Kwenye Ishu ya Uzanzibari na Utanganyika Lissu amekuwa upande wa haki siku zote

Well said
 
Lissu yuko sahihi.kila mwenye akili timsmu anamwelewa labda wanafiki na wabinafsi ndio wasiomwelewa.Huu muungano zinatumika nguvu nyingi sana kuulinda hiyo maana yake kuna madudu mengi ambayo hayako sawa,sasa badala wenye akili wayajadili mapema ili yakae vizuri wao wanataka kuyaficha ficha wakati hawatakuwepo milele kuyaficha.
 
Tatizo jingine ni kuwa Wazanzibari kwa kuwa sasa hivi mzanzibari mwenzao ndo anatawala Tanzania, wamekaa kimya, kelele za madai yao ya kutaka Zanzibar huru wameyapunguza ili wasimkwaze mwenzao kwenye kutawala ILA siku akiingia Mtanganyika Ikulu ndo utaanza kusikia kwa wingi kelele za Watanganyika wanatubana watuache tupumue!

Huu Muungano unahitaji marekebisho makubwa sana
 
Narudia tena kusema. Huu muungano Nyerere alifanya kosa kubwa sana la kihistoria. Ilitakiwa iwe nchi moja tu. Naamin muda si mrefu hili kosa litafutwa kama alivyofanya India pale cashmir. Hicho kinchi kinatakiwa kuwa mkoa basi.
 
Lissu ni mtu ya Mungu sana
 
Mkuu Lisu ni mmoja ya mtu makini sana, kosa la lisu sio kuwatetea watanganyika, wala kulalamika juu ya mambo wanayohisi yanawaumiza kwenye muungano, Tatizo la lisu ni kunasibisha matatizo ya Samia na uzanzibari wake. Hiyo ni moja njia ya kutengeneza chuki za kibaguzi kwenye jamii, Lisu anajua nini anafanya anachofanya lisu ni kutembea na upepo unavyovuma Lakini Lisu anaelewa vizuri sana ni nani anaeumia kwenye huu Muungano, Infact karibuni tu aliwahi kuzungumza kuhusu hizo ishu za nafasi za ubunge na ukuu wa wilaya ni moja kama rushwa wanayotoa Tanganyika ili waendelee kuwatuliza wana CCM wa Zanzibar waendelee kutawala zanzibar.

Mimi ni mshabiki mzuri wa Lisu, ila tuseme ukweli kuwa safari hii ameteleza kidogo,. Ila kwa upande wa pili anachokifanya Lisu wazanzibari wanakifurahia sana mana ndipo wanapopataka kinuke ili kieleweke. tafauti na watangyika wengi wanavyohisi humu mitandaoni wao wanahisi kama vile wanawakomalia.
 

Hapana mkuu hilo sio kweli, Kinachowafanya wazanzibar kuwa kimya nikuwa wana hope kuwa Samia anaweza akafanya kitu Zanzibar, inavyosemekana kumekuwa na vikao vya siri vya hapa na pale baina ya Samia na ACT, na amekuwa akimbana bana Mwinyi kwenye mapambao yake na ACT. Kama unakumbuka majuzi tu ACT walitangaza kuwa wanajitoa Serikali ya umoja wa kitaifa, Samia aliwaita wakaelewana na ndio mana wametulia.

Wanahope kuwa anaweza kutatua matatizo ya tume ya Uchaguzi zanzibar. na ndio mana unawaona wametulia.
 
Narudia tena kusema. Huu muungano Nyerere alifanya kosa kubwa sana la kihistoria. Ilitakiwa iwe nchi moja tu. Naamin muda si mrefu hili kosa litafutwa kama alivyofanya India pale cashmir. Hicho kinchi kinatakiwa kuwa mkoa basi.

Unasikitisha sana, Halafu nawewe pia unawezakuta unalalamikia wakoloni walituonea wakati mindset yako haina tofauti na walivyokuwa wao.
 
Unasikitisha sana, Halafu nawewe pia unawezakuta unalalamikia wakoloni walituonea wakati mindset yako haina tofauti na walivyokuwa wao.
Kwan wakolon walikuwa na shida gan ambayo leo haipo. Tufafanulie
 
Shida ni moja wachumia tumbo ukigusa maslahi Yao tu unaonekana mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…