Mimi binafsi sipendi kuwaamini hawa wanasiasa wetu nasemaga kabisa niwachumia tumbo hasa hawa wanaojiita watetezi wa Wanyonge ( Wapinzani) hawana tofauti na Wanaccm labda tofauti yao kidogo ni rangi za uniform huwezi kwenye Hili ukakuta Wapinzani hawa wanatangaza kuingia barabarani kulazimisha hii tozo za miamala zipunguzwe zaidi utawasikia wanatishia kuingia barabarani kwenye mambo yanayohusu maslahi ya chama chao.
Pia huwezi kusikia wakiomba posho zao za kibunge zipunguzwe au utaratibu wa kutumia magari ya gharama ya serikali uondolewe ili isaidie serikali kupunguza matumizi makubwa na kutokana na Hili inapelekea Wanyonge kubanwa na kodi nyingi kama sehemu ya kufidia walipopunguza.
NB: Nawashangaa Sana watu kupigania hiv vyama au kutukana eti kwa mapenzi vya hivi vyama unaacha kupigania familia yako unawapigania watu ambao matumbo yao yameshiba sambusa, chips mayai si ujinga na ni uzezeta na ndio maana siwezi kuwa mashabiki wa chama chochote zaidi ya kuwa mshabiki wa Taifa langu la Tanzania