Kwenye haya Maisha kuna watu ni untouchable , hii nimejifunza kwa njia ngumu.

Maelezo yako hayajitoshelezi hata kidogo.
Unaenda kumuuliza mtu swali kama Hilo kwa lengo gani
 
You look humble
 
Binafsi Mimi siamini katika nguvu za Giza namuamini Mungu sana.

Ila kitu Ambacho nimewahi kujifunza Mimi MTU akinifanyia jambo baya huwa namsamehe na muombea Amani , kwakuwa Mimi huwa najitahidi kuishi bila kumuumiza MTU

Ila kama mnavyojua Binadamu unaweza kuwa Mwema na kujizuia kuingia katika migogoro Ila bado watu wabaya wakajaribu kukuingilia katika mipaka yako.

Hivyo Mimi sio rahisi mtu aniingilie kwa nia mbaya na abaki salama na huu sio uchawi ni mambo ya Asili tu.

Naweza kusema Mungu anatulinda au anatupambania au vyovyote vile .

Hii kitu anayo mzee Wangu pia.

Ila kuna tetesi wakati tunazaliwa Bibi yetu RIP alikuwa kuna tamaduni anazifanya ili kutulinda na kuishi maisha mazuri hapa duniani .

Hizi ni tetesi Ila nasikia yule bibi alikuwa ni untouchable
 
Mbona mimi uliniliza?
 
Ninyi watu wa hivi kila mnalogusa huwa linaenda ama sijaelewa.

Maana hata mimi kwa historia yangu wengi walionikosea kwa kiwango kile cha kuniharibia maisha yangu, huwa hawana mwisho mzuri na hata wengine hunitafuta na kuomba amani na mimi LAKINI haimaanishi kuwa na mimi huwa nafanikisha mambo yangu kiurahisi hapana kuna wakati unapitia msoto hadi unasema eeeh kweli ni kama dunia imeamua kuninyoosha vile. Nguvu hii ninayo ila nacho kiamini kwangu ni nguvu ya kupanda na kuvuna.

Afu hii si kwa mtu binafsi tu ngoja nikupe mkasa mmoja; kuna taasisi fulani nilifanyia kazi baada ya muda zikaanza ma fitina kiwango cha kukosa amani na kazi basi nikaona isiwe kesi nikawaachia ofisi yao, nikajiuzulu ndani ya masaa 24, huwezi amin hazikupita miezi mitatu ofisi ikaharibikiwa, wateja wakawakimbia, ofisi ikaanza kupunguza wafanya kazi, kibaya zaidi yule aliyenifanyia fitina hakupunguzwa ila alitumbuliwa tena kwa aibu sana, imagine mtu unaingia kazini kuendelea na majukumu yako huna hili wala lile unakutana na barua ya kuachishwa kazi, mlinzi anaitwa akusindikize ukakabidhi mali za ofisi immediately jamaa akawasha kompyuta aweke flash ahamishe document zake alizokuwa amehifadhi, anaingiza password kumbe walishamnyima access bila yeye kujua anaomba wamruhusu achukue ahamishe vitu vyake wanamwambia ni oda kutoka makao makuu sisi hatuna uwezo wa kuifungua. Unaambiwa jama alianza kutoka jasho kwenye upara wake na ukizingatia ofisi ilikuwa full kipupwe, wambea hawakawii wakanipa taarifa hizo huku wakiwa na furaha ya ajabu. Nikajisemea ofisini hakuna rafiki ni kuishi kinafiki tu.
 
Baba angu mzazi ( R. I. P) alikuwa na hiyo nguvu pia.
Sisi kwenye ukoo wetu huwa hatuibiwi, haturogwi wala kudhulumiwa.
Sasa mkuu kama mnaishi ushuani mtaibiwaje na kurogwa?
Wezi na wachawi wanapatikana sehemu zenye jamii masikini wa Elimu na kipato.
 
'Kupoteana' ndiyo kufanyaje?
Ni kupotea au kudhurika au ni kufanyaje?
 
'Kupoteana' ndiyo kufanyaje?
Ni kupotea au kudhurika au ni kufanyaje?
 
Si wengine Vijukuu wa Isaka na yakobo Mafile yetu uko Mbinguni yapo juu juu hatuna mawaa tukilia kidgo tu baya lazima likukute
 
Kupoteana ndio kufanyaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…