Kwenye mambo yanayohusu maslahi ya Wanyonge ni ngumu Sana kuwasikia Wapinzani

Kwenye mambo yanayohusu maslahi ya Wanyonge ni ngumu Sana kuwasikia Wapinzani

nadhani ni hivo!ukishajua kAzi ya mpinzani ni kupinga kile mtawala anachofanya ili aingie madarakani,na kAzi ya mtawala ni kutumia madaraka yake kubaki pale alipo,, utaachana na wanasiasa ,wew kuwa na misimamo yako binafsi ambayo inaleta manufaa kwa Tanzania,,endapo mtalingana kimawazo na mwanasiasa wa Upande wowote ,yote heri🤣
Hapo sawa tumesimama upande mmoja.,sikukuelewa mwanzo
 
Ukitaka kujua CDM ni kichaka cha wachumia tumbo na genge la utetezi wa mafisadi na mabwanyenye basi huu ndio wakati muafaka.

Nakumbuka wakati Hayati JPM anawapeleka mpera mpera matajiri walionyakua fedha za wanyonge Mbowe aliibuka kila kukicha kuwatetea "wafanyabiashara" wakubwa ambao wengi walikuwa wanakwepa kodi.

Mbowe akatuonesha kuwa kuwabana wafanyabiashara wakwepa kodi ni kukimbiza uwekezaji.

Sasa kibano kimehamia kwa wanyonge Mbowe kauchuna kimyaa na anakula bata Dubai kama kawaida baada ya kuwafitinisha kina Sabaya na jamii.
Brother mbona wajichanganya? Post nyingine una justify hizi tozo kwa kufananisha na kodi za US. Wakati huo huo wataka Mbowe awe na msimamo kinzani. Msimamo wako wa TOZO ni upi? Mijitu kama nyie ndio mwatufanya CCM tuonekane malofa kila kona.
 
Mimi binafsi sipendi kuwaamini hawa wanasiasa wetu nasemaga kabisa niwachumia tumbo hasa hawa wanaojiita watetezi wa Wanyonge ( Wapinzani) hawana tofauti na Wanaccm labda tofauti yao kidogo ni rangi za uniform huwezi kwenye Hili ukakuta Wapinzani hawa wanatangaza kuingia barabarani kulazimisha hii tozo za miamala zipunguzwe zaidi utawasikia wanatishia kuingia barabarani kwenye mambo yanayohusu maslahi ya chama chao.

Pia huwezi kusikia wakiomba posho zao za kibunge zipunguzwe au utaratibu wa kutumia magari ya gharama ya serikali uondolewe ili isaidie serikali kupunguza matumizi makubwa na kutokana na Hili inapelekea Wanyonge kubanwa na kodi nyingi kama sehemu ya kufidia walipopunguza.

NB: Nawashangaa Sana watu kupigania hiv vyama au kutukana eti kwa mapenzi vya hivi vyama unaacha kupigania familia yako unawapigania watu ambao matumbo yao yameshiba sambusa, chips mayai si ujinga na ni uzezeta na ndio maana siwezi kuwa mashabiki wa chama chochote zaidi ya kuwa mshabiki wa Taifa langu la Tanzania
Mbona unawasakama wapinzani kwani hujui kua bunge in LA ccm walaumu ccm ndo walotunga sheria kandamizi upinzani uliuwawa na watu walisema mathara take ndo haya
 
Walipokua bungeni wakipinga miswada mibovu na bajeti zisizotekeleza mlikuwa mnasema wapinga maendeleo sijui wasipewe mishahara maana wamepinga bajeti eti leo hii mnataka wapinge tena?

Walikua na platform bungeni mfano kikotoo cha mafao walikipinga bungeni kupitia mfumo rasmi na hoja ikaeleweka. Leo hii wametolewa bungeni mpo kimya then mnataka waje tena wapige kelele??

Watanzania tuache unafiki kama hamkuona faida yao then let them do their thing kufikia 2025 akili zitawakaa tu hamtorudia makosa.
Kwahiyo hoja yako ni ipi kwamba wametususia na tunastahili kususiwa ndio maana wako busy na kudai katiba mpya kwa masilahi yao ya kisiasa? au kwamba kwa sababu hawapo tena bungeni hivyo hawawezi kuwatetea wananchi wakiwa nje ya bunge?
 
Lkn mleta mada ana hoja. Kwamba wapinzani wanatuahawishi tupiganie tume huru kwasabb imebana mkate wao moja kwa moja. Kwann hawapambanii hili lililobana mkate wa wanyonge??

