Kwenye maisha usiruhusu kila mtu akuzoee ni KOSA kubwa mno pia weka muda maalum wa watu kukupigia simu

Una complicate sana maisha na yalivyo mafupi sasa !!
Its not worth it.
 
Haya yote ya nini kama siyo uturutumbi a.k.a uchawi???
 
Umesomeka ndugu. Kila jambo lifanyike kwa kiasi na kuwe na mipaka kwa kila jambo. Tusiishi kiholela kama mbwa koko.
 
Niko mbali na mama yangu nipigieni tu wakati wowote asije umwa nikashindwa kutima ka pesa ka kumuwahisha hospital kisa eti limiti ya kupiga simu nipigieni yu jamani.

Hata siku nikifa mnizike na simu yangu huwezi juwa ya huko mbinguni. Nikifika.mbinguni nimpigie shoga yangu alietangulia nimjulishe nimefika.
 
Mdogo wangu; umeandika mambo mengi lakini nina maoni machache kwako;

Kwako kuzoeleka na watu inamaanisha nini?

Nikuuibie siri kidogo; mazoea huwa hayaleti dharau; dharau huja kutokana na aina ya mazoea uliyonayo kwa watu/mtu.
Mtu akikuzoea na mkawa na mambo ya muhimu na yenye tija huwa anakuheshimu zaidi na sio kukudharau; maana atajua misimamo yako na namna ulivyo na uwezo wa kupima na kuamua mambo; ila kama unazoeana na mtu katika mambo ya kijinga/mizaha na hadithi za ujinga hapo dharau umeikaribisha mwenyewe.

Namna nzuri ya kuishi na watu ni kuzoeana kwa maana ya kutambuana na kujenga ukaribu; Kuna msemo wa miaka mingi ''Human being is a social being''.

Wapo watu wamezoeana na watu katika mambo stahiki na wala hawatakuvunjia heshima.

Watu ni mtaji; iwe mtaani kwako ama mahali unapofanya kazi; zoeana nao kwa heshima katika mambo ya maana.

Kuna misiba imesimamiwa na watu ambao sio ndugu wa marehemu kwa sababu ya ukaribu wa mtu kwa watu. Kuna sherehe zinafana kwa sababu ya mazoea na watu; mimi nimeshuhudia nikiwa nakuwa mtaani kwetu misiba kusimamiwa na majirani; mtu anafiwa na mtoto na hapa mjini yupo yeye na mkewe tu; lakini watu aliojenga nao mazoea ndio wanakuwa wa kwanza kufika na kusimamia shughuli nzima ya msiba.

Weka mipaka lakini usijitenge kwa vikanuni vya kujiona kuwa una taratibu zako za maisha, maisha hayatabiriki.

Katika maisha yetu ya Kitanzania; watu ni mtaji mkubwa sana kuliko elimu na hela zako; watu ndii hukukimbilia ukiwa na majanga iwe hospitali ama nyumbani; hawa ndio huweka turubai, huchimba kaburi na kubeba jeneza liwe la kwako ama la mwanafamilia wako.

Unaweza ukapata msiba huko mkoani aidha wa baba au mama na ndugu yoyote ; ukajikokota ukafika siku ya pili lakini utakuta watu wmeshaweka sawa mambo ya msingi; kuandaa mazingira na hata kuweka taratibu za msiba wakati wewe upo kwenye basi ukielekea msibani.

Mazoea ya dharau hayafai kabisa lakini ni muhimu kutambua umuhimu wa mahusiano na watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…