Mapungufu yanayostahili au kupaswa kuvumiliwa ni yale ya kimaumbile na ya kibinadamu ambayo kila mwanadamu kwa kuwa hatujakamilika wakati mwingine tunateleza.......
Kumvumilia mtu ambaye kwa utashi wake na msukumo wa tamaa ameamua kukusaliti na kulala na mwanamke/mwanaume mwingine huo sio uvumilivu bali ni ujinga.........
Kumvumilia mtu anayekupiga mara kwa mara na hata wakati mwingine kuhatarisha usalama wako na afya yako huo sio uvumilivu bali ni ujinga
Kumvumilia mtu ambaye alipaswa sehemu ya kukufariji, kukutia moyo na kukupa furaha badala yake kila uchao anakuletea kero, mauzi na makasiriko sio uvumilivu ni UJINGA.......