Wangeweza kuwashawishi wanyonge waingie barabarani ktk hili halafu wakachomekea na katiba mpya humo ndani wangeua tembo kwa ubua.
Kweny hili siwatetei CDM maan wapo mmoja mmoja kule Twitter walilalamika since day one, but kwann CCM hawalalamiki au kupaza sauti juu ya hili? Yaan hata kwa mmoja mmoja tu kamwe huez ona walilalamika?
 
Umeongea point sana nilitegea wapinzan kutumia mwanya huu kujijenga zaid nilitegemea wameita wandishi wa habar kulaani vikali nakuomba bei zirud kama mwanzo viongoz ni mpuuzi ntupu ( mzee mpili voice
Ingekua vyema ukawapasha hbr hasa wale waliopitisha hili kuliko kuwasakama wale ambao hata hawahusiki kulipitisha hili. Yaan wengine watengeneze tatizo then lawama watupiwe wengine? Think about it!!
 
Hao ni mawakala wa mabeberu,

Hitaji lao ni kupata nafasi ya kutawala tu Ili washirikiane na mabeberu kutuchuna ngozi, hawana jingine.

Angalia wanachokidai, "tume huru ya uchaguzi".

Lisu mwenyewe kwenye kampeni alitoa proposal ya kuwakabidhi mabeberu rasilimali zetu halafu wao watupe fedha za maendeleo, utaona ni namna gani wanatumwa walete Ajenda toka Kwa ngozi nyeupe.

Watanzania tunalo , kama sio ngozi nyeupe basi ni macho madogo.
 
Mimi binafsi sipendi kuwaamini hawa wanasiasa wetu nasemaga kabisa niwachumia tumbo hasa hawa wanaojiita watetezi wa Wanyonge ( Wapinzani) hawana tofauti na Wanaccm labda tofauti yao kidogo ni rangi za uniform huwezi kwenye Hili ukakuta Wapinzani hawa wanatangaza kuingia barabarani kulazimisha hii tozo za miamala zipunguzwe zaidi utawasikia wanatishia kuingia barabarani kwenye mambo yanayohusu maslahi ya chama chao.

Pia huwezi kusikia wakiomba posho zao za kibunge zipunguzwe au utaratibu wa kutumia magari ya gharama ya serikali uondolewe ili isaidie serikali kupunguza matumizi makubwa na kutokana na Hili inapelekea Wanyonge kubanwa na kodi nyingi kama sehemu ya kufidia walipopunguza.

NB: Nawashangaa Sana watu kupigania hiv vyama au kutukana eti kwa mapenzi vya hivi vyama unaacha kupigania familia yako unawapigania watu ambao matumbo yao yameshiba sambusa, chips mayai si ujinga na ni uzezeta na ndio maana siwezi kuwa mashabiki wa chama chochote zaidi ya kuwa mshabiki wa Taifa langu la Tanzania
Kama ni hivyo unaweze usiwe sawa,na watu jamii hii yaweza kuwa ndio sababu ya mkwamo huu tunao uona kwenye taifa letu.
 
Hao ni mawakala wa mabeberu,

Hitaji lao ni kupata nafasi ya kutawala tu Ili washirikiane na mabeberu kutuchuna ngozi, hawana jingine.

Angalia wanachokidai, "tume huru ya uchaguzi".

Lisu mwenyewe kwenye kampeni alitoa proposal ya kuwakabidhi mabeberu rasilimali zetu halafu wao watupe fedha za maendeleo, utaona ni namna gani wanatumwa walete Ajenda toka Kwa ngozi nyeupe.

Watanzania tunalo , kama sio ngozi nyeupe basi ni macho madogo.
Sasa bora yupi,wakala wa uwasemao ama wakala wa shetani.
 
"bora wapinzani walikosa ubunge....wangetuchelewesha kufikia maendeleo...bunge zima tumelishika sisi ccm..". lilisikika taga moja.
 
"bora wapinzani walikosa ubunge....wangetuchelewesha kufikika maendeleo...bunge zima tumelishika sisi ccm..". lilisikika taga moja.
Wao wanasikika tu kwenye unyongaji wa wanyonge ,ila sii kwingineko.
 
Chawa kutoka wasafi naye anafungua uzi wa kuwananga wapinzani..and we all know ni kwa sababu ya zile kunguni zilizosagwa kuhusu BET.
 
Chawa kutoka wasafi naye anafungua uzi wa kuwananga wapinzani..and we all know ni kwa sababu ya zile kunguni zilizosagwa kuhusu BET.
Wasitake tukawageukia tena,hasira zetu kwao bado kuisha.
 
