.

4 Nami niendako mwaijua njia.

5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?

6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

7 Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.

8 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.

9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?

10 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

11 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.

12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.

14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.

16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

19 Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.

20 Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.

21 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.

22 Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu?

23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.

24 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.

25 Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu.

26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.

28 Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.

29 Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, kusudi litakapotokea mpate kuamini.

30 Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.

31 Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.
 
Kwa wakristo wanaoamini Imani ya TRANSUBSTANTIATION, kwenye mkate na divai, pale ni Yesu peke yake yupo? Maana Mungu ni mmoja na hagawanyiki. Basi tulipaswa kusema pale Yuko Mungu katika ukamilifu wake, katika nafsi zote tatu, ama sivyo basi yupo Yesu katika Hali yake ya kibinadamu tu na umungu wake haupo pale. Tujadili hili Kwa mapana na marefu ya kitheolojia.
Luka 22
1 Ikakaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo Sikukuu ya Pasaka.

2 Na wakuu wa makuhani na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua; maana walikuwa wakiwaogopa watu.

3 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara.

4 Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao.

5 Wakafurahi, wakapatana naye kumpa fedha.

6 Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano.

7 Ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja pasaka.

8 Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie pasaka tupate kuila.

9 Wakamwambia, Wataka tuandae wapi?

10 Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye.

11 Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki wapi chumba cha wageni, nipate kula pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu?

12 Naye atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa; andaeni humo.

13 Wakaenda, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa pasaka.

14 Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye.

15 Akawaambia, Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu;

16 kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.

17 Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi;

18 Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja.

19 Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]

21 Walakini, tazama, mkono wake yeye anayenisaliti upo hapa pamoja nami mezani,

22 Kwa kuwa Mwana wa Adamu aenda zake kama ilivyokusudiwa; lakini, ole wake mtu yule amsalitiye!

23 Wakaanza kuulizana wao kwa wao, ni yupi miongoni mwao atakayelitenda jambo hilo.

24 Yakatokea mashindano kati yao, kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa.

25 Akawaambia, Wafalme wa Mataifa huwatawala, na wenye mamlaka juu yao huitwa Wenye fadhili;

26 lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye.

27 Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye.

28 Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu.

29 Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi;

30 mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

31 Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;

32 lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.

33 Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni.

34 Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui.

35 Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!

36 Akawaambia, Lakini sasa mwenye mfuko na auchukue, na mkoba vivyo hivyo; naye asiye na upanga, na auze joho yake akanunue.

37 Kwa kuwa nawaambia, hayo yaliyoandikwa hayana budi kutimizwa kwangu; ya kuwa, Alihesabiwa pamoja na wahalifu. Kwa sababu yanipasayo yanao mwisho wake.

38 Wakasema, Bwana, tazama, hapa pana panga mbili. Akawaambia, Basi.

39 Akatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa desturi yake; wanafunzi wake nao wakafuatana naye.

40 Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.

41 Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba,

42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.

43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.

44 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]

45 Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni.

46 Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni.

47 Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Thenashara, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu.

48 Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?

49 Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotukia, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga?

50 Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume.

51 Yesu akajibu akasema, Mwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya.

52 Yesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maakida wa hekalu, na wazee, waliokuja juu yake, Je! Mmekuja wenye panga na marungu kama kukamata mnyang'anyi?

53 Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza.

54 Wakamkamata, wakamchukua, wakaenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Na Petro alimfuata kwa mbali.

55 Na walipokwisha washa moto katikati ya kiwanja, waliketi pamoja, naye Petro akaketi kati yao.

56 Ndipo mjakazi mmoja akamwona ameketi mwangani, akamkazia macho akasema, Na huyu alikuwa pamoja naye.

57 Akakana, akisema, Ee mwanamke, simjui.

58 Baadaye kitambo mtu mwingine alimwona akasema, Wewe nawe u mmoja wao. Petro akasema, Ee mtu, si mimi.

59 Halafu, yapata saa moja, mtu mwingine alikaza kusema, Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya.

60 Petro akasema, Ee mtu, sijui usemalo. Na papo hapo alipokuwa katika kusema, jogoo aliwika.

61 Bwana akageuka akamtazama Petro. Petro akalikumbuka lile neno la Bwana jinsi alivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu.

62 Akatoka nje akalia kwa majonzi.

63 Na wale watu waliokuwa wakimshika Yesu walimfanyia dhihaka, wakampiga.

64 Wakamfunika macho, kisha wakamwuliza-uliza wakisema, Tabiri, ni nani aliyekupiga?

65 Wakamtolea na maneno mengine mengi ya kumtukana.

66 Hata kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema,

67 Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie. Akawaambia, Nijapowaambia, hamtasadiki kabisa.

68 Tena, nikiwauliza, hamtajibu.

69 Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi.

70 Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.

71 Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.
 
Back
Top Bottom