plan z
JF-Expert Member
- Jun 10, 2019
- 1,394
- 1,434
Mkuu Mimi naweza kukushauri kulingana na uzoefu wangu kwenye biashara ya steshenari,waweza pata hadi sh 200,000 kwa siku ikiwa utapata eneo zuri
Mfano Mimi hununua ream kwa Shiling 9000 na hiyo ream ina karatasi 500 na kopi huwa natolea sh 100 ,printing sh 500 typing na printing sh 1000 per page, kwa hiyo kama eneo ni zuri kwa biashara, ream tatu kiwango cha chini zaweza isha kwa siku Moja ambapo utakuwa umeingiza takribani 150,000 kwa kila ream.
Ukija kwenye karatasi za kusafishia picha,box Moja huwa na karatasi 100 ,ambapo Mimi huwa nasafishia kwa sh 300 ikiwa mteja atakuja na picha zake, ila nikimpiga Mimi nafanya sh 700,ambapo kama uko eneo zuri kwa siku waweza maliza box 5 kwa kiwango cha chini ambapo utakuwa umepata sh 50,000 kwa kila box hadi kuisha
Hapa ni kwa uchache sana,maana utaweka vitu Vingi tu humo bandani,maana Mimi pia Nina freezer huwa nagandisha ice creams, so faida hii unaipata bila shida mkuu
Try it,nadhani hata Mimi wakati nataka kufungua hii biashara nilileta Uzi humu,japo hili wazi la steshenari sikulitoa humu,maana nilipewa na kaka yangu ambaye hata hajasoma ila faida yake naiona,ninampango wa kuchukua mkopo nipanue hii ofisi iwe kubwa zaidi,maana hata ukiniamsha usiku ukaniuliza biashara yenye faida maradufu hapa Tanzania ni ipi nitakujibu steshenari.
Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Hili nalo wazo