Unaandika huu upupu kwa sababu CCM haijakutia sawasawa.The worst is yet to come.Subiri CCM itakutia sawasawa na utatoka huko mafichoni na kauli mpya ya kukanusha kauli hii.
 
Mimi binafsi sipendi kuwaamini hawa wanasiasa wetu nasemaga kabisa niwachumia tumbo hasa hawa wanaojiita watetezi wa Wanyonge ( Wapinzani) hawana tofauti na Wanaccm labda tofauti yao kidogo ni rangi za uniform huwezi kwenye Hili ukakuta Wapinzani hawa wanatangaza kuingia barabarani kulazimisha hii tozo za miamala zipunguzwe zaidi utawasikia wanatishia kuingia barabarani kwenye mambo yanayohusu maslahi ya chama chao.

Pia huwezi kusikia wakiomba posho zao za kibunge zipunguzwe au utaratibu wa kutumia magari ya gharama ya serikali uondolewe ili isaidie serikali kupunguza matumizi makubwa na kutokana na Hili inapelekea Wanyonge kubanwa na kodi nyingi kama sehemu ya kufidia walipopunguza.

NB: Nawashangaa Sana watu kupigania hiv vyama au kutukana eti kwa mapenzi vya hivi vyama unaacha kupigania familia yako unawapigania watu ambao matumbo yao yameshiba sambusa, chips mayai si ujinga na ni uzezeta na ndio maana siwezi kuwa mashabiki wa chama chochote zaidi ya kuwa mshabiki wa Taifa langu la Tanzania
Mbwa nyie, si mlibinuka binuka kwa filimbi na vinubi pale bajeti ilipokuwa ikisomwa na mlikuwa mnasema wapinzani hupinga kila kitu? Yamewafikeni sasa mbwa nyie mjue kuwa wapinzani wanamaanishaga nini wanapopinga vitu. Huwezi kuelewa uzito wa tatizo mpaka tatizo lenyewe likufike. MATAGA yamewafika sasa mnawaomba wapinzani wapaze sauti, paza sauti na mamako waacheni wapinzani wapumue sasa!
 
Lkn mleta mada ana hoja. Kwamba wapinzani wanatuahawishi tupiganie tume huru kwasabb imebana mkate wao moja kwa moja. Kwann hawapambanii hili lililobana mkate wa wanyonge??

Wangeweza kuwashawishi wanyonge waingie barabarani ktk hili halafu wakachomekea na katiba mpya humo ndani wangeua tembo kwa ubua.
Mlituaminisha kuwa wanyonge hawaitaki katiba mpya wanataka uchumi kwanza. Waambieni walipe kodi uchumi upae
 
Mimi binafsi sipendi kuwaamini hawa wanasiasa wetu nasemaga kabisa niwachumia tumbo hasa hawa wanaojiita watetezi wa Wanyonge ( Wapinzani) hawana tofauti na Wanaccm labda tofauti yao kidogo ni rangi za uniform huwezi kwenye Hili ukakuta Wapinzani hawa wanatangaza kuingia barabarani kulazimisha hii tozo za miamala zipunguzwe zaidi utawasikia wanatishia kuingia barabarani kwenye mambo yanayohusu maslahi ya chama chao...
Haya maneno yanaoonyesha nawe ni mmoja wa wafuasi wa CCM, kwa sasa mliamua kuwa na Bunge la kijani na Mabaraza ya Madiwani ya Kijani ili mlete maendeleo kwa kuwa wapinzani walikuwa wanachelewesha maendeleo.

Maendeleo tumeanza kuyaona kwa kasi ya kuongeza kodi kwenye pembejeo, tozo kwenye miamala ya simu, Kodi ya majengo kupitia ununuzi wa luku za umeme bila kujali kuwa wananunua umeme ni wapangaji katika nyumba au ni mmiliki wa nyumba nk.

Tungekuwa na Bunge lenye Wabunge wa Upinzani wengi hakika mambo haya yasingepita kabisa, lakini sasa tunaendeleza ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI. Namalizia kwa kusema sasa TWASOMA NAMBA WOTE KWENDA MBELE
 
Wapinzani walipoitisha maandamano ya kupinga uchaguzi wa mwaka Jana, wanyonge tuliwambia waache kutuharibia nchi yetu. Leo tunataka nini tena jamani. CCM wako sawa wanataka kutujengea madarasa ambayo wameshindwa kutujengea tangu Uhuru.

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom