Kwenye hili wakristo mna la kujifunza

Twende mahakamani leo hii nani wanaongoza kwa kudai talaka? Tena zenu mnojiita wasomi ndo hazidumu kabisaaa mna elimu mnaiacha kwenye vyeti tu sio matendo
Sasa nyie si mnaachana kwa talaka tatu tu hata mahakamani hamuendi so ndoa za kiislamu ni chache mahakamani kwa sababu hamfuati utaratibu mnamalizana kwa kadhi. Si unakumbuka ishunya dokta mwaka kesi ilikua kwa sheikh wa Dar.

Wasomi tunafuata process na tunajua kuna kugawana mali ukishangaa unaweza geuka masikini dakika sifuri....

Kusoma raha sheikh.... hata wale waislamu waliopiga shule wanafuata sheria na wana mke mmoja....

Si unaona matajiri wa kiislam kina Mo na wengine.
 
Hata kwenye ukristo mnaweza mkafungishwa ndoa na kiongozi wa dini chapu chapu tu. Kufanya sherehe ni mbwembwe tu sio hitaji la lazima kwenye dini
 
Kwa wakristu ndoa inaishia kanisani, Haichukui hata masaa ma3, Hakuna wali wala pilau ni wapendanao wa2, Ndugu, Mchungaji na pete, Shughuri imeisha.

Baada ya hapo, ni sherehe ambapo hizo ni mbwembwe zako, ila ukiamua kutoka kanisani kwenda gheto hakuna shida maana cheti unakua nacho kabisa.
 
Sisi wakristo tunaoa kwa gharama lakini mahakamani zimejaa kesi zetu za kudaiana talaka
 
Suti sio vazi la kikristo, na kanzu sio vazi la kiislamu
 
Hata kwenye ukristo mnaweza mkafungishwa ndoa na kiongozi wa dini chapu chapu tu. Kufanya sherehe ni mbwembwe tu sio hitaji la lazima kwenye dini

mbwembwe maana yake nini? kusherehekea baada ya kufunga ndoa ni utamaduni wa Christians, ni sehemu ya maisha isitoshe kwa nini ikusumbue wengine wakisherehekea? wewe nenda kwa shehe fanya ya mkeka basi maliza nendeni nyumbani kesho ongeza mwingine kama manara hivyo hiyo, kwa nini iwe ishu kwako wengine wakipenda kusherehekea tukio muhimu kabisa ktk maisha yao? ...
 
Mimi siku ya kuoa nilienda ukweni na msafara wa wapambe wangu. Nikatoa mahari, tukapiga msosi, zikafuata story mbiki tatu, nikaondoka na jiko. Ilikua shughuki ya familia mbili tu hata majirani wanaweza wasijue. Hapakua na mbwembwe za sherehe, kuvalishana pete wala kusainishana mikataba
 
Point of correction! Kwa wakristo kinachowagharimu sio ndoa ila ni sherehe za harusi ambazo sio sehemu ya ndoa hata kidogo.
 
Kazi ya pesa ni kutumika, ya nini kutafuta pesa kwa shida halafu mfurahie maisha kwa kikombe cha uji na andazi, that's madness!!
Wengine huwa wanakopa au wanaanza kusumbua kutaka michango. Mfukoni ana milioni 4, bajeti ya harusi milioni 20. Mtu hauna ili wala lile unajikuta tu umeungwa kwenye kundi la michango ya harusi.
 
Ndoa ya uji hiyo kuchepuka kunaruhusiwa kwa mwanamke sasa kazi kwako.
Kupanga ni kuchagua..!!
 
Umepaniki? Sherehe ni mbwembwe tu. Ndoa inaishia pale kanisani. Kiongozi wa dini, wasimamizi, pete na mkataba basi.
 
Hawajui kuna watu wanafunga ndoa na kurudi nyumbani.
Na wengine, kuna sherehe zinaandaliwa na kanisa.
Ndoa hata nne zote zinafanyiwa sherehe moja

Kuna options nyingi tu ila inategemeana na uwezo wako. Ukitaka kufurahisha macho ya watu, RUKSA na ukitaka ndoa ya uwezo wako. RUKHSA PIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…