Kwenye mahusiano kila mtu ana mapungufu yake , kumuacha mtu ni kutafuta mapungufu mapya kwako

Kwenye mahusiano kila mtu ana mapungufu yake , kumuacha mtu ni kutafuta mapungufu mapya kwako

Moto wa volcano

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
2,682
Reaction score
6,638
Usifikirie kubadilisha mahusiano ndio hautakutana na matatizo/ changamoto . Kila mtu atakuja na changamoto zake mpya. Kuna muda jifunze human nature , mapungufu madogo ya mpenzi wako yavumilie. Unaweza ukamuacha mtu m baya ukakutana na m baya zaidi. Ukasema ni afadhali yule
 
Mi nikipenda sina kawaida yankuacha ata kama madhaifu ya huyo mtu kuomba pesa

Wakuu mi napenda na nakuwaga seriously kwenye mahusiano

Wakuu mi napenda sana na napenda na madhaifu ya mtu
Mi siachi
 
Mapungufu yanayostahili au kupaswa kuvumiliwa ni yale ya kimaumbile na ya kibinadamu ambayo kila mwanadamu kwa kuwa hatujakamilika wakati mwingine tunateleza.......

Kumvumilia mtu ambaye kwa utashi wake na msukumo wa tamaa ameamua kukusaliti na kulala na mwanamke/mwanaume mwingine huo sio uvumilivu bali ni ujinga.........

Kumvumilia mtu anayekupiga mara kwa mara na hata wakati mwingine kuhatarisha usalama wako na afya yako huo sio uvumilivu bali ni ujinga

Kumvumilia mtu ambaye alipaswa sehemu ya kukufariji, kukutia moyo na kukupa furaha badala yake kila uchao anakuletea kero, mauzi na makasiriko sio uvumilivu ni UJINGA.......
 
Ilo kweli huwez vumilia mpk mkauana halaf huyo mleta mada watu wa kiuana kwenye mahusiano atakuja kusema si bora mngeachana tu ndo binadam hao 😁😄😆😂
🤣🤣🤣 Mimi nilikuwa nashauriwa kuwa ndoa ni kuvumilia...hivyo niendelee kuvumilia...nilipokoswakoswa panga na kukimbia,haohao wakasema bora uachane naye...ningekufa je wangesemaje?

Za kuambiwa changanya na zako..maisha ni yako si ya mwingine,ukifa linasahaulika mpaka jina lako
 
Haya mimi ni kijana wa kiume
Miaka 23-25
Mkoa dasalam
Nimejiajiri

Njo PM ili tuongee zaidi....
Moyo wangu bado una gape la kupenda.
Your warmly welcome dear
Dahh nishakuwa mshangazi kama ndo ivi😢
 
Back
Top Bottom