Kwenye mkataba nimemwandika kama mrithi Ila yeye kamwandika baba yake

Suala la nani atarithi nani harithi mali za mtu ni la kisheria. Ukiwa hai unaweza kutoa baadhi ya mali zako kama zawadi kwa uwapendao. Lakini once ukifariki mirathi yako haitajalisha kuwa kule kazini nani alikuwa listed kama mrithi.

Mtu anaweza kumuondoa mtu kwenye mirathi yake kwa kupitia wosia..tena atoe sababu za msingi sana ambazo mahakama itazikubali.

Kisheria mume ana haki ya kurithi mali ya mkewe, awe ameorodheshwa kazini kwenye hiyo mikataba au la. Hawezi kunyimwa haki hiyo ya kurithi simply because mkewe hakumuorodhesha kama warithi wake.

kwenye kugawa mali za marehemu, msimamizi wa mirathi anaongozwa na sheria mbalimbali ikiwemo za kidini, kitamaduni na za bunge.
 
Kuoa siku hizi ni fashion tu na wala siyo lazima.Ndoa za mikataba ndio wakati huu sasa siyo eti hadi kuzikana.Watu mmekutana kila mtu ana meno 32 eti hadi mzikane? Hakuna kitu kama hicho
 
Yani ww na mkeo mnacheza makida. Mmoja akifa hata kama kamwandika sijui ni mzazi wake, jua kabisa atajayepata % kubwa ya mali ni mwenzi mume au mke, watoto wa marehemu wana % zao wazazi wa marehemu nao wana %zao japo sio kubwa. Na wala sio lazima eti mtu aliyeandikwa ndio sijui apate vitu halafu mwenzi aliyebaki asipate haki yake simply kwa sababu hakuandikwa kwenye karatsi la kazini. Yani mali mnayotafuta kwenye ndoa ni ya wanandoa. Sijui kwa nini wanandoa wanapenda kuleta sintofahamu kama hizi za mke wa mtoa mada.
Kama unaona mume au mke hafai kupata jasho lako ebu achaneni kwa talaka mgawane mlichovuna ndio utakuwa umemtoa huyo mwenzi kwenye vitu unavyoendelea kutafuta.

Utakuta eti mtu ananunua hata nyumba anamwandika mama yake. Mama yako akitangulia kufa ujue hiyo nyumba ni ya familia. Yani mumewe kama yupo na watoto(kaka na dada zako) na wazazi wa mama kama wapo. Huwezi kuiclaim hata kama upo. Labda familia ikuhurumie. Vinginevyo utaanza upya kununua kiwanja chako.Kama humwamini mtu usiingie naye kwenye ndoa. PERIOD
 
Usiumize Sana kichwa.
Kamfute yeye weka ndugu yako.
Mali za mume huwa ni za mke na watoto.
Ila za mke huwa ni zake na ndugu zake.
Kwenye priority ya mwanaume iko hivi;
Mume
Mke
Watoto
Ndugu wa mke
Ndugu zako.

Lakini mke huwa iko hivi;
Mke
Watoto wake
Ndugu zake
Mume.
Marafiki
Majirani
Ndugu zako.
Huna nafasi yoyote kwa mkeo.
Kula raha tu duniani humu.
 
Jamaa kapaniki. Sijawahi weka mwanamke katika kipengele hiko. Anyway mali ya mwanamke siku zote ni yake.
 
Mkuu ukiwa na mtazamo huu, ndoa haitofika mbali.

Lazima kuwe na kushirikishana katika hayo, mfanye maamuzi kwa pamoja.

Ukiangalia hapo, mtoa mada kasema wazi walishakubalia nini cha kufanya, ila mke kaleta janja janja na kumzunguka jamaa.

Hilo tu linaweza leta mpasuko sababu hakuna uaminifu hebu.

Swali kwa mtoa mada: ilikuaje ukapata wazo la kukagua karatasi yake? Ana historia ya janja janja?
 
Ushawishi utakao pelekea singo maza mwingine kuzalishwa
 
Mmmh unauwakika
Ni kweli kama familia ya mwanamke wana uchumi mzuri mwanamke hawezi kuandika urithi majina ya wazazi wake na hivyo hivyo kwa upande wa familia ya kiume, Umasikini ndiyo chanzo cha mambo yote, tatizo linaanzia kwa wazazi wetu kuwa masikini wa kipato hawana uwezo wa kujihudumia mataji muhimu na kutokuwa na uzazi wa mpago utakuta mzee ana miaka 50 bado ana majukumu yakulea familia, kumbe ange zaa kwa mpango watoto watatu au wa 4 wa ngekuwa wana jitegemea na mzazi ana kuwa hana majukumu zaidi ya majukumu ya yeye mke wake na wangepata nafasi ya kutembea kwenye vivutio vya kitalii, Sasa wa zee weu utakuta mpaka ana kufa hajawahi kutoka mkoa anaoishi.
 
