Kwenye hili sitaki nifeli, naombeni ushauri wenu waungwana


Hili nalo wazo
 
Forex ndo mkombozi wako usisikie ya wasioijua
 
Njoo mtera tufanye biashara ya samaki wa kubanikwa,soko lipo songea ni uhakika,tukianza na 500k siyo mbaya. Bei ya samaki bwawani 30-35/= na bei ya kuuzia Songea ni 100-200/=

Nipo tayari kusimamia hiyo biashara,karibu sana

Mtoa mada hii idea nilishawahi kuisikia kwa dogo mmoja hivi hivi nadhani inaweza kuwa nzuri sana.

Mtafute huyu
 
mkuu hongera km umejichanga na kusave toka mwezi may last year hadi sasa ni mwaka mmoja na una 10mil basi hiyo kazi yk inalipa..

kifupi hiyo hela igawe mara mbili nusu ya hela fanya biashara na nusu kaanze ujenzi kwenye kiwanja chako.
biashara zipo nyingi inategemea na wewe unapendelea ipi na namna ipi ya usimamizi, mm nitakushauri mbili tu..
moja km unataka biashara uifanye ww mwenyewe iwe chini yk 24 hrs basi hapo fanya online business tu km online financial markets e.g forex, indexes na kadhalika ila biashara hii zinakuhitaji uwe mwingi wa maarifa na mfuatiliaji wa mambo ulimwenguni hivyo km upo bize sana achana nayo ..

badala yake,
kwa mtajiwa 5mil fungua biashara ya mpesa,tigopesa,airtelmoney crdb wakala na nmb tafuta sehemu iliyochangamka hata km wapo watoa huduma km hizi usiogope angalia udhaifu wao then wewe boresha zaidi hii biashara ni nzuri na kwa mtaji huo utapata faida nzuri tatizo ni moja tu utapeli na kumpata msimamizi mwaminifu basi utapiga hatua kubwa tu.

mwisho, km utahitaji usimamizi wa biaashara yoyote kati ya hizi au tofauti na hizi nipo teyari mkuu tuyajenge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…