Nikifa mali anaanza mke, watoto halafu wazazi wangu kama wako hai.
Akifa mali zake naanza mimi, watoto halafu wazazi wake.
Ndio maana ya kuwa mwili mmoja!!!!! Na kwa mazingira yetu vya kurithi si vingi!!!! Msivurugane kwa sababu ya mirathi furahieni maisha maana ni mafupi mno! Hujakaa sawa umegonga 50 na ndio kwa heri kwa wastani wa kuishi kwa Mtanzania.
 
Duh haya Maisha tunatofautiana sana, hakika nimekuja kugundua wanawake wa kuoa Ni wanyakyusa , Ni watiifu sana kwa waume zao na wanapenda sana kutengeneza familia , no matter Ana pesa kiasi gani, Nina mifano miwili niliyoshuhudia , wa kwanza Ni kwa mke wangu, yeye hata kadi ya benki hajui iko wapi, na sifahamu Mara ya mwisho kuishika ilikuwa Ni lini, maana Mimi ndo naimiliki, Wala sio kwa ubabe wangu, la hasha ni mahaba na utashi wake.

Mfano wa pili ni mwanamke ambaye Ni office mate wangunaye Ni mnyakyusa, anampenda sana jamaa yake(mme,)licha ya kwamba mme wake ni mtu wa vidosho, lakini huwezi mwambia amuache, kaenda benki kachukua mkopo na kumnunulia pikipiki ili Bwana mkubwa alilaksi,na hapa Naona kachukua Tena mkopo wanajenga

Sasa Mimi huwa nashanga watu wanaosema kuooa wanawake wafanyakazi Ni changamoto, Mimi has sio kweli, Bali inategemeana na Sina ya mwanammke uliyenaye


Pongezi ziende kwa mabinti wa kinyakyusa!!!!
 
Wanawake wa kaskazini ndiyo wana fanya wanawake waonekane wabinafsi.
 
Hata kama mume hajaandikwa, mje akifa hela za NSSF au PSSF anapewa mumewe. Halafu mmojawapo akifa kama hajaandika wosia rasmi hayo makaratasi ya ofisini wala hayatumiki, watafuata sheria ya murathi etc
 
Sio wanyanyakyusa tu, mimi nelelewa kwenye familua baba na mama wanashirikiana, na sisi ni hivyo hivyo. Hakuna cha mwanaume eti yeye ndio kila kitu. Mwanaume anapata mshahara laki 3 au 5 kwa mfano kwa mwezi , kumtegemea yeye ndio kila kitu hamtakaa muendelee. Nyumba nzuri, gari etc mtaishia kuona kwa wenzenu
 
Next of kin, kwenye taarifa zako za kidigitali inamaanisha "mtu wako wa karibu anayeweza kupokea taarifa zako kutoka kwa mwajiri au kutoa taarifa zako sahihi kwa mwajiri wako pindi pale panapotokea hitaji la lazima au dharura"
*msimamizi wa mirathi anayetambulika ukipiga chini ni yule aliyeidhinishwa na kikao cha mirathi/kisheria ...

Sasa labda hadi kumfikia msimamizi wa mirathi kisheria, huyo next of kin anaweza kuact kama daraja kwa njia moja au nyingine..

Take a chill pill bro, INGAWA SITUATION YAKO INAKUALERT UKAE KIMACHALE NA MWANANDOA MWENZAKO
 
Usiwaze Sana urithi maana wanaume Kwa % kubwa hutangulia mbele ya haki.
 
Hapo umepigwa mkuu. Chunguza vizuri huenda hata watoto siyo wa kwako. Lakini kabla ya hatua hiyo, muulize kwanza usikie maelezo yake
 
Nenda uombe mkataba wako ufanye amendment kidogo na wewe badilisha weka hata mdogo wako tena wifi yake.

Ngoma iwe draw, wanaita Ngoma ngondoigwa
Huku kukomoana ni kutesa watoto lofoten likitokea. Ni mara chache sana watoto kupata haki zao pindi mzazi anapofariki.
Afanye chochote lkn ahakikishe kuwa siku hayupo watoto wake watapata haki yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…